Ijumaa, 6 Januari 2017




THAMANI NA FAIDA YA KUACHANA NA UMBO LA KWANZA LENYE UHARIBIFU.


Wakili wa MUNGU amesema Hatma ndio kusudi la kila mmoja ambalo amemkusudia kwani majira hii Kanisa linatakiwa kuwa juu ya Umbo ambalo ulianza nalo.

Kuna jinsi MUNGU atakutoa kwenye Umbo la kwanza maana kila ulichonacho kina nafsi na mahali MUNGU alipotupeleka ni juu sana mahali alipotukusudia tangu mwanzo.

Aidha Wakili ameongoza Wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kutengwa na mwanzo wa umbo lenye uharibifu.

Hatahivyo  ametaja sababu za MUNGU kutupeleka juu zaidi ya viungo kuwa ni pamoja na kututenga na wale ambao wamekataa kuhama vituo na kutupeleka mahali ambapo hakuna umbo.

Maana tukiwa na umbo ni rahisi kupigwa na Yule mnyama mwenye umbo lisiloeleweka maana mahali tulipo ni juu ya viungo nilivyoanza navyo. Watoto wapo juu ya viungo vilivyoanza.

Nitaanza kupendeza zaidi. Maumivu ya kizembe zembe hutayasikia ndipo utakapo kuwa juu umehama kituo.

Hatma ya ila Mwenye haki atendaye kwa haki 1Yoh 5:8-9

Kumkamilisha MUNGU. Maana MUNGU ni MUNGU lakini bila Kristo na Kanisa hakamiliki. Ukamilifu wa MUNGU unakamilishwa na Kanisa.

Umoja wa MUNGU unakamilishwa na Kanisa. Namba 1 aliyokusudiwa na MUNGU na inakamilishwa na Kanisa. Hiyo namba 1 ni Kanisa.

Kwahiyo kama ulikuwa huliombei Kanisa sasa utaliombea. hatma 1 halisi ni kumkamilisha MUNGU.

Kuhakikisha Kristo anatawala na Kanisa  juu ya nchi.

Uf 20:6. Ufu 22:4 watamuona uso kwa uso akiwa nyumbani kwako, shambani kwako nk.

Ukitembea kwa mguu
                    Kwa ndege} 
                    Kwa gari    
MUNGU ataonekana hivyo hivyo.

Haya yalikuwa hayawezekani mpaka utoke kwenye umbo la 1 la uharibifu na uingie juu zaidi  pasipo kuwa na umbo lililotangulia.

Mwa 18:1 ilitokea Israel kwa Ibrahimu majira hi MUNGU anataka tuonekane kila mahali tukiwa na MUNGU na Kristo.

Math 19: 23-25 Israel ya mwilini ndio ilikuwa urthi wake. Hawataki taifa hili liitwe urithi wa MUNGU. Hawataki Hatma halisi ya Kanisa kwani utajiri halisi utaonekana ndani ya taifa kwa sababu ya nguvu ya hatma ya Kanisa.

Ukikutana na anayezuia mafanikio haya utafanyaje? utampeleka kwa MUNGU amtambue yeye mwenyewe.

Hivyo shukrani zetu zibadilike ili haya yote yatokee kwa amri moja halisi.

Watakusalimia kwa heshima. Wataona wewe ndiye chanzo cha thamani nzuri. Hazina lulu na juya.

Milionea, trionea na bilionea huwa wanajifanya ndio madini, fedha, uchumi.

Kama umekubali kuwa na zaidi ya umbo la 1 basi utaonekana kuwa thamani halisi.

*NB:-*Karamu ya leo imegeuzwa kuwa ni Sheria ya Roho wa Uzima inayonitenga kabisa na sheria ya mauti.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni