Jumatatu, 23 Januari 2017


KWELI MOJA TU IMESIMAMA NDANI YA KANISA NA UUMBAJI WOTE.


Wakili wa MUNGU leo amesimaisha Kweli moja tu ndani ya kanisa na uumbaji wote na kusema “Maisha yangu yote kuanzia sasa hivi yatakuwa na Moyo mmoja, hivyo Moyo mmoja umekuwa ni sehemu ya maisha yangu yote milele.”
Sasa baada ya Moyo mmoja tunasimamisha kweli moja halisi. LEO KWELI INASIMAMA NA UKWELI NA UONGO UNAFUTWA.
Kulikuwa hakuna namna ya kuwa na kweli kutokana na mioyo mingi iliyokuwepo tukajikuta hata ukiambiwa uongo unaona ni kweli lakini leo ndio mwisho kweli itajulikana kuwa kweli na uongo utajulikana kuwa ni uongo.
Kwa sababu kweli imesimama sasa hatutasingiziwa tena, hatutazushiwa tena. Mashitaka ya uongo kwa wenye haki leo yameungua.
Maisha ya mateso kwa wenye haki, masingizio kwenye familia, kuchukiwa kwenye familia yako kutengwa kwenye familia yako, kuonekana hufai kumefutwa hutaona tena maana kweli imesimama.
Sasa utaonekana ni mwenye haki kwenye familia nk.
ZEKARIA8:1 na YOHANA8:31-. Kweli pekee ndio inayokuweka huru kila mahali. Tangu zamani kweli haikuwahi kusimama.
Hata wakati wa YESU kila aliposema kweli waliokota mawe wakitaka kumpiga nayo na wakati huo hata wao wanajiita ni wa MUNGU.
Leo tambua hata wale wote WANAOMKATAA wanaomtukana WAKILI WA MUNGU hao sio wa MUNGU japo wanajiita ni wa MUNGU.
*Kweli ilikuwa haikuwahi kukubaliwa popote.*
Kuanzia leo TUMEAGIZWA kusema kweli tu! Kwa kuwa hakuna wa kuokota mawe hakuna wa kukupiga jiwe milele.
KUANZIA LEO TAMBUA KWAMBA MUNGU AMEKUBALIWA NDANI YA UUMBAJI WOTE KWA SABABU KWELI IMESIMAMA.

ZEKARIA8:1- Sasa kanisa ni mji wa kweli ya MUNGU  na MLIMA MTAKATIFU .
Sasa MUNGU atakuwa ni MUNGU wetu katika Kweli na katika Haki.
Adui alikuwa ni moyo wa pili kwa sababu hiyo  MUNGU aliacha tupigane power chafu lakini leo MUNGU hataacha wakusumbue wakupige power chafu kwa sababu tayari Kweli imesimama.
Mwanzoni tulionekana ni laana lakini sasa hatutaonekana laana tena. Wakati wa natuwasha tulionekana kama vile hatuna MUNGU lakini  sasa MUNGU amesimsmisha kweli yake hakuna wa KUNIGUSA.
Kila mmoja na aseme kweli  na jirani yake. Kila mmoja asimame kwa haki asiape kwa uongo.
Huu ndio mwisho wa kerubi , ibilisi, shetani, nyoka mwamamke, mwanaume, kahaba mkuu, mnyama asiyejulikana sasa KANISA LA MUNGU litajulikana.
Kila mmoja na aseme kweli na ndugu yake . mashtaka yaliyokuwa yamepelekwa popote ya uongo yamefutwa.
Aidha wakili ameongoza wenye haki kutoa Sadaka Maalumu ya Kusimamisha kweli. Kufuta  uongo ukweli. Kufuta mashitaka ya uongo juu ya wenye haki.
Sasa kweli imesimama wengi waliofungwa gerezani wataachiliwa huru kwa sababu wengi walihukumiwa mpaka kufungwa kwa sababu ya mashitaka ya uongo leo mwisho. Mataifa yaliyokuwa yanatumia nguvu ya taifa hili sasa utaona wengi wakiishiwa  wataanguka kwa kuwa kila kitu kinarejea mahali pake.
Sasa hivi ni majira halisi ya KUJULIKANA NA KUTAMBUA kwamba nani alikuwa anamsaidia mwingine /mwenzake. Hii majira ilikuwa inasubiri leo.
Ibada ya jana ilikuwa si ya kawaida ndio iliyotuletea ibada ya leo.  Sasa wewe ambae umeoa  umeolewa badala ya mwingine hapo ndio sijui tumuachie MUNGU mwenyewe.
Wengine tunawaona wamepararaizi lakini kumbe ni mzima ila kuna mmoja anayetumia  upande huo mmoja leo mwisho.
Kuna tuliowaona ni zezeta kumbe ndio wana akili nzuri. Kila aliyekuwa anasoma kwa ajili ya wengine wakaenda juu leo wanafukuzwa vyuoni.
Kila aliyeshitakiwa kwa uongo leo anaachiwa huru. Kweli imesimama kila mmoja atasimama kwa NAFSI yake.

Wengine hapa hawana afya zao sura zao leo zinarejea. 
Haya yote yanatokea kwa kuwa kweli imesimama.
Na ijulikane wale akina mama wenye macho mekundu kule SHINYANGA  kama ni wachawi au laa.
Dini na dhehebu wanasema kuwa SILOAMU ni freemason leo kweli imesimama na ijulikane kama SILOAMU au ni wao dini na dhehebu ndio freemason.
Baada ya kweli kusimama sasa mchawi na asimchawi atajulikana.
Kila mmoja anapokea shea yake kwa MUNGU iliyokusudiwa tangu mwanzo.
Sasa anayesema kweli atajulikana na anayesema uongo atajulikana. Ambae ni mwizi atajulikana na asiye mwizi atajulikana.
SHUKRANI: Kuna kiapo kimesimama *NI MWISHO WA MUNGU, KRISTO WAKO, WAKILI WAKO, KANISA LAKO, TAIFA LAKO NA KIZAZI CHAKO KUSHITAKIWA.*
Tumeinua mnara wa kweli  ambao unasababisha kila mmoja  kuona kuwa SILOAMU ndio wanaosema kweli pekee. Mnara wa uongo uzushi  adui umefutwa.
Hakuna atakae gombana na jirani ndugu yake milele. Mafaili ya kila aina ya uongo yamefutwa.
Leo ni cku ya kukumbukwa mno kwetu. Maana kila nafsi inarudi mahali pake. Kila shilingi dola rasilimali heshima vyote vilivyokuwa vimeibiwa vimerejea mahali pake.
Kila ulichowahi kuibiwa jua leo kimerejea. Mambo ni matamu. MUNGU awabariki awape kila mnachohitaji. 
KWELI NDIO INAYOKUPA KUCHUNGWA NA MUNGU AMBAYE  NDIYE  MCHUNGAJI MMOJA HALISI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni