Jumatano, 25 Januari 2017


SIKU 7 ZA KUKABIDHI MOYO MMOJA HALISI KWA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE

Kushukuru MUNGU kwa ajili ya mwezi tammuzi uliotupa moyo mmoja halisi. 
Moyo  ambao umetupa Kweli Halisi inayotupa kuishi na MUNGU na inatupa kuchungwa na Mchungaji mmoja Halisi.
SADAKA; Kufuta chochote chochote kilichokuwa kimekaa  kwenye moyo wangu na kuondolewa ngani yangu, Kanisa kwa wenye haki na kila kinachoitwa kwa jina langu.
ZABURI27:4 Sadaka hii inanipa mimi kukaa kwenye Neno sawa na ninavyofundishwa kwa uzuri wa MUNGU, Nifurahie na kutafakari  ambayo MUNGU ametenda kwetu Kanisa.
Mwezi wa tammuzi tumepewa Moyo mmoja Halisi, MUNGU anachoangalia ni Moyo wake ndani yangu, Moyo ambao ndani yake hakikai wala hakai yeyote zaidi ya MUNGU peke yake.
Ukiweka kilimo ndani ya Moyo, siku ya kupanda  unasema napanda kwangu kwanza kwa MUNGU baadae.
Huu sio moyo mmoja unatakiwa kumuweka MUNGU kuwa namba moja   kwako.
Hakikisha hufanyi chochote kilicho chako kabla kufanya kwa MUNGU.
Na sasa unatakiwa ujenge tabia ya kujenga au kupanda kwanza kwa MUNGU kabla yako.
Ifike mahali  pa kusema MUNGU kwanza vitu vingine baadae.
Unatakiwa uwe na Moyo mmoja Halisi sio mioyo mingi, mioyo ya vitu vingine ndani yako.
Matendo13:22 WAKILI WA MUNGU siku zote anatenda anafanya yaliyo mapenzi ya MUNGU peke yake.
Tunaona hata kizazi cha pili Daudi aliyatenda mapenzi ya MUNGU.
Leo mimi mwenye haki ndiye ninayetakiwa kuyatenda mapenzi ya MUNGU ndani ya kizazi chake.
ZABURI 89:1- Ni Daudi peke yake ambaye MUNGU amesema kuwa kiti chake kitakuwa cha MUNGU kwa kuwa aliyatenda mapenzi ya MUNGU kwa sababu ya Moyo mmoja ndani yake.
Kiti kuthibitika, Moyo wa MUNGU unakupa kushinda  kama WAKILI wa MUNGU alivyoshinda na zaidi ya kushinda.
KUMB5:29 Laiti wangekuwa na Moyo kama huu siku zote wa kunicha wangefanikiwa wao na watoto wao yaani [uzao] MUNGU anasema ukiwa na Moyo wake ndani yako utafanikiwa.
Kinachozaa ni Moyo kwa hiyo usipokuwa na Moyo wa MUNGU unazaa mambo ya Moyo ulionao sawa na ulivyopanda  utavuna hivyo hivyo.
Math12:33-35 ili uzae lazima uwe na Moyo wa MUNGU unaozaa vitu vizuri.
Hata ukisema tasa ni Moyo wako ndio tasa lakini kizazi chako ni kizuri ila kwa sababu Moyo ni chanzo cha vitu vizuri kama haupo vizuri huwezi kupata mtoto.
Madoctor utakuta wanahangaika na pracenter akijua ndio tatizo lilipo kumbe tatizo lipo kwenye moyo wake mwenyewe maana kinachozaa ni moyo sio pracenter.
VITU VINAVYOKAA KWENYE MOYO:- Moyo umebeba yafuatayo;-
#Nguvu ya udhihirisho,
#Nyota ya mambo mazuri [MAFANIKIO].
#Moyo ni mtawala wa vitu vyote.
#Ndani ya huu moyo wenye vitu vizuri anahitajika akae  MUNGU peke  yake.
Katika NYOTA KUNA;-
*nguvu,
*hekima,
*Baraka,
*utukufu,
*heshima,
*uweza,
*utajiri.
Moyo ukiibiwa ujue vitu vyote hivyo utavipoteza.
Pia jua kwamba akija mwingine kukaa ndani ya moyo vitu vyote vinakimbia hata ulivyokuwa umeahidiwa hupewi tena.
Ndio sababu MUNGU anasema linda sana moyo wako kuliko vitu vyote uvilindavyo Mith 4:23.
ZABURI32:1- Neno linasema heri aliyesitiriwa dhambi zake yaani heri anayesamehewa dhambi, Daudi alieleza moyo wake jinsi usivyomficha MUNGU. 
Wenye haki hatutakiwi kuruhusu moyo kubeba uchafu ndani yetu, siku zote tutafakari ukuu wa MUNGU.
1nyakat29: Daudi alikuwa ni mtoaji kwa viwango visivyo vya kawaida, sadaka alizokuwa anatoa zilikuwa zinaonyesha moyo wa MUNGU ndani  yake.

MUNGU anataka kila mmoja awe na huo moyo wa MUNGU ndani yake.
Kila kitu unachofanya ufanye kwa ajili ya MUNGU kama WAKILI WA MUNGU anavyofanya. Tujifunze kwa mtini .
WAKILI wa MUNGU hakuwahi kumtolea MUNGU kitu kinyonge, je sisi tunatoa wapi?
Tunatoa vitu vingine hata sisi wenyewe tukipewa haturidhiki na hata tukipata wengine tunavitupa au kugawa kwa wengine, leo tubadilike.
Leo unatakiwa uondoe chochote kinachosababisha usimuabudu MUNGU kwa Roho na Kweli.
Unapoona Kichwa,  Kanisa, watoto, biashara, shamba, nyumba  anasababisha usije hata ibada za majibu usimtolee  MUNGU ujue vipo ndani ya moyo wako leo uwaondoe na uviondoe ukatae kabisa.
Jikague kuna mahali unajikuta unaongea maneno mengi badala ya NENO ujue kuwa ni kwa sababu ya walioko ndani ya moyo wako .
Kuna ambao mko hapa lakini kuna jambo ndani ya mioyo ambalo halitoki ili MUNGU akae leo kubali wewe mwenyewe likatae na uyakatae yote uliyowahi kufanyiwa  ambayo mpaka leo ukilikumbuka hata MUNGU Kristo Wakili wa MUNGU unawaambia wakae pembeni kwanza leo kubali kulitoa ili MUNGU akae ndani yako.
MUNGU anaangalia moyo kitu gani ukiguswa unalalamika unanung’unika unakwazika unanuna unakasirika unafura?
je ni fedha, mahali pa juu pa cheo kazi umri fedha kichwa kanisa watoto.
Hivyo kwa sababu wote tumekubali tumekiri kuwa kuna kitu tukiguswa ndani yetu tunashindwa kuvumilia basi yatupasa kutubu.
Leo tunatakiwa tutoe kila kitu kilichokuwa kimebaki ndani yangu/ yako / yetu badala ya Moyo mmoja wa MUNGU.
*MCHUNGAJI MMOJA ANAKAA KWENYE MOYO WENYE AKIBA NJEMA.*

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni