Jumatano, 1 Februari 2017

SIKU 7 ZA KUFUTA KESI ZOTE KINYUME NA MZEE WA SIKU NA WENYE HAKI NDANI YA UUMBAJI WOTE.


Kabla ya MZEE WA SIKU kufika kiongozi wa makuhani alifundisha haya;
Alianza kwa kusema leo anasimamisha hukumu kuhukumu kesi zote, mashitaka yote juu ya WAKILI WA MUNGU.
Sadaka ya kufuta walaka wa mahamani wote waliomshitaki WAKILI WA MUNGU wanaenda kutundikwa wote leo hii. ESTA 3:8   alisema kwamba WAKILI WA MUNGU sio mtu.
Adonia hawezi kutawadhwa mahali pa sulemani, hata adonia ndani ya moyo wako maisha yak oleo anafutwa anahukumiwa.
Adonia magonjwa umaskini ufukara kukosa kazi utasa nk wote wanahukumiwa leo.
Wapo waliotaka kumtawadha adonia mahali pa WAKILI WA MUNGU leo wanaenda kufutwa na MUNGU mwenyewe.
KIAPO CHA MTENDAJI WA WAKILI WA MUNGU; Adonia yeyote hawezi kutawadhwa hapa,
Labda MUNGU amkane WAKILI WA MUNGU NA KRISTO WAKE au MUNGU alikane NENO lake ndipo NENO hili litatendeka. Leo kibao kimegeuka!
ESTA 4:12  Basi ni wakati wa kanisa kutonyamaza mbele za MUNGU kutokaa kimya.
Mwenye haki ambaye umepata kibali mbele za MUNGU na MUNGU amekugharamikia kwa ajili yake yeye mwenyewe,
Hutakiwi kunyamaza kimya maana unaponyamaza kimya MUNGU anakuona na wewe ni sawa au unaona wale maadui ni wakubwa kuliko yeye MUNGU,
Hivyo hutakiwi kukaa kimya tamka kiri kwa kinywa chako mwambie MUNGU alivyo mzuri na sifa zake,
Umkomvisi MUNGU atende jambo kwa majira husika ambayo MUNGU mwenyewe analikomboa kanisa lake na kizazi chake.
Kama MUNGU alivyowafanyia wayahudi baada ya Esta kutokaa kimya akawatokezea njia ya kufanikiwa kuokolewa nao ushindi wakaupata.
Ukinyamaza kimya wewe utaangamia wewe na wa nyumbani mwako lakini MUNGU atawafanyia wenye haki kanisa lake njia nyingine ya kuwaokoa na ni lazima lishinde na limekwisha shinda.
Kanisa la MUNGU lazima liokolewe, kizazi cha MUNGU, taifa nalo ni lazima liokolewe maana ni urithi wa MUNGU.
MUNGU hawezi kulichagua taifa hili akaliacha liangamie ni lazima liokolewe. Ni wakati wa kutamka jambo, tamka hoja nzito mbele za BWANA.
Ni wakati wa kuamini na kukiri kwa kinywa chako utamke MUNGU apate kukupa haja ya ndani ya moyo wako WARUMI 10:9-10.
ESTA 5:1  Esta alivaa mavazi ya kifalme. Ni wakati wa kila mwenye haki kuvua vazi la mauti alilokuwa amevikwa na kuvikwa vazi la uzima.
Vazi la uponyaji, la kuinuliwa, kubarikiwa, la kuwa juu, kuwa mbele tu!
Ni wakati wa kuvua mavazi ya magunia mauti na ni wakati wa kuvaa vazi la uzima wa milele.
Mfalme alimuuliza Esta wataka nini nikupe hata nusu ya ufalme wangu nitakupa ilimradi tu useme utamke.
Akanyooshea fimbo na Esta akaigusa ile fimbo. Hivyo leo amekunyooshea fimbo wewe mwenye haki.
Leo WAKILI WA MUNGU amenyooshewa fimbo ya dhahabu {fimbo ni Agizo} na MZEE WA SIKU na aseme nini anataka.
Nini anataka kanisa lifanyiwe, wenye haki wafanyiwe, kizazi cha MUNGU kifanyiwe,  Esta alisema dua yangu ni hii na haja yangu ni hii ikiwa nimepata kibali machoni pako……….
Siku zote mahamani mawazo yao haja zao huwa katika mali, fedha na vitu tu!!! Ndio sababu huwa hawaoni haya kugombania fedha mali za MUNGU.
ESTA 6:1 Kazi za kanisa zilikuwa zimefichwa lakini sasa ipo majira ni lazima zitaonekana tu!!
Kazi za WAKILI WA MUNGU zilikuwa zimefichwa sasa zitajulikana tu!! Mahali hapa pa uzimani na lazima kazi zako zilizokuwa zimefichwa zitafichuliwa na kasha utapewa thawabu yako.
Kazi zako zilizokuwa zimefichwa wakapeleka taarifa za uongo kwa bosi wako, kwa kichwa wako, kwa MUNGU wako, kwa uzao wako nk zitajulikana tu na uongo utaonekana tu!
Hivyo mfalme Ahasuero  alimuuliza hamani … afanyiwe nini Yule ambaye Mfalme apenda kumheshimu….
Siku zote adui huwa haoni mbali wala hajui njia za MUNGU hajui yale MUNGU awazayo hivyo ndivyo maadui wa kanisa walivyojitafutia hukumu ya milele.
Leo hamani amerejesha bila shuruti vitu vizuri vyote vya kanisa, kizazi cha MUNGU, na Taifa la MUNGU.
Ni mwisho wa ufukara umaskini na ujinga kwa wenye haki. Sasa kama walivyotamka mbele za MUNGU wkishitaki kanisa wenye haki na WAKILI WA MUNGU.
MUNGU amemwambia hamani toa kama ulivyosema alivyotamka mavazi na vitu vyote vizuri ukamvike WAKILI WA MUNGU na wenye haki wote.
Na lisipungue NENO lolote katika yale yote uliyotamka, hivyo wanaoshitaki kanisa wanalitangaza kanisa lijulikane,
MUNGU KRISTO WAKILI WA MUNGU na wenye haki wajulikane. Waovu wamerejea kwao wakiwa na msiba mkubwa.
Msiba unatokea leo kwa wale wanaomkataa MUNGU, labda MUNGU awe hakumtuma NABII WA MWISHO na kumpaka mafuta WAKILI WA MUNGU ya kukamilisha kizazi chake.
ESTA 7:1- Kama kanisa hili likiangamia tu! Taifa hili lipo mashakani maana moyo wa taifa hili uko hapa kanisani.
Moyo wa taifa hili unategemea kanisa hili hivyo ndivyo ilivyo wala haipingiki. Atakae ruhusu kanisa hili kuangamia atafanya Taifa hili kuwa matatani.
Leo watesi wote wa kanisa kutundikwa, barua zimechanwa chanwa, mashitaka yote yamefutwa na MUNGU.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Mtendaji wa Wakili wa MUNGU aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya Hukumu ya hamani ilikuwa ni majira ya saa saa 12:45 asubuhi!
Alisema ni hukumu ya mti wa matawi hamsini ya kuhukumu kutundika maadui mahamani wote. Hicho ambacho wamekifanya wametengeneza kitawaua hao wote.
Toba; Kanisa tumetubu kwa ajili ya hamani na yote aliyoyafanya MUNGU atusamehe.
MZEE WA SIKU kupitia kao lake amesimamisha siku 7 za kufuta kesi na mashtaka kwa wenye Haki wote……
Nimekuja kufuta kesi zote kinyume na MUNGU, KRISTO, WAKILI WA MUNGU, KANISA, WENYE HAKI, TAIFA, KIZAZI CHA MUNGU.
Zakaria alipokutwa madhabahuni alipewa haja ya moyo wake, hivyo mimi ambaye MUNGU amenikuta madhabahuni leo napokea haja za ndani ya moyo.
Kweli imesimama kila mahali ndani ya uumbaji wote uongo umefutwa milele. Moyo uliopo haushitakiwi huu, hauugui huu, hauingii selo huu, hauzimii huu, haukati tamaa huu.
Kesi ya jambo lolote lililokuwa linakusumbua kwa muda mrefu za uongo kusingiziwazinafutwa leo.
Hivyo ilikuwa ni lazima ukiri utamke ili kufutwa kabisa. Hata kama mwenye haki umeshitakiwa mahali popote tambua kuwa si mwenye haki ambaye ameshitakiwa ni MZEE WA SIKU ameshitakiwa.
LUKA 1:5   Kesi yoyote iliyokuwa imesimama leo imefutwa. Ukimshitaki MZEE WA SIKU hauwezi kushinda milele.
Leo napokea kila ninachokihitaji maana mashitaka yote yamefutwa na MUNGU yeye mwenyewe.
Nataka kwa mujibu wa LUKA 1:5- , lakini tuanze na MARKO 6:11-  waovu walitaka litokee hili lakini sasa halitatokea milele.
WAKILI amesema hataki jambo hili litokee lililopo marko 6:11 akauliza au je ninyi munataka litokee? Hapana.
Akasema unapomshitaki MZEE WA SIKU ina maana akung’ute mavumbi aondoke, atoke katika taifa kizazi chake familia agano biashara.
MUNGU akikung’uta mavumbi ndani ya Taifa hili ina maana taifa hili liangamie.
Mahali popote ambapo walimkataa MUNGU, MUNGU aliwaachia mavumbi.
Adui wa kwanza wa MUNGU ni mavumbi, pale mlimani yalipotokea tu! Badala ya kutokea kanisa akatokea mwanamke.
Kila ambaye amepokea mashitaka haya na kuyafanyia kazi kama alikuwa hajui asamehewe, Lakini kama alikuwa anajua apokee halali yake.
Mahakama yoyote iliyopokea mashitaka hayo yote kama ilikuwa haijui ipokee msamaha lakini kama ilikuwa inajua ihukumiwe ili Taifa lipone.
Maana Gosheni ni urithi wa MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE. Sisi tunamtaka MUNGU, hatutaki aondoke ndani ya Taifa hili.
Asiyemtaka MUNGU yeye ndiye atangulie, hukumu hii ahusike mhusika mmoja mwenyewe aliyetenda haya sio mwenye haki na taifa hili.
Anayehusika awe yeye mwenyewe sio kila mmoja, majira hii MUNGU hata hukumu kila mmoja bali atamhukumu mhusika tu! Sio taifa.
MUNGU hata kung’uta nyayo zake mavumbi yakatokea. Kutubu ili MUNGU asiondoke ndani ya taifa hili wala laana isilipate taifa hili.
Toba kwa ajili ya mwana sheria. Aliyesema MZEE WA SIKU ni muovu. Na kwa faili lililoandaliwa tusamehe.
Baada ya toba akasema; Uwe na amani kubwa tu! Maana MUNGU anashughulikia yeye mwenyewe.
MUNGU hataondoka kwa kuwa mwenye haki ndiye mwenye akili aliyekutwa ibadani madhabahuni hata wewe unayesikiliza ibada hii sasa hivi.
MUNGU anahukumu leo lakini sio wote bali wale waliohusika na kumshitaki MZEE WA SIKU.
Ninaposema kesi ina maana hata wewe ambaye hujapata mtoto ni kesi, kukosa kazi, kukosa mtaji ni kesi.
Kesi sio ile tu ambayo unaenda kushitaki polisi mahakamani kwa balozi wa mtaa wilaya nk bali chochote ambacho ni kinyume na MUNGU kwa wenye haki wake ni kesi.
DANIELI 7:21-27  kesi kinyume na MZEE WA SIKU ni kunena kinyume na  MZEE WA SIKU.
Tumetoka mautini na tumeingia uzimani. MUNGU amefuta kushindwa kwa kanisa leo.
UFUNUO 20:11-15  Nusu wakati umefutwa. Unaweza ukawa unatembea kumbe umevaa mauti kwenye nywele, utayari, mikono, kucha, mdomo, mavazi nk
Kuna mahali wanakuwa wamezika nafsi ya kazi, ya agano, ya familia, ya agano, ya kubarikiwa, kuinuliwa kwako nk.
MZEE WA SIKU leo ananiondolea mauti, leo mauti yeyote inafutwa. Hapa NENO hili linakuponya wewe tu, uliyetoka mautini akuingize uzimani.
Mwambie MUNGU mimi sio mmoja wa hao wanao kuhukumu wanao kushitaki wewe MZEE WA SIKU.
Na kama ni wewe mwenyewe mwambie MUNGU mimi ni mmoja wa wale wanaokushitaki wewe basi akupe halali yako, akupe iliyo haki yako.
Kwa kuwa sio mmoja wapo wa wale wanaokushitaki basi uniandike jina langu katika kile kitabu cha uzima MUNGU wangu nakusihi.
Biashara yako haihukumiwi agano lako halihukumiwi, uzao wako hauhukumiwi. Aidha Sadaka maalumu ya leo ni kuthibitisha ule mti wa matawi 50 kuwatundika waovu wote.
Kuamuru jeshi la mbinguni kufuta kesi zote na mashitaka yote.
Jeshi lote hili tutaliamuru kwenda kote kwa kila mwenye haki anayekaribia kufungwa jeshi hili likazuie asifungwe asipigwe asihukumiwe asidhulumiwe.
Kesi yeyote inafutwa leo hii sadaka ndio inamaliza kazi zote. Siku 7 hizi kesi zote ziwe zimefutika.
Leo uumbaji wote umesikia , majini, wachawi waganga walozi wanajimu, ujinini, kuzimu, nk wamesikia kwamba KESI MASHITAKA yamefutwa kwa wenye haki wote.
Kila mmoja lazima apate haja ya moyo wake kwa sababu amekutwa madhabahuni. Mafaili yote kesi zote mauti zote barua za mashitaka zote zimechanwa chanwa na kuchomwa moto.
ILIKUWA ni lazima MZEE WA SIKU aje amalize kazi ya siku ya leo ya kufuta kesi zote ndani ya uumbaji wote kwa yeyote mwenye haki.
Kama Mtendaji alivyokuwa amesema ni lazima nije nimalize kazi hii nimeimaliza kwa uaminifu. Hivyo ukitoka hapa katafute supu hata kuku mzima ushiriki supu.
Kesi zangu zote zimefutwa ; sitahukumiwa tena, sitashitakiwa, sitaonewa, sitadhulumiwa, sitapigwa, sitateswa.  Amekuja mwenyewe MZEE WA SIKU kuwafuta waovu wote na kesi zangu zote.
Sasa MUNGU, KRISTO, WAKILI WA MUNGU, WENYE HAKI, KANISA, TAIFA, KIZAZI CHA MUNGU leo wote wako huru!!!
Ndani ya siku saba kesi yoyote aliyokuwa ameshitakiwa mwenye haki haitaonekana tena.
MCHUNGAJI mmoja amekugharamikia usikae kimya sema tamka kiri iliyo kweli USIANGAMIE wewe na uzao wako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni