THAMANI NA FAIDA YA KUWA NA MOYO WENYE AKIBA NJEMA
MITHAL 4:23 linda sana moyo wako. ISAYA 57:15 MUNGU anakaa kwenye moyo uliotubu na kunyenyekea. Yer 29:11 Mawazo ya MUNGU ni mema kwetu siku zote.
Tunatakiwa tuwaze yaliyo mema kama MUNGU KRISTO na WAKILI wa MUNGU WALIVYO. ISAY14:13 Mawazo ya shetani kerubi ni mabaya siku zote.
EZEKIEL 28:17 Ukiwa na mawazo mabaya unakuwa na akiba mbaya ya moyo wako.
Moyo ndio unateketea na vitu vyako moto unaotoka ndani yako ndio unaua kila unachokifanya.
Mt 7:20-23 Kilichoko ndani ya moyo wako ndicho kinachokupa kuonekana ulivyo, moyo wako ukiwa na akiba mbaya huwezi kuona umuhimu wa mwingine wala huwezi kusifia au kukubali kazi ya mwingine.
LUKA 6:45 Mtu mwema katika akiba yake hutoa matunda mema na mwenye akiba mbaya hutoa matunda mabaya.
Leo tunamwambia MUNGU kama kuna chochote kibaya kinachotoka ndani yangu kinachotokana na akiba mbaya ya moyo wangu ukiondoe.
Aidha leo tumetoa Sadaka Maalum ya kufuta akiba mbaya ndani ya Moyo wako, kwa wenye haki, na kwa kanisa.
Sadaka hii inasimamisha akiba njema ndani ya moyo wa kanisa na kwa mwenye haki mmoja mmoja.
Akiba mbaya ni hatari mno katika maisha yangu. Akiba mbaya ndani ya moyo ndio husababisha moto utoke ndani yako na kuangamiza maisha yako au familia yako au kazi zako.
Lakini pia Sadaka hii maalum inafuta kabisa akiba mbaya ndani ya wenye haki kwa kusimamisha nuru zaidi ya Isaya 45:7 ambapo MUNGU kwa uhalisi kabisa anaumba nuru na ana huluku kabisa giza ndani yetu.
*AKIBA MBAYA NI UCHAWI ULIOKO NDANI YAKO MWENYEWE.*
Unatakiwa usimwangalie mwenzio kuwa ni mchawi, mganga, msengenyaji, ana tabia mbaya.
Unatakiwa usimwangalie mwenzio kuwa ni mchawi, mganga, msengenyaji, ana tabia mbaya.
Yesu alisema usiangalie banzi lililopo ndani ya jicho la mwenzako wakati kwako kuna boriti, toa kwanza boroti ndani ya jicho lako ndipo ukalitoe banzi ndani ya jicho la mwenzako.
Moyo wenye akili mbili, Leo tunaenda kuona akili mbili ndani ya moyo. Akili zinakaa kwenye moyo, akili zipo zinazotokana na moyo wenye akiba njema.
Kuna akili zinazotokana akiba mbaya, na kuna akili zinazotokana na akiba njema ndani ya moyo.
Sasa kumbe akili zinatofautiana, kuna yale uliyosikia na uliyoyaona wewe mwenyewe hayo hutengeneza store, hifadhi na akiba ndani ya moyo wako.
Unapowaza unawaza kile kilichopo ndani ya moyo wako na kilichoingizwa ndani ya akili yako.
KUMB 8:5 Nawe fikiri moyoni mwako, kufahamu una akiba gani ndani ya moyo wako/wake/wangu.
KUMB 8:2 Nawe utaikumbuka njia yako ambayo BWANA MUNGU wako alikupitisha ili ajue kilichoujaza moyo wako.
MUNGU alikuacha uone njaa, kiu, shida, taabu, aibu ikupate akuone umejaza nini ndani ya moyo wako.
MUNGU anakupima kwa kipimo chake kimoja cha moyo (tester).
Anakuacha ulale na njaa, kuna wakati unawasha mpaka shukrani unaikataa njaa na unasema njaa imefutwa kwa wenye haki kumbe MUNGU ndiye aliyeweka hiyo njaa ndani yako.
Anafanya hayo yote aone kama utaendelea kushika njia zake au utaacha.
MUNGU hawezi kukuacha huru mpaka akupime kwanza aone kama unaendelea kumpenda au umepata wengine wa kuwapenda.
Kumbe kuna majira ambayo MUNGU anakutest moyo wako. Kuna testa ya akiba njema na akiba mbaya.
Anakutesti kwa njaa au kwa namna yoyote apendavyo MUNGU.
MUNGU anajaribu moyo sababu yeye siku zote huangalia moyo.
MUNGU anakutweza kwa njia yoyote ile ili aone moyo wako.
KUTOKA 14:1- MUNGU aliwajaribu wana wa Israel hata wakae miaka 40.
Hata kipindi cha miezi 6 wapo waliolaumu kwa kuwa MUNGU alikuwa anatupitisha kwa kututweza ili aone, Je unampenda au ndani ya mioyo yetu kuna akiba njema?
Israeli walijaribiwa na MUNGU kidogo tu pasipo kujua kwa ni MUNGU anawajaribu maneno yaliwatoka, malalamiko, manung’uniko, mpaka wakakumbuka nyama, wali, pilau na vituguu saumu vya kwa farao.
Kuna saa MUNGU anaruhusu jambo lolote likupate ili aone, Je moyoni mwako kuna nini kimeujaza moyo wako? kwa kuwa kila mmoja huyanena yaujazayo moyo wake.
Walimlaumu Musa mpaka wakasema Yupo nje ya reli nini mbona tunaona mambo yamezidi, mafunuo yamezidi “as if” utafikiri wao wanaijua hiyo njia.
Maswali ya malaumu kibao wengine wakasema kapotea, mbona tunaomba MUNGU hajibu kumbe wapo kwenye examination na wamekutwa na akiba mbaya ndani ya moyo.
Unamuwazia jambo baya mwingine hata hayupo ila sababu moyo wako umekaa kujihesabia haki tu huoni kama unakosea leo tutubu na tuache.
Leo MUNGU unaona amekuja kuondoa akiba mbaya ujue kwamba ina maana kwamba kanisa tumeshavuka tayari.
Je unapoona unatoka Madhabahuni au kazini ukakuta vyombo vyote vimetolewa nje na mwenye nyumba kashaweka kufuli lake huku anasema sifungui bila hela yangu ule wimbo wa naona memaa… unakuja kweli au kitu kipi kinatokea?
Kanisa unakuta kichwa wako yuko na kahaba na hashituki anaendelea tu na mabusu hivi unakuja ule wimbo wa naona memaa….
Leo tujifunze kwa Wakili wa MUNGU; 7abibu 6 alikujaa na gitaa akasema leo ni siku ya kuimba kucheza kuruka maana wengi walisema siku hiyo ni Judgementday wakiimba na kucheza……
Yoh 21:13 Habari za kutwezwa zilimpata Petro akaamua kurudi kuvua samaki. Petro alifanya hivyo kwakuwa alikuwa na akiba ya kuvua samaki.
Ilibidi aondoe akiba yote ndani yake abaki na akiba ya MUNGU tu!!
ISAYA 49:15 MUNGU amesema mwanamke hawezi kumsahau mwanae, Lakini MUNGU hata akikutweza hawezi kukusahau.
Kwa hiyo ramani ya kanisa MUNGU aliijua tangu zamani kuwa siku ya leo tutafika hapa kwa kuwa alituchora kwenye vitanga vya mikono yake.
MUNGU alijua leo utavaa vazi ulilovaa leo, utawaza unayoyawaza, utakaa ulipokaa leo na utaelewa somo kwa viwango ulivyoelewa kutokana na akiba ya ndani ya moyo wako ikoje ni ipi.
Unapokanyagwa ni makusudi ili tuone moyo uliokuwa nao yaani MUNGU karuhusu kabisa!!!
Leo ukipata mtihani unatakiwa umshukuru MUNGU.
MUNGU kuna wengine aliwafanya wawe akina farao ili tuwe imara katika imani.
Kwa hiyo kizazi hiki hatuna majaribu bali tuna mtihani.
[A] Uwe na msamaha kila wakati. Usikumbuke yaliyopita, uwe mwepesi wa kuachilia na kusahau haraka.
Usiamke nalo na ukafika nalo wajibu ukashinda nalo ukarudi nalo huo sio moyo wa MUNGU.
Katika moyo wa MUNGU ni kuwa na msamaha 1Sam 1:12 Unatakiwa kusamehe kuachilia na kusahau yote.
*UKIWA NA AKIBA MBAYA WATU HAWAKUONI VILE UNAVYOJIONA KWENYE KIOO.*
*UKIWA NA AKIBA MBAYA WATU HAWAKUONI VILE UNAVYOJIONA KWENYE KIOO.*
Hana alikuwa akiomba lakini akiwa hajasamehe wala kuachilia hivyo mbele za MUNGU alionekana ni mlevi wa kutisha.
Ukiwa na akiba mbaya ndani ya moyo wako kila unachokifanya chochote kinakufa pia unaonekana kitu kisichofaa.
Utakuta mwalimu ametoa swali 1+1 na umeweka jibu 2 lakini akisahihisha akaweka kosa sio kwamba kakosea yeye kaona 4 kutokana na akiba ya moyo wako. Leo tubadilike MUNGU ametuvumilia mno.
Kuna mahali unatembea unajiona binti mrembo mzuri kumbe wote unaokutana nao unaoonana nao wanakuona wewe ni kijana au babu au bibi nk. Sura yako imerejea leo.
Moyo ndio huwa unapika, kichwa wako anaposema chakula ulichopika ni kibaya ni kwa sababu ya moyo wako ulioubeba.
Kila siku anakuambia upike kama Fulani ni moyo wala sio kwamba huyo Fulani ni hawala wake hapana, leo badilika.
Unapika huku unaongea sana karamu huwa mbaya, pika karamu kwa toba shukrani na imba na kucheza uone kama hajafurahia karamu yako.
Ukimpa shamba mwenye akiba mbaya mazao yote yanaoza, ukiuza dukani duka lote linafilisika na hajaiba na mahesabu yapo vizuri, ukimpa kitu wote wanakufa na wengine anawala yeye mwenyewe kituo hakiongezeki.
Moyo wenye akiba mbaya ni moyo usiozaa, ukiomba nao mito ya shukrani inakufa, ukimpa mwenye haki amlee anamuua, ukifanya nae biashara inakufa, hata ukimpa bilioni tilioni zote zinaisha zote bila kufanya chochote cha maana.
[B] Kibali, kiwango cha kibali unachokuwanacho kinatokana akiba ya moyo wako. Kiwango cha akiba njema ilioko ndani yako Zab 119:1-
[C] Kumcha BWANA ukiwa na akiba njema moyoni mwako ndipo unaweza kumcha BWANA.
[D] Nguvu ya kutamka jambo likatokea, Kung’oka kwa mlima mbele yako kunatokana na akiba iliyoujaza moyo wako MARKO 11:23
[E] Hakika ya NENO, War 10:9-10 Kwa kadri ulivyokuwa na hakika iliyojaa ndani ya moyo wako hukiri na kupokea yale uliyokusudia kupokea.
Isaya 55:11 MUNGU anasema kuwa kama mvua isivyorudi juu mawinguni ndivyo NENO analolituma kwangu lilivyo kwamba lazima litimizwe sawa na kusudi lake, halirudi bure.
Aidha tumeshiriki Karamu ya Akiba njema ambayo ni Sheria ya Roho wa Uzima.
MWAMBIE MCHUNGAJI MWEMA AKUPE AKILI YAKE ISIYOKUWA NA PANDE MBILI !!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni