KUFUNULIWA KWA KANISA AMBALO NI UMOJA NA MUNGU NA KRISTO MILELE
Kiti cha MUNGU, Meza ya MUNGU na fimbo ya MUNGU vimerejea ndani ya kanisa (Mlimani kwa MUNGU).
Akijenga msingi wa Ibada hiyo Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu inayonipa kuketi pamoja na MUNGU nikiwa namilikiwa na (Baba, Neno, Roho na Kanisa) iliyounganishwa na hakika ya NENO na Heshima ya NENO.
Neno lililozuia nisipotee lipo ktk 2 wafalme 5:20-26.
MUNGU anatuona lakini tumekuwa tukimdanganya Wakili wa MUNGU nakakwamba hatuoni kila tunapokuwa.
Amesema dunia imetengeneza makuhani wamdanganye Wakili wa MUNGU ili alie lakini Wakili wa MUNGU halii.
MUNGU nakushukuru kwa kuwa umoja wako umeonekana ndani yangu kila mahali nitakapokuwepo.
Umbo la kizazi cha kwanza ni manung'uniko, malalamiko, vilio na kumchukiza kiongozi.
Umbo la kizazi cha pili ni kufundishwa kweli na kuikataa na kuvunja madhabahu ya MUNGU.
Umbo la kizazi cha tatu lilikuwa ni kuendelea kukataa yale yanayofunuliwa kama ilivyokuwa katka Yoh 6:30- hasa kilichosababisha kutopokea ufunuo ni tabia ya mwili.
Umbo la kizazi cha nne lilikuwa la tabia za vizazi vyote kuanzia kizazi cha kwanza hadi cha tatu.
Rumi8:4-7 nia ya mwili ni mauti hata vile tulivyoingia zaidi ya viungo kwa kuwa tulikuwa na nia ya mwili ilikuwa ni lazima mauti ingetupata, lakini MUNGU anataka tuwe na Roho ya Uzima kwa kuwa nia zetu ni za Roho ambayo ni uzima.
Kuongea na kuhoji hoji sio tabia ya MUNGU. MUNGU atanionyesha mambo mengi iwapo nitakuwa na tabia ya kunyamaza kimya na kusubiri majira hivyo niache tabia ya kuona jambo na kuongea nilichoona.
Kila mwenye tabia ya kushindana na mwingine ni kwakuwa anatabia ya au kile kilichompata Hawa.
Mambo ya kufuta yanayofatana na mwenye umbo la mwili:-
Mwa 3:1-6 hiki ndicho kilichompata Hawa kutaka kukalia kiti cha MUNGU.
Mwa 5:3 tabia ya mtu ya kupanda na kushuka.
Tabia ya kujitetea ni tabia ya Adamu na ni tabia isiyofaa mbele za MUNGU kwani imesababisha wengi kujitetea na kuwa sukumia makosa wenegine.
Kujitetea ni tabia ya mwili au umbo la mwili na viungo hivyo nilazima nitoke kwenye viungo na umbo la mwili.
Tunaweza kuishi kama Wakili wa MUNGU kuto kuwa na principle za maisha ya mwili na viungo na umbo lake. Sitakiwi kuadilika badilika tabia.
Habari ya Musa Kut 32:1-6 na Hesabu 2:9-10 Musa alikuwa mwepesi wa kutubu kwaajili ya wengine lakini kwaajili yake alikuwa hawezi.
Hiki ndicho kinachompata Yule anae tubu kwaajili ya wengine lakini yeye mwenyewe hatubu inasababisha kuchoka kutenda mema.
Tubu kwa kile ulichofanya na usichofanya huo ndio utakatifu MUNGU anaoutaka. Tuwe na tabia ya toba binafsi.
Tabia ya kusanyiko la MUNGU la kizazi cha kwanza lilikuwa na manung'uniko.
"MUNGU tusamehe kwa ajili ya Kanisa la jangwani kwa kuwavusha lakini kwa muda mfupi walinung'unika.
Sisi leo kukatae tabia ya tumbo ya kutokusema asante Mt17:1-8.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni