Ijumaa, 6 Januari 2017



THAMANI NA FAIDA YA KUISHI JUU YA UMBO

Umbo la nyoka lililowahi kuwepo katka mlima wa BWANA na Bustani ya Edeni lilikuwa likisimamisha anguko likisababisha anguko kila wakati lakini sasa halitasababisha anguko tena milele.

Sasa tutatembea na MUNGU pasipo kukosea na kila ambacho MUNGU ameahidi sasa tutaona MUNGU akitenda kwa uhalisi hakuna atakayeiba milele.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo aliongoza wenye haki kutoa Sadaka Maalumu ya Mhubiri 10: 5-7 ambayo ni sadaka ya kila mmoja kusomeka kama alivyo mwenye haki atasomeka kuwa ni mwenye haki na mwovu atasomeka kuwa ni mwovu maana chujio la haki namba 3 limesimama.

Kanisa litasomeka vizuri na watagundua kuwa linaombea jamii, taifa na wote.

Wakili wa MUNGU amesema kuishi juu ya umbo faida yake ni pamoja na kila unapotoa kiongezeka kwa uhalisi yaani kila kitu kitakuwa kinaongezeka zaidi sawa na kituo kanisa tulipo mahali pa uhalisi wa kila kitu.

Umbo ndilo lilikuwa linasababisha thamani ya vitu vizuri ninavyotamkiwa kutotokea leo chagua kuishi juu ya umbo uone vitu vizuri vinavyotokea kwa uhalisi.

Aidha Wakili wa MUNGU ametoa ushuhuda wa baada ya kumtoa falasi wa moto wa makusudi ya MUNGU amepata falasi mwingine siku hiyo hiyo.

Ikiwa ni pamoja na baada ya kutoa fedha za kununua taili kwa jeshi la polisi mkoa katika kijiji cha nguruka mkoani kigoma amepata kamera mbili mpya za video na mnato za thamani ya mamilioni ya fedha.

Hata hivyo ametaka wenye haki kuishi maisha ya zaidi ya mtoto mchanga ambaye hajui kitu kingine zaidi ya kujua kunyonya na kusinzia huku akijua akiamka maziwa yapo na sio yakutafuta.

Yaani anaponyonya akasinzia akiamka anayakuta maziwa yameongezeka na kusema haya ndio yatakuwa ni maisha yetu ikiwa nitaishi juu ya umbo.

Amesema nitapokea maongezeko hayo iwapo nitakubali kutoka kwenye umbo la:-
*Nyoka
*Mnyama
*Ukoo wa baba, mama.
*Kabila
* lugha
*Jamaa
*Mila na desturi.
*Tabia ya asili.
*Sheria ya dhambi.
*Matendo ya mwili
*Tabia ya kinyonga.
*Mwanamke.

Amesema kinachotuponza ni kuuliza maswali kwa waliofeli na walioshindwa badala ya kutafuta ushauri madhabahuni, tutafute faida madhabahuni, tuisikie sauti ya madhabahu.

Awali akianza ibada hiyo Wakili wa MUNGU amesema kuwa ilikuwa mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe lakini sasa mti wenye matunda ndio unaolindwa badala ya kutukanwa sasa unaheshimiwa.
Wakili wa MUNGU Kizazi cha MUNGU akifafanua Neno

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni