Ijumaa, 6 Januari 2017



MADHABAHU YA UMOJA WA MUNGU, KRISTO NA KANISA


Wakili wa MUNGU leo amesema tumefika mahali pa kuachana na umbo la vizazi vilivyopita Mdo2:34- kwani lile umbo la mwili lilisababisha Kristo kwenda mbinguni na maadui ndio maana aliambiwa kaa pembeni kwanza mpaka maadui zake awaweke chini ya miguu.

Utawala wa amani umesimama na MUNGU amekuja ndipo adui anakimbia uso wa MUNGu kwa mimi kutolipa kisasi kwa kuwa kisasi ni cha MUNGU.

Aidha Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kujenga madhabahu ya umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa 1wafalme 13:4-6.

Kwa sadaka hii itadhihirisha wazi wale wenye wepesi wa kuonea wengine na kupiga wengine na kusema "yeyote anayetaka kukupiga kofi mkono utakatika, atakaye kunyoshea kidole mkono utabaki hivyo hivyo na atakayeomba maombi mabaya na kumsengenya mwingine mdomo utaenda upande na atakuwa bubu".

Aidha kabla ya kutoa sadaka maalumu hiyo alilivua Kanisa mwonekano wote wa zamani kwa Toba ilithibitisha MUNGU yupo juu ya nchi yaani anayekugusa akutane na MUNGU kwa kushughulikiwa saa hiyohiyo. Lazima kuhakikisha mwenye haki analindwa na jambo hili lazima litokee.

Amesema dunia ilichukua nafasi ya MUNGU kwa kuchukua namba moja ili kanisa lisifike majira ya saba tuishie majira ya sita kwa mahesabu ya saba kutoa moja kanisa likabaki na majira ya sita hadi hapo MUNGU alipolifunulia kanisa kuhusu majira ya saba na sasa tumeingia kwa uhalisi maana namba moja imepatikana.

Hatahivyo alifanya ufafanuzi wa vizazi vyote na utawala wake kuwa kizazi cha kwanza hadi cha nne kilitawaliwa na mwili,viungo na umbo.

Alisema viungo ni vya ndani, kwa nje ni mwili na umbo linaonesha tabia yako ambapo kulikuwa na ushirikiano kati ya mwili, viungo na umbo ambao sasa tunaushirikiano wa MUNGU, Kristo na Kanisa lakini ni baada ya kufuta ushirikiano wa mwili, viungo na umbo.

Amemshukuru MUNGU kwa kizazi hiki kuwa juu ya mwili, viungo na umbo ambapo sasa Kanisa kwa ushirikiano wa MUNGU, Kristo na kanisa halina mwili, viungo wala umbo ambapo sasa MUNGU yupo kila mahali mwenye haki alipo na anafanana hivyo hivyo ilimradi mwenye haki huyo anatenda kwa haki.

Aliyataja Mambo ya kushughulikia ili kufuta kabisa mwili, viungo na umbo kwa kila mwenye haki kuwa ni pamoja na:-
Moyo- kwa kuungana na moyo wa MUNGu

Kiuno- kufunua mambo mazuri.

Tumbo-lizae vitu vizuri.

Macho-yaone mazuri tu.

Kifua- tupokee haki ya MUNGU.

Damu- kuugua, magonjwa hayapo tena.

Pumzi- utamke Baraka.

Mabega- yawe ya haki, furaha na amani.

Masikio- kusikia NENO na lizae matunda.

Kitovu- kurithi kutoka kwa MUNGU.

Uti wa mgongo-tumaini lako liwe MUNGU tu

Ulimi- unene NENO tu.

Sauti- yako iungane na sauti ya saba.

Mikono-kazi zote ziwe kwa utukufu wa MUNGU.

Koromero- utoe sauti ya MUNGU tu.

Aidha Wakili wa MUNGU alihitimisha ibada hiyo kwa kufafanua umbo la kufuta katika agano la kichwa na kanisa lililokuwa likimzuia MUNGU asitamalaki katika familia ambalo akaliita Umbo la bustani ya edeni.

Alisema hilo ni la kila mmoja ndani kanisa analotakiwa kulifuta kuwa ni kwamba Adamu ingawa alipewa maelekezo yote na MUNGU kuhusu kila kitu cha kulima na kutunza bustani ya edeni lakini yeye hakutoa taarifa na maelezo yote kwa mkewe Hawa na kusababisha kukalia kiti cha aliyepewa maelekezo yote ambae ni Adamu.

Hata hivyo Wakili alisisitiza kila mmoja kutanguliza toba ya kina kuanzia bustani ya edeni kwaajili ya kichwa kutokutoa taarifa kamili kwa kanisa wake, kanisa kukalia kiti cha kichwa na kichwa kikalia kiti cha kanisa kwa lengo la kurejesha Mlima wa Bwana na mahali pa Bustani ya Edeni kwa uhalisi Ezek 28:15 na Mwa 2:15.

Na ndipo alijenga Madhabahu hiyo ya Umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa ambayo itasimamishwa kwa siku saba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni