Ijumaa, 27 Januari 2017

AKIBA NJEMA NI IPI NA AKIBA MBAYA NI IPI?? MITHALI 4:23

Kusimamisha akiba njema ya moyo inayofuta akiba mbaya zote ndani yaa moyo. Moyo una pande mbili.
Kuna chumba kinachohifadhi akiba njema na kingine kinahifadhi akiba mbaya. Tumepewa Moyo halisi ingawa haya yako kwenye Moyo mmoja.
Chemichemi ya uzima inatoka  kwenye moyo wenye akiba njema. Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo.
Moyo ni store na ni hifadhi ya wanyama wadudu na ndege, majoka pundamilia.
Huu moyo unahifadhi mabaya na mazuri kwa wakati mmoja na ninao moyo mmoja.
LUKA2:18-19  wote waliyasikia maneno hayo lkn mariamu aliyahifadhi moyoni mwake maneno yale.
LUKA 6:45 Mtu mwema katika hazina ya moyo wake hutoa yalio mema ktk moyo wake.
Kadhalika mtu mwenye hazina mbaya katika  moyo wake hutoa mabaya katika moyo wake.
Yote haya yanatokana na kiwango chako cha yale uliyo yasikia na kuyaona.
Maana kila uliyoyasikia yanakaa katika moyo.
Kuna mambo ambayo uliyakokota tangu ukiwa tumboni mwa mama yako tokea siku uliyotungwa mimba kuna uliyoyakuta na yakaendelea kuwepo hapo yakiongezeka kila siku mpaka siku unazaliwa.
Ukiwa tumboni mwa mama yako  kuna ambayo ulikuwa unayasikia yalemama yako anatendewa hata ukayaweka ndani ya moyo wako kwa kuwa moyo ndio hifadhi ya kila ulichosikia na kukiona.
Hii ndio sababu ukizaliwa tu lazima ulie kutokana na yale unayoyajua kuwa yapo ndani ya mji unaouendea.
Kila anachopatwa mama na wewe unapatwa hukohuko tumboni ; mfano, mama akiumwa na wewe unaumwa, akiongea mabaya, akitukana akisengenya, akipigwa, malalamiko, manung’uniko.
Kuna mwingine tokea mimba alichukiwa akakataliwa na baba ukiuliza kwa nini anakuambia ilikuwa si majira niliyokuwa nimepanga kupata mtoto, amenivurugia mipango yangu.
Hivyo mpaka siku akizaliwa mtoto anajua kuwa baba hanipendi  wala hawezi kupatana au mama hanipendi, mama hata kunyonyesha ananyonyesha tu huku akisema sina jinsi ndio hivyo kashazaliwa.
Kuna mjomba, shangazi, babu, bibi walimchukia mama akiwa amebeba mimba au ujawepesi angu hivyo hata nikizaliwa siwezi kupatana nao automatically pasipo hata kuambiwa yaliyowahi tokea nyuma,
Hata wakijifanya kukupenda taa nyekundu inawaka ikisema hawakupendi hawa tokea ukiwa tumboni mwa mama yako.
Pia kuna wanaozaliwa na uchungu na kukataliwa huu ni msingi uliokutana nao ukiwa tumboni uliotangulia.
ZABURI 11:3  Kama msingi ukiharibika mwenye haki atafanya nini? Kwa kuwa tangu zamani ukiwa tumboni mwa mama yako ndiko msingi wako ulianzia halafu ukaharibika, Je ukikua utafanya nini?
Je chumba cha moyo wako kinahifadhi gani? Kuna wenye chumba cha mataarifa ya kusikia, mataarifa ya namfahamu huyu vizuri hadi kwao na tabia zao.
Wengine wengi nafsi zao zimekuwa kama gari la taka, mavi linavuta mitaro.
Kiwango unacholinda moyo wako usiingiwe na mambo mabaya ndicho kiwango cha akiba njema kilichoko ndani yako.
Nafsi ya mtu haili itakula jeuri yake. MITHALI 13:2- Kila mtu atakula matunda ya kinywa chake, kwa kuwa kinywa hunena yaujazayo moyo wake.
MARKO 7:20-23 Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi, maana midomo ya mtu hutoa unajisi matusi ujinga na upumbavu lugha mbaya tu!
EZEKIEL 28:17-18 Nimetokeza moto ndani yako nao umekuteketeza umekuwa majivu najisi kitu kisichofaa.
Moto uliokula biashara yako, kazi, agano lako, nk ni moto ulioko ndani yako wewe wenyewe.
Moto ulioko ndani yako ulioutengeneza kwa chuki  jeuri nk ndio unaosababisha ukwazike, unaovuruga agano lako, unakufarakanisha na kichwa wako, ndio uliokufikisha hapo ulipo wewe katika kila eneo.
Moto uliotokeza ni ile akiba ya ndani ya moyo wako, kile ulichokijaza kwenye moyo  kama kinatokana na maneno au NENO.
Kama una akiba njema  basi utakuwa na mema tu!! Kama ilikuwa akiba mbaya ndani ya moyo basi utakuwa na mabaya tu.
Store ya mambo mabaya akiba mbaya ni moyo wako wewe mwenyewe hiyo ndio imekuteketeza hata huwezi kuwaachilia wengine huwezi kuwatoa ndani ya moyo wako huwezi kuwasamehe na kusahau;
Ndio imekufanya kuwa majivu najisi na kitu kisichofaa, kitu kibaya, ukifanya kazi unajiona house girl, maswali maswali ya kwa nini mimi tu?
Akiba mbaya ndio inakufanya uone unanyanyaswa na kichwa wako, hata kama unaambiwa kweli unaona unadharauliwa, huheshimiwi, kumbe limoyo lako wewe mwenyewe, unasema kila siku unanikwaza kitu kidogo tu hasira umefurai yanakutoka kama umemeza betri leo hama kituo hicho.
Kazi ya akiba mbaya ni kutoboa madirisha kwenye moyo wako ili aje akuibie:-  
+nguvu,
+Uweza,
+Baraka,
+hekima,
+heshima,
+utukufu na                                                               +utajiri.
Akiba mbaya analeta ukimwi kisukari ili ujue kama ni akiba mbaya utasikia doctor anasema usiwaze sana, usipaniki, usikasirike kasirike, usikwazike, manung’iniko yote haya husababishwa na akiba myaya ndani ya moyo.
Kwa hiyo ujue akiba ya MOYO wako ndio inayokupa maisha ya kuishi. Akiba mbaya hufungua milango ya mabaya na kukuletea mauti.
Huleta magonjwa, ukiwa na vidonda vya tumbo ujue una akiba mbaya ya moyo wako. *DALILI ZA AKIBA MBAYA;*
#Magoti kulegea,
#mabega kuchoka,
#mgongo kuuma, 
#kiuno kuuma,
#miguu kuwaka,
#kujisikia kununa saa zote,
#vidonda vya tumbo,
#kukosa hamu ya kula kitu chochote,
#kutokuwa na amani wakati wote,
#macho kupungua nguvu ya kuona,
#kukosa usingizi au kusinzia sana,
#kutembea huku unaongea peke yako mwenyewe mpaka unaamua mwenyewe,
#kupenda kujieleza sana .
#Kutojiamini ,
#hisia mbaya kila anayeongea anakusema wewe,
#kukosa furaha saa zote,
#hata ukivaa hupendezi, #hakuna hata siku moja ambayo unambiwa umependeza, #unafilisika tu huongezeki, #unaharibu mahusiano yako na MUNGU na unakufarakanisha na kuoa kuolewa fedha, kazi,
Inakula mifupa ,
#ndio unaokuchafua, unaokutaabisha, unamuangamiza, unakushusha chini, unakufedhehesha, unakukosesha na kazi nzuri,
#kila unachoongea ni kibaya.
Je hujawahi kuona mwenye diploma anapata kazi nzuri lakini mwenye digrii mfagiaji tena anapewa kufagia nje? Sababu ni moyo.
Badala yakuwa na moyo wenye kutoa chemichemi ya mambo mazuri unakuwa ya kutoa mabaya.
Dalili hizo ni pamoja na; uso wake hukunjamana ,kuwa na hasira saa zote, ana maswali yasiyo na majibu, kuwa na hofo, woga hata kupanda pikipiki tu utakikia anaogopa kufa, kuota ndoto za kufukuzwa na wanyama, kutomwamini mwingine.
Kutokuwa na moyo wa shukrani, kutokuwa na furaha hata ufanyiwe nini,huoni mema kwa wenzako yote ni mabaya tu, hata uimbe vipi naona mema aa naona mazuri tu ….. akiba mbaya anakuzomea maana anajua unadanganya kupritent!
Hupati tenda kwa sababu ya moyo wako… unapoandika application sio yale maandishi yanayokua kazi tenda tena bosi anaposoma hasomi lile karatasi bali anasoma moyo wako ndio sababu hupati unachotaka.
Unapaka cream ili uonekane mzuri, kuwa na machunusi usoni, ngozi inakubabuka, umeoauka  midomo inakauka na kupasuka.
Ni mkali cku zote kitu kidogo tu anashikilia bango, akitembea utasema ni mnyenyekevu kumbe amejaa akiba mbaya tu!
Kila unachofanya ili kipate kibali au kikose kibali ni kutokana na akiba uliyonayo.
Kuna moto unaotoka ndani  ya kila mmoja unasababisha uwe kitu kisichofaa mbele za MUNGU na mbele za wengine.
Leo kila tabia uliokuwa nayo au moyo uliokuwa nao wenye akiba mbaya unatolewa.
MAMBO YANAYOSABABISHA AKIBA MBAYA;
*Kufukuzwa kazi kwa kuonewa kwa ghafla,
*kuna jambo ulilolitarajia likachelewa kutokea,
*kuna majibu mazuri uliyoyategemea yakajibiwa vibaya,
*kuna matokeo mazuri uliyategemea yakaja kinyume visivyo,
*kuna uliyemtegemea akakuacha kwa ghafla,
*uliyemuamini sana akakuasi,
*akakugeuka, akakusaliti,
*akakutenda ubaya,
*ulitenda mema ukalipwa mabaya,
*kufiwa ghafla na uliyempenda,
*aliyekupenda,
*uliyemwamini,
*ukamwamini,
*Tendo au matendo uliyowahi kufanyiwa ukatili,
*kubakwa kulazimishwa kufanya mabaya,
*kuugua kwa muda mrefu,
*kuuguza kwa muda mrefu na kwa gharama kubwa halafu asipone akafa,
*kupita mahali pagumu kukosa fedha,
*kusalitiwa na uliowaamini,
*waliokuwa karibu na wewe.
*na mambo mengine hayo yote yanayoleta kuwa na akiba mbaya ndani ya moyo  wako.
*Aidha kuna madeni yasiyolipika ,
*kudaiwa kwa vurugu mfululizo.
*Kesi za kusingiziwa,
*kusingiziwa umezini,
*unaiba na uchawi hizi ndizo kesi ambazo huleta shida mara nyingi pia huleta akiba mbaya.
*Na wengine huchukua uamuzi mbaya mno, hatua mbaya.
Tunatakiwa tuwe na moyo wenye akiba njema pekee.
Homework ; kila mmoja kuanzia leo akutane na mwenzake au kuhani ili ufunguliwe ili kuondoa akiba mbaya zote ndani ya moyo kwa siku saba. Pia katika wiki hii hutakiwi kukosa ibada za majibu.
CHUNGAJI MMOJA LEO AMETUKUTA NA AKIBA MBAYA KILA MMOJA AONDOE ILI APATE  PA KUKAA.
POINT: EZEKIEL 28:18{b}

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni