KUSIMAMISHA SIKU 7 ZA ADENI NA EDENI ISIYO NA UMBO LA NYOKA
Wakili wa MUNGU amesema kila siku ina msingi wake na jengo lake ambapo kazi ya msingi ni kuchora ramani.
Aidha alizungumzia Eb1:14 na Eb 1:5 kuhusu utendaji wa ibadi kubwa ya malaika ambao MUNGU amewaachilia malaika wengi wasio na idadi kwaajili kumuhudumia kila mmoja.
Yaani kwajili ya somo, kukuongoza, uponyaji, kuelewa, fedha, Baraka na kila kitu kulingana na mahitaji yako 1 Petro2:9-10 sisi tuna ukuhani wa kifalme ambao tunahudumiwa kwa kila kitu.
Kuna malaika wanaonihudumia na kuhakikisha ninapata kila ninachokihitaji isaya 44:26 kwamba MUNGU anathibitisha NENO litokalo madhabahuni Isaya 45:7-8 MUNGU anathibitisha NENO ninalotamka hivyo nitamke ili kuumba siku yangu kwani nina nguvu hiyo.
1yoh4:17 kama MUNGU alivyo ndinyo tulivyo hivyo tamka vitu vizuri na halkikisha unaweka ulinzi kwa kila unachotamka kwa akukiumba kila siku.
Hatahivyo Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya kusimamisha siku 7 za kufuta umbo la nyoka ndani yetu.
Uumbaji wote tunaouona upo katika Adeni na Edeni. Mlima wa BWANA inamaanisha BABA, NENO na Roho.
Adeni ina maana ya mkusanyiko wa NENO la MUNGU na Edeni ni Bustani ya BWANA.
Adeni ni marejesho ya vituo vyote vya Rohoni (mkusanyiko wa Ufahamu wa NENO ambao haujaibiwa.)
Edeni ni Bustani ya Kanisa. Edeni ni nafsi inayomjua MUNGU. Maisha yote yanapatikana ktk Adeni na Edeni.
Kanisa lilitakiwa kukaa katka Adeni na Edeni lakini walitolewa zikaa dini na madhehebu na dunia.
Biashara yako na kazi yako ikiwa ni pamoja na kila kinachotajwa kwa majina yako kinatakiwa kukaa Adeni na Edeni.
Kukaa Adeni ni kukaa na BABA na NENO na mimi nikiwa ni Roho. Kukaa Edeni ni mimi au nafsi yangu kumjua MUNGU.
MTIRIRIKO WA UUMBAJI WA MUNGU
Ufu 12:1 mwanamke
Ufu 12:3 nyoka
Ezekel 28:15 Adeni.
Mwa 1:1 mbingu na nchi
Mwa 1:3-31
Mwa 2:1-4
Mwa 2:15 Edeni
Mwa 3:1 nyoka
Kutoka MUNGU kilichofuata ni nyoka. Kabla hujakutana na MUNGU nyoka na kabla ya kumjua MUNGu ulimjua kerubi na nyoka kwanza.
Kaba ya kukutana na Wakili wa MUNGU anaezuia ni nyoka. Nyoka anakusababisha nafsi yako isimjue MUNGU kwa maana ya kukaa Edeni.
"kabla sijaja mimi hapa mnatakiwa mpige kwanza nyoka anayevuruga ufahamu usielewe wala kukumbuka na MUNGU hawezi kukupa kile usichokifahamu wala kukikumbuka" alisema Wakili wa MUNGU.
"MUNGU amekuja kuishi na sisi akiwa ni BABA hivyo usikubali shida yoyote ikufanye usiwe na furaha wala kukosa amani maana MUNGU anasovu yote hayo" amesema Wakili wa MUNGU.
"Jambo lolote usipolipiga halitoki na ulipige katika majira yake, sasa majira ya kupiga umbo la nyoka imefika piga umbo hilo ili MUNGU atamalaki katika maisha yako" aliongeza Wakili wa MUNGU.
Kulikuwa taasisi Fulani zimeweka nembo ya nyoka kwa kuwa wajua ya kuwa nyoka ni mwelevu. Ndio umbo la nyoka lilikuwa linaendelea kufanya kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni