Jumanne, 31 Januari 2017


*TUMETOKA MAUTINI TUMEINGIA UZIMANI.*                   
1YOH 3:13-14. Ndugu zangu tumetoka kwenye mauti tunangia uzimani.


Aidha SADAKA maalumu ya Leo niya kuondoa mauti kutuingiza uzimani.
Kufuta mauti yote ndani ya kanisa na kizazi cha MUNGU.
Ya kutoka kwenye mauti na kuingia uzimani.
Leo kanisa limetolewa mautini na kupelekwa uzimani.
Sisi tunajua ya kwamba tumepita toka mautini na kuingia uzimani.
Ni kituo kipya tumeingia kanisa cha kufutiwa mauti zote na sasa tumeingia ktk kituo cha uzimani.
Kituo hiki hakuna amchukiaye ndugu yake kwa kuwa amchukiaye ndugu yake ni muuaji.
Kituo tulichofika hakuna mauti MUNGU ametimiza NENO lake.
Agano la kichwa kanisa leo ni agano la Uzimani, ni la kutoka mautini kuingia uzimani.
Agano hili halitakaa lipate shida milele.
Agano hili limefutiwa kifo na mauti.
Agano hili limebarikiwa na MUNGU laana hazitakuwepo.
UFUNUO 20:6 huu ndio ufufuo wa kwanza sisi ni makuhani wa MUNGU na KRISTO wake.
Mahali hapa mauti ya pili haina nguvu tena.
KUNA TOFAUTI KATI YA MAUTI NA KIFO;
Mauti ya pili unatembea lakini vitu vyako vyote vimeibiwa/ vimekufa.
Kutembea ukiwa huna mikono kwa maana ya kila unachofanya kufa.
Huna akili ya MUNGU, ufahamu.
Huna agano la kichwa kanisa japo kuwa tunaona unaishi na kichwa wako na watoto unao lakini huna uzima.
Yaani hapo unatembea nafsi yako ikiwa kaburini ilishazikwa umebakiwa na roho tu ndio inadunda.
Lakini leo hatuna mauti tena maana tunatawala na kristo na tunamilikiwa na MUNGU mwenyewe.
MWANZO 2:17  walaikini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
MWANZO 3:6  akaona ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, wa utamanika kwa maarifa ….
Siku zote vitu vya kerubi huwa vinaushawishi urahisi wa wewe kuvipata lakini ndio unaangamia hivi hivi.
Unaibiwa nafsi yako kizembe , unauza thamani yako kwa vitu visivyokuwa na faida.
Vinakupa majuto makubwa mno ya muda mrefu, kitendo cha kuhiari kuwasikiliza walioshindwa waliofeli, walioasi, …. Tu!
Unaangamiza maisha yako yote, uzao wako ulionao na utakaokuja baada yako.
Unafuta yale yote ambayo MUNGU alikusudia kwako.
Leo umeingia kituo cha uzimani acha kusikiliza taarifa za wajinga.
Moyo mmoja wa kanisa umepokea na ndipo huo uzima unakaa.
Badilika geuka acha njia ambazo zinasababisha urudi nyuma.
MUNGU anapowaadhibu waliokuwa wanakutesa usiwaonee huruma maana yeye MUNGU amekusamehe, amekutakasa, amekuvika vazi jeupe, amekugharamia kwa ajili yake yeye mwenyewe.
Achilia sahau ili MUNGU aingie kazini mwenyewe wewe mwenyewe huwezi kujitetea na huwezi kupata haki yako.
MWANZO 5:3 Kuuza mtoto wa kufanana naye badala ya mtoto wa kufanana na MUNGU.
Je hujawahi kuona mtu anaumwa mpaka anaanza kuoza ile ni mauti ina maana huyo mgonjwa mauti ilishamvaa kinachosubiriwa hapo ni kifo japo anaongea.
Hayo yote ni kwa sababu ya kutokuwa na utii katika yale ambayo MUNGU alisema nao wakashindwa kuwa na umoja wa MUNGU.
Ubinafsi ndio ambao ulisababisha kuzaa wa kufanana nae badala ya kufanana na MUNGU.
Kutokuwa na moyo wa toba na unyenyekevu, kuwasukumia wengine mabaya badala ya kutubu.
Leo tunaishi na tunatembea na MUNGU hivyo mauti ya pili haipo ndani ya agano, biashara, kazi, familia, pia kila utakachoanzisha kitaleta faida.
Kizazi hiki cha MUNGU KRISTO NA KANISA hakuna mauti milele.
1KOR 15:20-28 sharti amiliki yeye aliyevitiisha vitu vyote chini ya miguu yake.
Adui wa mwisho aliyebatlishwa ni mauti, hatutaishiwa maana hatuna mauti. Limbuko ni kristo na msingi uwe ni kristo, maana mwisho naye tumeupata.
MUNGU amesema hatoki kwetu lakini hawezi kukaa mahali penye mauti.MUNGU hawezi kutawala na aliyevikwa vazi la mauti.
KRISTO kz4 alisema iko majira inayokuja ambayo MUNGU mwenyewe atakuja.
Kwenye dini hawakufundisha kwamba MUNGU atakuja ila walitufundisha kwamba yesu atakuja.
Sasa MUNGU amekuja mwenyewe na mwana amemtiisha chini ya miguu yake ili MUNGU awe yote katika yote.
EFESO 1:9-10  Atajumlisha vitu vyote vilivyo mbinguni na vilivyo duniani view vya kwake.
Hii ni majira ambayo MUNGU hakai mbinguni tu bali anakaa katika nchi, anatembea katika nchi, anatawala katika nchi.
MUNGU amekuja kumiliki.
MATHAYO 21:33-43  Amekuja kuangamiza vibaya wabaya wote.
Taifa lenye kuzaa matunda limepatikana, ni taifa la Gosheni ambalo ufalme wa MUNGU.
YOHANA 19:1-18  Ukiona agano /ndoa yako ina migogoro ujue kwamba mauti imeingia.
Yesu alivikwa vazi la mauti, zambarau.
Wakaanza kumpiga mateso kutemewa mate nk ukiwa na vazi la mauti huwezi kupata haki yako.
Pamoja na kuwa hujatenda dhambi ulikuwa unauawa kwa sababu una vazi la mauti.
Mwenye haki hata kama hana kosa alikuwa anasingiziwa uongo ili mradi tu achukiwe afukuzwe kazi
Kwa kuwa mauti imefutwa hakutakuwa na mateso milele.
Pilato hakuona kosa kwa Yesu lakini alishindwa kumsaidia kwa kuwa alikuwa amevikwa vazi la mauti.
Tunamshukuru  MUNGU kwa kuwa sasa kweli imesimama, pilato nae anajua kweli na mwenye haki hataonewa tena.
YOHANA 18:37 kizazi kile pilato hakuijua kweli,alikuwa ni mkubwa serikalini lakini hakujua kweli.
Ndio maana tumetoka mautini na tumeingia uzimani kwa kuwa kweli imesimama.
Wote walikuwa ndani ya kizazi cha MUNGU, vazi la mauti limeondolewa kwao.
LUKA 1:45  Heri aliyesadiki haya yote aliyoambiwa na BWANA maana yatatimizwa kwake yote aliyoambiwa na BWANA.
Unaweza kujiuliza kwa nini tunavaa pete mkono wa kuume ZABURI 45:6
Mabinti wa wafalme wapo pamoja na wameketi mkono wa kuume.
MWANZO 48:1-  Efraimu alikuwa mdogo lakini alikuwa au aliwekwa mkono wa kuume, wakati wa kubarikiwa kwake.
Efraimu maana yake kanisa.
MHUBIRI 10:2 MOYO WA MWENYE HEKIMA UPO MKONO WA KUUME.
Lakini moyo wa mpumbavu upo mkono wa kushoto.
Kanisa tunawavika mabibi harusi pete mkono wa kuume kwa kuwa twajua tufanyacho.
Yusufu alipoona Efraimu amewekwa mkono wa kuume na ni mdogo, Yusufu alisema sio hivyo baba baba yangu…. Israeli akasema nyamaza kimya najua mimi najua.
Kuanzia leo umepokea kuishi uzimani siku zote, usisikilize sauti yoyote kinyume na NENO linatoka madhabahuni.
Tumepokea agano la kutembea na kuishi  na MUNGU uzimani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni