Ijumaa, 6 Januari 2017

      HATMA MOJA HALISI

Wakili wa MUNGU amefunua kuwa ilikupata hatma moja halisi ni lazima kutubu kwaajili ya kufuta Agano la mfanano milele na kufuta umbo la kwanza milele.

Wakili wa MUNGU amesema Leo kitabu kinaandikwa na tofauti kati ya mwenye haki na mwovu lazima ijulikane. 2.) anayemtumikia Bwana na asiyemtumikia lazima ajulikane.

3.) Sasa  mimi nimeachiliwa kuwa hazina ya MUNGU. Amesema MUNGU anataka wote tuwe na hatma moja halisi. Na iwapo tukiwa na hatma moja hakuna mwenye kumkanyaga mwingine.

Kila mmoja nyumbani kuwa na amani na furaha kwa afya nzuri itokayo Madhabahuni. Hatma moja halisi ni zaidi ya viungo. Na ukishatoka kwenye umbo la kwanza utaona ugonjwa uliokuwa unakusumbua unakukimbia.

Aidha Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya Madhabahu iliyosimamisha hatma moja halisi zaidi ya viungo.

Sadaka hiyo inakutoa kwenye hatma ya kwanza na kukupeleka hatma moja halisi. Inakutoa kwenye umbo la kwanza na kukupeleka kwenye juu ya viungo.

Hata umbo la kwanza la MUNGU, Kristo, Wakili wa MUNGU,  kizazi na Taifa tunatoka hapo na kuwekwa kwenye hatma moja halisi juu ya viungo.

Efeso 1:18  macho ya mioyo yetu yatiwe akili yapate kuona. Kushukuru kwaajili ya kuwa:-
+ Mti wa uzima.

+Na njia ile iendayo uzimani tunayo.

+Hakuna anayepita katika njia hiyo.

 Awali akijenga msingi Wakili wa MUNGU amevitaja na kufafanua vituo ambavyo Kanisa tumepita katika mwezi siwani mwaka 6.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni