KUISHI JUU YA UMBO
WAKILI wa MUNGU leo ameanza ibada kwa kujibu maswali mawili ambayo jana aliulizwa na Wakamilifu kwa lengo la wote tupate ufahamu kwa pamoja.
Swali aliloulizwa ni “kanisa tunafuta umbo la nyoka lakini umbo la nyoka hatujawahi kuliona kanisani?”
Akajibu kwa kusema “nyoka ana ndimi mbili, maana yake ni:-
1.) ulimi mmoja ni wa mema.
2.) ulimi wa pili ni wa hila.
Alisema tunaposema umbo la nyoka maana yake ni hila. Kanisani kulikuwa na wenye ndimi mbili. Hivyo MUNGU amefuta wale wenye ndimi mbili kanisani.
Hao wenye hila walikuwa wanachaua wenye haki wasimfahamu Wakili ni nani kwasababu wanajua usipo mfahamu huwezi kupokea kutoka kwa MUNGU.
Swali la pili:-
Nitajuaje kama nina umbo la nyoka ? alijibu kuwa kulikuwepo na waliouza nafsi zao kwa kujua na wengine waliibiwa bila kujua.
Wapo waliouza nafsi zao kwa kerubi wakaja kanisani wakiwa na moyo na roho hawana nafsi ili waishi lazima waibe nafsi ya wenye haki kwa kuwavulia matakataka yao hivyo ndivyo MUNGU amefuta kuibiwa.
Hatahivyo aliongoza wenye haki kutoa sadaka Maalumu ya wote kuja kujisalimisha kwa MUNGU Madhabahuni kwakuwa MUNGU ni halisi, waabuduo halisi na kanisa ni halisi.
Sadaka hiyo inarejesha wote waliondoka kwa kudanganywa ikiwa ni pamoja na kuwaleta ndugu zetu tunaotaka waje kwa MUNGU Aliyetuma wote.
Aidha Wakili wa MUNGU ametaja aina za chujio la Haki ambalo kanisa tumepitishwa na MUNGU mwenyewe hadi kufika mahali pa kizazi cha MUNGU kimefika:-
1.)Chujio la kutenga kondoo na mbuzi. Mbuzi na kondoo hao kuchujwa kupitia malaika wa MUNGU, kristo na wa Wakili wa MUNGU.
2.) Chujio la Toba ya MUNGU. Ambayo imeondoa magugu.
3.) Chujio la umoja wa Baba, Kristo na Kanisa kutusafisha kwa upya ili kuondoa umbo la nyoka.
Mt 12:32 makuhani wa MUNGU kizazi cha MUNGU ni Roho atakae mgusa anashuhulikiwa na MUNGU mwenyewe.
UMBO
Wakili wa MUNGU amesema tunapozungumzia umbo maana yake ni zile tabia tulizokuwa nazo kutoka kwenye kabila, koo, lugha, taifa nk.
Lakini MUNGU anataka wenye haki tutoke mahali pa umbo laaina yoyote na tuende kuishi juu ya umbo maana umbo linasababisha tusimwelewe MUNGU.
Mwanzoni kanisa tulikuwa tunajipatanisha au kuungana na Nabii yaani hapo Nabii alikuja kwakuwa alitumwa lakini Sasa hatuungani tena bali tunamwalika Wakili wa MUNGU ili kuja na jeshi lote la MUNGU hapo ulipo.
Amesema tumekuwa tukishindwa kuwaleta wengine kanisani kwasababu tumekuwa na umbo kama wao wakati tunatakiwa kuishi juu ya umbo.
Faida ya kuishi juu ya umbo ni pamoja na:-
#kutetewa na MUNGU na uumbaji wote.
# Mhub3:14 Najua maana yake Hakika (ufahamu)kila anachofanya Wakili ni MUNGU anafanya.
#Kila kazi aifanyayo MUNGU itadumu milele. Kuzifuta kazi hizo haiwezekani.
#Hauwezi kuiongeza kitu chochote.
#Hauwezi kupunguza kitu.
#MUNGU amefanya hivyo ili wamche yeye.
Mhubiri 3:17-22 Wakili wa MUNGU alichukia kuishi kwenye viungo na umbo kwa kuwa hakutaka kufanana na mnyama.
Aidha amemtaka kila mwenye haki kukubali kuhama kuishi kwenye umbo kwani kuishi kwenye umbo ni maisha ya kufanana na mnyama hivyo uishi juu ya umbo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni