Jumatatu, 9 Januari 2017

12 Siwani, 6
*MAWASILIANO KATI YA KANISA NA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE KTK MAJIRA NA SAUTI YA SABA*
Wakili wa MUNGU alianza ibada kwa kuuliza swali na kulijibu; swali hilo ni "tutawasiliana na huyu MUNGU?"
Yaani MUNGU ambaye tayali tumekuwa na umoja nae ambapo kila ninapokuwepo nae yupo.
Alisema ktk *Majira ya kwanza:-* "Ufu12:1, Ezekiel 28:15 hadi Mwa1:1.
Katka Majira hii kerub alikuwa akiongea na MUNGU uso kwa USO. Hapakuwepo na maombi, kulikuwepo na mawasliano ya moja kwa moja.
Kila alichowaza au kutamka MUNGU kilikuwa Roho. Wote walikuwa wakimwona MUNGU ni mpole, mnyenyekevu, mpaji mweza yote n.k".
*Majira ya pili:-*Mwa1:3 hadi kutoka 12:2 mawasiliano yalikuwa ya aina mbili; =>mawasiliano ya moja kwa moja kabla ya anguko.
=>Hapa baada ya anguko ndipo maombi yalianza. Maombi yalitokana na kuwepo kwa dhambi.
*Majira ya tatu:-* kut 3:10 hadi 1 falme18:30 "mawasiliano yalikuwa kupitia Musa (kut 20:19 wana wa Israel walimkataa Mungu na walitaka miujiza.
Zab 103:7 Musa alitaka kumfaham MUNGU. Je wewe unampenda ufaham".
*Majira ya 4:-* 1falme17:1, Luka2:21 kile kizazi cha pili. "Hapo dhambi zilikuwa zikinuka. Zilisababsha umwite MUNGU na haitiki. Hapa madhabahuni ukija kuchafua Neno ua kutofanya ulichoambiwa unabomoa madhabahuni.
Mawasiliano yalikuwa kupitia kwa Eliya mtishibi.
*Majira 5:-*"ilianza Mdo10:38 hadi 28 Adari, 2011. mawasiliano yalikuwa kupitia kwa Yesu. Hata sisi tulipoanza mawasiliano yetu yalikuwa kupitia kwa Yesu.
*Majra ya 6:-* imeanza ktk yoh 9:7- Mt 21:41 hadi 8 siwani, 6.
Mawasiliano yalikuwa kupitia Damu ya Haki kweli na Hukumu zab84:14- Kugeuza maji.
=>Damu, kitabu
=>Haki Kweli Hukumu.
 Kwa sababu Nabii wa mwisho aliyoyafundisha yalikuwa ufunguo".
*Majra ya 7:-* imeanza 8 siwani, 6 hadi sasa. "mambo yaliyokuwa yakizuia mawasiliano:-
=>kulikuwepo na umbo la nyoka ndani ya kanisa. Kabla ya mlima wa BWANA yaani ufahamu alionekana kwanza nyoka.
Nyoka alikuwa akichafua usipate ufahamu kwa kuamini alikuwepo kabla ya ufahamu.
(Kinacho-sababisha kutoka ni kwa kupata ufahamu). Akavaa umbo la nyoka pale eden na kudanganya kanisa na likadanganyika, umbo la nyoka lilichafua Aden na Eden.
=>Kabla ya anguko jina la Hawa halikuwepo lilitokea baada ya anguko.
Pale alipoongea na nyoka Nafsi yake ilienda kwa nyoka na ya nyoka ikaja kwake, aliyechuma tunda ni nyoka na Adamu alipokula akawa nyoka.
Aliyesema wewe utaitwa Hawa ni nyoka akmwambia nyoka. Aliyesema utakuwa mama wa wote kwenye mwili ni nyoka akimwambia nyoka.
Kilichosumbua vizazi vyote ni nyoka na kusababisha anguko.
MUNGU kizazi hiki ametutenga kabisa na nyoka na milele na milele umbo la nyoka kwani nyoka ana ndimi mbili ya mema na mabaya.
MUNGU amekuja kuishi na sisi, je tutawasiliana nae vipi?
MUNGU NA KRISTO tuko nao Wakili wa Mungu ni wa nini? Swali lilojibiwa na Kuhani wa Njia ya Mataifa Fahari ya Bwana akasema MUNGU na Kristo hawaji kwako bila Wakili wa MUNGU.
Maana Wakili wa MUNGU ni kao la MUNGU na KRISTO hivyo ni lazima awepo ili MUNGU apate kao lake kwakuwa MUNGU ni Roho na Kristo nae ni Roho.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo WAKILI wa MUNGU aliongiza wenye haki kutoa Sadaka Maalumu ya Hesabu 16:15-30 nyoka kutengwa, kufutwa kabisa kwa wenye haki.
Ambayo pia sadaka hiyo maalumu ina hukumu mashtaka yote kwa wenye haki.
Yaani nchi kufunua kinywa na kuwameza waovu wote kwa sadaka hii wote wamemezwa.
HUKUMU YA MILELE IMESIMAMISHWA kwa wale waliokuwa wanamshitaki Wakili.
Ukumbusho wao umefutwa wala MUNGU kumbukumbu zao milele.
Aidha pia alionesha wenye haki ktk ibada hiyo ramani ya uumbaji wote ktk wilaya ya kinondoni iliyoonyesha mahali Kanisa
la *The pool of Siloamu church* lilipo kupitia "google map"
MASAHIHISHO.
1.Mwa3:20 Adamu(nyoka)alimwambia wewe utakuwa mama wa wote wenye UHAI siyo mwili.
2.HUkumu ya milele imesimamishwa Kwa waliokuwa wanawashitaki wenye Haki wote (siyo Wakili peke yake)
MUNGU AKUBARIKI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni