Jumatatu, 9 Januari 2017


*MAREJESHO YA UTAJIRI WA MADINI NDANI KANISA*
Wakili wa MUNGU alianza ibada kwa kusema tukae kama familia moja tukiwa na Baba, akaagiza wenye haki kupanga viti katika mduara na kiti chake, mama wakili, Mtendaji wa Wakili vikiwa vinaangaliana na viti vya wenye haki.
Nandipo mazungumzo ya kama BABA wa familia na familia yake yakaanza maana tayali kuna Agano la umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa akauliza swali kuwa ni kwa nini mvua haikunyesha jana hapa wakati baadhi ya mikoa ilinyesha?
Ni swali alilouliza kutokana na shukrani na toba iliyofanywa katika ibada ya jana kwaajili ya ukame wa kutonyesha mvua nchini.
Baadhi ya wenye haki waliopata taarifa za kunyesha kwa mvua katika mikoa mbalimbali nchini walitaja mikoa ambao mvua ilinyesha ambayo ni pamoja na mikoa ya jiji Mwanzo Malidadi (mbeya), Ufunuo wa Kristo( Iringa), Mlima wa Neema kubwa (morogoro), Hati miliki(mtwara).
Lakini swali hilo lilihitimishwa kujibiwa na Mtendaji wa Wakili wa Wakili wa MUNGU ambaye pia ni Kiongozi wa Makuhani Njia za Bwana akisema ni kwa sababu mkoa huu haukutubu walipopata barua za kumchafua MUNGU walikaa nazo tu lakini kuna mkoa ambao Mkurugenzi wake alipopokea barua ya kuchafua aliichukuwa mwenyewe na kuipeleka kwa kuhani wa pale na kusema wafanye Toba kwa ajili ya hilo.
Kisha Wakili Wa MUNGU akaruhusu kama kuna yoyote mwenye kitu cha kusema kwake; “hapa tumekaa Baba na watoto wake”.
Wakili wa MUNGU aliahirisha mkao huo wa mkutano akasimama na kurudi madhabahuni na kuanza kwa kuonyesha madini yaliyotoka kwenye migodi ya wakamilifu ambapo tangu walipopata wamepata sana madini ingawa wamefikia kuanza kuvuna madini.
“leo tunasimama tukiwa familia moja ya MUNGU wenye migodi ni lazima wapate madini na wenye biashara, viwanda ni lazima upate faida”
Awali kabla ya kusimamisha toba ya kufuta damu zisizona hatia za waliokufa wakiwa ni makafala ya uchimbaji wa madini kuanzia kipindi cha uchimbaji cha wajerumani hata leo huku wenye haki wakiwa wameizunguka madhabahu aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu.
Ambapo sadaka hiyo maalumu akaita ni sadaka ya Zab 23:1-6 kumsimamisha Mchungaji Mmoja Halisi ambae ni MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi Vyote.
Kwa sadaka hiyo Wakili wa MUNGU alisema “kwenye bonde la uvuli wa mauti sitapita tena”
“Hakika wema na fadhiri zitanifuata mimi milele, ninakaa nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu” alifafanua kuhusu sadaka hiyo maalumu.
Alianza shukrani na toba hiyo kwa kumshukuru MUNGU kwa ajili ya kutoka kwenye kituo cha umbo na kuagiza “tubu kwaajili ya damu zilizokuwa zinalia zinadai haki ya wenye haki wasipate madini leo tunazitubia hizo yaani damu za waliowahi kuzikwa wakiwa hai”
“Madini sasa yamerejea Madhabahuni hayataonekana kwa wachawi milele” lisisitiza
“Toba kwa damu zinazolia katika migodi ya madini zinazosababisha wachimba madini wasipate.
Hatahivyo wakati wa kusimamisha sadaka hiyo maalumu mbele za MUNGU alichagua baadhi ya wakamilifu na makuhani wenye migodi ya kuchimba madini saba wakiwemo kati yao kiongozi wa Makuhani Njia za Bwana na kuhani Njia za MUNGU kushiriki kuinua kapu la sadaka hiyo maalumu mbele za MUNGU Aliyetuma wote.
Baada ya kumaliza toba na shukrani hizo alihitimisha kwakuwatakia kila wenye haki kupokea kila anachota kwa MUNGU mwenyewe biashara yake, shamba lake, duka lake na kila chanzo cha mapato Baraka za viwango vya mgodi kutema vya thamani kama madini .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni