Jumanne, 24 Januari 2017


KWELI IMESIMAMA    KWA UHALISI

Tunashukuru MUNGU kwa sababu sasa Kweli imesimama kwa uhalisi. Kweli ilipotoshwa tangu UF12:1 alipo wa na Kanisa akatokea mwanamke [photocopy].
Tangu mlimani na vizazi vyote vinne kweli ilikataliwa kulikuwa na uongo na alifutwa jana. Mbinu za uovu zilizokuwa zinasumbua wenye haki  zimefutwa.
Tangu siku ya kwanza MUNGU alipoumba mbingu na nchi na kisha kuwakabidhi shamba wakulima kweli haikukubaliwa ilikataliwa.
YOHANA 19:1-20 PILATO alikubali kwa sababu kweli haikuwepo. Damu ya kweli kufuta uongo na ukweli.
Shinikizo limesababisha wengine watoke mahali pao.
Kuna waliofukuzwa kwenye agano lao, leo kiapo kimesimama; kuvunjwa kwa agano la kwa uongo.
Yeyote aliyekuwa anachukua nafsi za wenye haki na kuzitumia kinyume leo ndio mwisho wake.
*MBINU 3 WANAZOTUMIA MASHETANI*
Kwa nini mwenye haki anaadhibiwa?
1.)Muovu kuingia ndani ya nafsi ya mwenye haki na kutenda dhambi.
V Unajikuta unafanya kitu cha ajabu mpaka wewe mwenyewe unajishitukia unajishangaa kwa yale unayoyafanya.
Kuna wakati unajikuta unajiuliza maswali kwamba hivi ni mimi ninayefanya haya yote kumbe ni kutokana na Yule muovu aliyeingia kwenye nafsi yako.
Hali hii ya muovu kuingia ndani ya mwenye haki na kutenda mabaya kinyume na MUNGU kinyume  na Neno ni mwisho.
2.)Muovu kuingia ndani ya bosi wako , mzazi, mlezi, mwanao nk ili kuharibu uhusiano mzuri uliokuwepo kati yenu leo ni mwisho.
Unakuta bosi wako kwa ghafla kabadilika mpaka anatamani akufukuze kazi na wakati mwingine unajikuta unatamani usaini kuacha kazi kumbe ni adui leo ni mwisho.
Mlima wa moto unakutana na watoto ukiwaambia msifanye msiangalie tivi kabla ya kupika unakuta wameangalia mpaka wameunguza karamu.
Kijana, binti unajikuta mzazi wako kila ukipika anakuambia karamu gani hii umepika mbaya namna hii na amekula amemaliza kushiriki leo njia zote za adui kuharibu uhusiano mzuri na madhabahu yake imefutwa milele.
3.)Kuvalishwa mavazi mabaya ya waliokufa, uchawi, uganga, uloz, unajimu, hasara, kudharauliwa, leo yamefutwa.
Haya mavazi yalisababisha hata ukisema kweli ikataliwe leo ni mwisho.
Leo ukisema  kweli na kuonekana kuwa ni mchawi ni mwisho.
Wakili wa MUNGU anapokupa vazi lake ujue kwanza umepokea mafuta yake.
Hii nguvu wachawi walichukua na kuligeuza wenye haki kuonekana wachawi waovu leo mwisho. YOHANA 8:1-
Tabia ya kutafuta kumuua WAKILI WA MUNGU kila siku ni kwa sababu  NENO LA MUNGU halikuwepo halipo ndani yao.
Utasikia sisi ni wa Ibrahimu, Eliya mtishibi, Yesu, Eiya Ad2 lakini wanayofanya hayafanani nao ambao wanawasema ndio sababu Yesu mwasema ninyi ni wa baba yenu Ibrahimu;
Mbona mnayotenda hayafanani na huyo Ibrahimu, Eliya Ad2 maana hata wao wangekuwepo wasingefanya hayo mnayoyafanya leo kwa Wakili wa MUNGU.
Hata wakati wanaongoza vizazi hawakuwahi kumshitaki yeyote, hawakumtukana yeyote, hawakumkosoa MUNGU milele. Nyie mmetoa wapi?
Aliye wa MUNGU husikia na kuyajua yaliyo ya MUNGU na kuyelewa sasa mbona WAKILI WA MUNGU anasema yaliyo ya MUNGU lakini hamuelewi, mnamshitaki  MUNGU.
Ukisoma haya mazungumzo yaliyopo yohana 8 utajua kuwa kweli ilikataliwa siku zote hizo.
Hawataki kweli utasikia wanasema WAKILI tunampenda lakini mafundisho yake hatuyataki tunayataka yale ya baba yetu Ibrahimu,
Eliya Ad2, kizazi cha tatu walikataa mafundisho ya Yesu wakataka ya Ibrahimu yaani mafundisho ya kabla hata ya majira ya 3 ya kizazi cha 1.
YOHANA 19:1-20 Pilato naye hakuijua kweli japo alitamani alipenda kumtetea YESU ktk majira ile lakini haikuwezekana kutokana na kutoikubali kweli.
Kanisa tuna haja ya kumuomba MUNGU kweli kweli ili Pilato ajue kweli na aikubali. Leo tunaipeleka kweli kwa pilato.
Mpaka sasa serikali haina shida na kanisa na WAKILI WA MUNGU shida ipo kwa wale wanaopeleka taarifa za uongo, barua za masingizio, mashitaka ya uongo, michoro ya mabaya, ramani mbaya  leo tutubu.
Leo kwa sababu kweli imesimama mashitaka yote yamefutwa kwetu milele.
Mashitaka ambayo MUNGU, Kristo Wakili wa MUNGU Kanisa na Taifa wameshitakiwa leo yamefutwa milele.
Nira zote kamba zote zilizokuwa zimetufunga leo zimefutwa milele. Kizazi hiki pilato lazima aijue kweli ili mashitaka yote yaondolewe kwa YESU.
Maagano ya kichwa kanisa yaliyo haribiwa na kahaba leo yamerejea kwenye kusudi kwa sababu kweli imesimama leo.
Kesi za masingizio zimefutwa ila kama ulikuwa na machungwa ya watu kweli nenda ukaseme kweli kwa kuwa kweli imesimama yenye kukuweka huru. Vifungo vyote vimeng’olewa milele.
Roho za masingizio zimefutwa, kuanzia leo utaaminiwa kila akuonae ataona wema wako ulioutenda, uadilifu wako utaonekana, ukifanya kazi utalipwa kwa haki maana kwa kuwa sasa kila utakapofanya kazi utakapoonekana utakuwa KEKI kwenye wajibu wako mlima wa moto, biashara zako.
Kila kazi unayofanya ulikuwa unadharauliwa kuanzia leo utathaminiwa.
Sasa kama ulifanya biashara lakini ikakataliwa leo kaianzishe tena utafanikiwa itakubalika itapendwa itakimbiliwa utaitwa kwenye tenda mbalimbali.
SADAKA maalumu ya leo ni kufutwa kwa mavazi ya mambo mabaya yote, kutokuwa na thamani katika kila kitu unachofanya.
Kusimamisha Kweli ili kuunguza mavazi ya maneno mabaya yote kwa sadaka hiyo.
Pia Sadaka hiyo maalumu inafuta usingiziaji kwa maneno yote ya uongo na mavazi ya usingiziaji kwa wenye haki. 
Kufuta laana zisizo na sababu, kituo cha kufanya kazi kubwa bila malipo.
Mashitaka yaliyokuwa yamepelekwa kwa pilato yamefutwa.
Uongo uliokuwa umeenezwa kwa ajili ya Kanisa umefutwa kwa sadaka. Pilato + kaisari wataijua kweli kwa sadaka hii.
Mavazi aliyokuwa amevalishwa pilato asiijue kweli leo yameuungua yamefutwa kwa sadaka sasa ataijua kweli moja halisi.
*MCHUNGAJI MMOJA MWEMA NA AKUKUTE KWENYE KWELI SASA ILI APATE KUKUCHUNGA.*

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni