Jumatatu, 30 Januari 2017


KUFUNULIWA KWA MOYO MMOJA PEKE YAKE KWA UHALISI

Nanyi mtakuwa wa MUNGU na MUNGU ni wangu/wako milele. EZEKIEL 36:26
Ni mahali tumefika  pa kuogopwa na kila kitu, waganga, wachawi, walozi, magonjwa umasikini ufukara kuishiwa  nk kwa kuwa tumekuwa wake MUNGU.
MAJIRA HII; Yeyote akija kwa hila utajua tu, atakayekubariki utajua tu kuwa Baraka hii ni ya namna gani, atakayekuja kwako utajua tu ujio huu ni wa aina gani!
WAEBRANIA 8:10-   MUNGU amesema kuwa atatutoa uchafu wetu kwa maana atafuta dhambi zetu na kutusafisha.
Mahali tulipofika hatasimama muovu wa aina yoyote.
Ndio maana anasema kuwa ataziandika sheria zake ndani ya moyo wangu/wako.
Sasa ni ile majira ya aliyemdogo na mkubwa kumjua MUNGU.
Aidha Sadaka Maalumu iliyosimamishwa leo ni kufunuliwa kwa Moyo mmoja peke yake kwa uhalisi.
Sheria ya MUNGU ikiandikwa ndani yangu /yako utajua tu kila kitu kilichoko mbele yako.
Sheria ya MUNGU ikiandikwa ndani yaa moyo wangu/wako MUNGU anaita utajiri uje kwangu na kuuongeza mbele.
Ni majira ya kuita karamu ije inakuja na maongezeko pia.
MUNGU atazidisha matunda ya mti na mazao ili usipatwe na njaa.
Atakuongeza ili usitukanwe kwa ajili ya njaa, maana tumefika mahali ambapo hatutukanwi tena wenye haki.
Kama walikuwa wanakuita tasa kuanzia leo wewe sio tasa tena milele, uliitwa masikini kuanzia leo wewe ni tajiri hutaitwa maskini tena.
Ni majira ya wewe mwenyewe kuichukia dhambi, hutatenda dhambi kwa amani milele.
NENO linasema amani haipo na haitakuwepo wa waovu watenda dhambi milele.
MUNGU atanitajirisha kwa ajili yake yeye mwenyewe.
Atakusafisha, atakutoa uchafu, ili uwe safi kwa ajili yake yeye mwenyewe.
MUNGU atanigharamikia kwa ajili yake yeye mwenyewe ili nifanane nae.
WAKILI wa MUNGU alimnunulia mavazi 7 mtendaji wake ili afanane nae.
WAKILI WA MUNGU alimvika vazi Mtendaji wake ili afanane  na yeye ili pia ukimuona Mtendaji ujue umemuona WAKILI WA MUNGU.
Hivyo MUNGU atanitengeneza vizuri kwa ajili yake yeye mwenyewe, atatengeneza agano lako, familia yako biashara yako kazi yako kwa ajili yake yeye mwenyewe.
Kwa hiyo itakuwa kwa kila anionaye atamuona MUNGU KRISTO NA WAKILI WA MUNGU ndani yangu.
Kila nitakapoenda watauona ule utatu wa MUNGU.
MUNGU hapendi kuitwa mchafu  ndio sababu analazimika kunisafisha kunitakasa kuondoa mavi walioninyea, mikojo walionikojolea, walivyoniharishia kwa ajili yake yeye mwenyewe.
Siku ile nitakapoitakasa …. Palipobomolewa…. MUNGU atapafanya kuwa pazuri.
Mahali pa mateso kudhulumiwa kudharauliwa kutukanwa MUNGU amepafuta ili niwe safi.
MUNGU anafanya haya yote kwa sababu majira zote 6 hakuwahi kuabudiwa wala hakuwahi kupata wa kumuabudu yeye katika roho na kweli.
*IBADA YA KUMTOA BINTI/KIJANA KIUNGU.*
Kwa nini tunamtoa binti na kijana kiungu?
Je ni lazima kumtoa binti na kijana kiungu??
Msingi wa ibada hii ni kile alichosema mwenyewe.
MWANZO 2:24 Mafanikio yako yapo katika kile MUNGU aliongea nasi alisema nasi alichoagana nasi,
Ukiwa nje ya kile alichosema MUNGU huwezi kukutana na mafanikio yako.
Lakini pia lazima ujiulize ya kwamba Je unaanzaje kwenye agano lako?
ZABURI 11:3 msingi ukiharibika mwenye haki atafanya nini? Mwanzo wa familia ukiharibika utafanya nini?
Msingi ndio unaoamua hiyo nyumba idumu kwa muda gani! Au hiyo nyumba iwe gorofa au ya ukubwa gani!
Maana msingi wa vyumba viwili huwezi kujenga gorofa ni mpaka uwe umejenga msingi wa gorofa.
Binti kijana anaposhindwa kutoa kwa wazazi ndipo tatizo linapoanzia, ndipo shida inapoanzia na ndipo taabu inapokuwepo.
Maana unakuta wameoana lakini wote wawili mioyo yao ipo kwa wazazi, moyo wa binti uko kwa baba na moyo wa kijana uko kwa mama.
Wewe ukikuta baba anayesema nitakurudisha kwenu ujue ni Yule ambaye moyo wa agano aliuacha kwa wazazi.
Hivyo hajui kwamba hata wewe kanisa wake ulitoka kwenye ubavu wake.
Akisema urudi umwambie kwetu ni kwenye ubavu wako, nawezaje kuwa na kwetu zaidi ya kwenye ubavu wako kichwa wangu.
utoke mahali pa uvulana na usichana; mpaka sasa kuna wazazi ambao bado wana usichana na uvulana.
Siku zote asiyependa kupika ujue huyo bado ana usichana anaona bora aende kibandani akanunue chipsi kupika aa!
Ukiwa mvulana pia unaweza kuondoka na kwenda popote bila kuaga.
Uvulana kupenda kula chakula cha gengeni, kuliko urudi ukale mlima wa moto kwa kanisa wako unasema aaa ngoja nikale kwa mama nitilie.
Usichana ukienda kwa rafiki yako ukiona muda umeenda unasema mimi nalala huku huku hata aibu huna umemuacha kichwa wako apumzike peke yake.
Kuna wababa ambao hata wakifuliwa mavazi wanakuja kurudia kufua kanisa akipiga pasi anakuja kurudia kupiga pasi huu ni uvulana kutomwamini kanisa wako.
1KOR 3:9 MUNGU kupitia Paulo alisema wa kila mmoja na aangalie jinsi anavyojenga huo msingi  ni msingi gani unajenga?
MUNGU amesema kuwa kijana anatakiwa atoke kwa wazazi wao  ataambatana na binti hao watakuwa si wawili tena bali ni mmoja 1+1=1.
HESABU YA MUNGU                                                                                                                NI 1+1=1
Hapa ndipo MUNGU alipowapiga chega wana mahesabu ya dunia na ulimwengu, sayansi, tenolojia.
Leo kijana na binti wanatoka kwa wazazi wao.
Pia wanatoka kwenye uvulana na kwenye usichana.
HESABU 30:1-  Kuna nadhiri ya binti kwa babaye, leo tunavunja ule uhusiano wa baba na binti ili binti akimuona kichwa amuone na baba yake huko.
Vile vile kijana anatakiwa akimuona kanisa aone amemuona mama yake, shida zote alizokuwa anampelekea mama yake akuletee wewe kanisa.
Na wa mama muwaachie vijana wenu musianze kusema ooh!!
Nilikuweka tumboni miezi 9 hapana kwa upendo wa MUNGU ili wawe na mafanikio mazuri mama baba muwaachilie vijana wenu.
Ulikuwa na swali muulize kichwa wako, muulize kanisa wakona vilevile wewe kanisa kichwa unapoletewa swali umjibu mwenzako vizuri kabisa.
Acha kusambaza maneno ya familia yako agano lako.
MITHALI 31:10- Kilichomponza hawa ni kwa sababu ya kuwa na kinywa chepesi kujibu ujuaji mwingi akajikuta anajibu hata maswali ambayo japo anajua lakini ilikuwa sio haki yake kujibu.
Kanisa mwema hakai kwenye nafasi ya kichwa wake.
Ukikuta mama anayekaa kwenye nafasi ya kichwa wake mwangalie vizuri utakuta hata agano familia yake haipo vizuri.
Agano linakuwa na mafarakano muda wote, watoto na wazazi hawaelewani muda wote.
Ukikuta kichwa kavaa vibaya shida ni kanisa, kichwa kanisa unatakiwa kuuweka wazi mwenzio.
Kanisa unatakiwa kuamka mapema kabla usiku haujaisha, usikubali kichwa aende kazini bila kunywa mtamu tamu.
Uongee kwa hekima, acha umbeya, maneno maneno.
Usiwe msemaji zaidi kuna wakati unatakiwa useme hili naomba ajibu kichwa wangu.
ISAYA 6:9 ufalme upo mabegani mwake, vichwa ni wafalme.
Ukijifanya mkali unasababisha na baba awe mkali bila sababu.
Jifunze kukaa kimya, acha baba aseme kwanza. Kanisa isifike mahali ukawa muamuzi wewe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni