Ijumaa, 3 Februari 2017

THAMANI NA FAIDA YA MOYO WA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.

Kabla ya MZEE WA SIKU ndani ya WAKILI WA MUNGU kuja kufuta wa waliokuwa wanahifadhiwa ndani ya moyo wa mwenye haki, Mtendaji wa Wakili wa MUNGU alisema kuwa;
Mahali tulipofika kanisa hatutakiwi kujihesabia haki, muda wote tuwe wenye haki wa toba, kutubu na kuinua taifa na viongozi wote wa nchi;
Kwamba kila kitu wanachofanya wafanye kwa utukufu wa MUNGU wakimtanguliza MUNGU kwa kila jambo wanalolifanya.
Alisema kama Esta alivaa magunia basi alikuwa kwenye toba ili aliokoe Taifa la MUNGU.
Na wewe leo kaa kwenye toba ishi kwenye toba ili kuvusha familia yako, agano lako, kazi yako, biashara yako, safu yako, uimbaji wako, sauti yako nk kwa njia ya toba tu! Ndio utafanikiwa.
MUNGU anapenda moyo unaotubu na kunyenyekea mbele zake, hivyo tukitubu tu MUNGU anakuja yeye mwenyewe kutupa haki kwa sababu tumetubu kwa kukiri na kutamka udhihirisho ni lazima.
Bila toba MUNGU hawezi kuishi na wewe hawezi kuja kwako, hivyo ili huyu ALIYETUMA WOTE aje kwako ni lazima uwe na; toba binafsi, toba ya kweli, toba ya vizazi vyote, toba ya Kristo na toba ya MUNGU.
Silaha kubwa 2 ni toba na unyenyekevu. Pale unapoonewa jambo la kwanza ni toba  na unyenyekee zaidi kusudi ni usiingiwe na kujitetea na kujihesabia haki.
Kwa kuwa kinachokupa haki si wewe kujitetea bali ni toba ambayo inamleta MUNGU kukutetea na huu ndio utakatifu katika kizazi cha MUNGU.
Kilicholeta mauti ni dhambi na kinachoondoa dhambi na mauti ni toba pekee naa si vinginevyo.
Kwa hiyo kama ulikuwa unaichukia toba mimi nafikiri uanze kuipenda tu! Maana ndio inayokutoa kwenye kila aina ya mambo mabaya.
Toba halisi inaondoa mauti War 5:12, Mt 21:37  wakasemezana wakisema na tumuue tuutwae urithi wake, walimkataa, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na wakamuua.
Mwa 4:1- kwa sababu ya nyoka aliyekuwa ndani ya adamu na hawa hata mtoto aliyezaliwa wa kwanza alikuwa nyoka, kaini.
Tunaona kuwa kaini alikuwa mkulima lakini alikuwa anamtolea MUNGU sadaka ya mavuno ambayo yamechoka yaliyodhoofika nayale manono alikuwa anabaki nayo.
Lakini mzaliwa wa pili alikuwa Habili nae ni mwenye haki mbele za MUNGU alikuwa mfugaji mzuri na alimtolea MUNGU siku zote sadaka iliyonona.
Hivyo MUNGU aliitakabali sadaka ya Habili kuliko ya kaini, kaini alipoona ya kuwa MUNGU anazipenda kuzikubali na kuzipokea sadaka za nduguye kaini wivu mbaya na hila ukamkamata na kujifanya mwema hivyo akampeleka nduguye uwandani akamuua huko.
Hivyo tambua leo kuwa kabla ya adui yako kukuua anakutoa kwanza kwenye urithi wako uliopew na MUNGU,
Utasikia kuna wanaokukatisha tama na kukuambia yaani tokea umeenda huko kanisa huna hata fedha, kuna mwingine anaambiwa na kichwa wake usiende tena siloamu , kanisa la mapepo, freemason ink ilimradi tu akutoe kwenye urithi wa MUNGU kwenye kusudi la MUNGU.
Adui wa kwanza wa MUNGU ni vumbi ambalo lilimtoa kanisa kwenye urithi wake. Mahali pa juu pakamtoa kerubi kwenye urithi wake, kerubi akamtoa adamu kwenye urithi wake kwa kitendo cha kujigeuza nyoka.
Manung’uniko na malalamiko yalimkasirisha Musa hakumstahi MUNGU, akatoka kwenye urithi wa MUNGU.
Kitetemeshi na vitisho vilimtoa Eliya mtishibi kwenye urithi wake akakimbilia msituni mapangoni akawa ametoka kwenye urithi wa MUNGU.
Mafarisayo na masadukayo ,wayahudi walimkataa Yesu wakamtoa nje ya shamba wakamuua, wakachukua urithi wake Yesu akiwa msalabani alilia ee MUNGU mbona umeniacha MUNGU akamgeuzia kisogo kwa dhambi za dunia alizokuwa amebeba.
Hivyo Yesu nae akawa ametolewa kwenye urithi wake.
Wenye hila na mashetani walimtoa Eliya Ad2 kwenye urithi wake kupitia zile silaha alizokuwa ameachilia amelipa kanisa kuuza , kuuza vibebea nguvu, shukrani za kuwapiga maadui tukatumia kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Tukakosa moyo wa shukrani , hatukumjua kuwa alikuwa ni MUNGU ndani yake hatukumtambua wala hatukumuelewa tukamtenda kwa hila.
Hata wewe mwenye haki jifahamu leo ishi kwenye toba maana MUNGU amekuja mwenyewe.
Usikubali adui akutoe kwenye urithi wako kwa MUNGU, kuanzia leo mwenye haki hatatolewa kwenye nje na kuuliwa.
Sitatolewa kwenye mlima wa BWANA kwanza.
Kizazi hiki cha MUNGU hakitatolewa nje ya shamba, hakitatolewa kwenye urithi na kusudi la MUNGU, hakitauawa milele.
Leo tunatubu na kufuta kabisa kituo hicho.
Nitang’ang’ania mlima wa BWANA, sitatoka milele kwa damu ya MUNGU.
MUNGU hatatolewa mahali pake, hatafukuzwa, hatahukumiwa, hatashitakiwa, hataondoka kwetu milele.
Mwenye haki hatafukuzwa hataonewa nk milele.
WAKILI WA MUNGU
Namshukuru MUNGU kwa kuwa siku ya leo sina kesi inayosimama mbele yangu.
Hakuna kesi ya aina yeyote, hakuna kesi ya magonjwa, utasa, hasara, umasikini, ufukara zimefutwa na MUNGU mwenyewe.
Mashitaka yoyote yamefutwa kwa wenye haki.
Wakili amesema amethubutu kumuuliza MUNGU kwamba kwa nini umetuletea ujumbe huu ndani ya wiki hii wakati tayari ule umoja wa MUNGU Kristo na Kanisa umetimia?
Tangu siku ile ya kerubi kutupwa chini hakuwahi kupanda juu mpaka alipokuja kufanikiwa kumuibia Adamu ndipo alipanda tena kule juu lakini kwa nguvu ya Adamu.
Na hakuna aliyewahi kutubu au kufuta hicho kituo cha muovu kutumia nafsi ya mwenye haki, kerubi kutumia nafsi hai ya Adamu ambaye alikuwa ni mwenye haki.

Hivyo waovu walitengeneza agano la mwenye haki kutoonekana ni mwenye haki ndani ya uumbaji wote.
Kila mmoja na aseme MUNGU nisamehe kwa kuwa nilikuwa na nyoka ndani ya ufahamu.
Badala ya muovu kuonekana muovu mwenye haki ndiye alionekana ni muovu na muovu alionekana mwenye haki.
Kwa sababu Adam alivyoanguka ilikuwa ndio sababu vizazi vyote vilivyopita vilianguka hapo.
Hivyo badala ya muovu kuanguka mwenye haki ndiye aliyekuwa anaanguka.
Badala ya kerubi kuonekana ndiye muovu kanisa ndilo lililokuwa linaonekana baya likakataliwa kwa sababu kerubi ndiye aliyekuwa anatumia nafsi ya kanisa.
Muovu kutumia sura ya mwenye haki na kwenda kufanya uovu hivyo badala ya kuonekana yeye na sura yake alikuwa anaonekana mwenye haki.
Kutubu kwa ajili ya wale aliokuwa wamechukua nafasi ya MUNGU KRISTO NA KANISA, waliokuwa wanakaa mahali pa MUNGU.
Kutubu kwa ajili ya waliokuwa wanamhifadhi nyoka bila kujua , muovu kuchukua haki ya mwenye haki na kwenda kufanyia mambo mabaya.
Dunia ilichukua hak ya Nchi, ulimwengu ulichukua haki ya Mbingu maana ukisoma MWANZO 1:1.
Hakuna mahali tunaona MUNGU alipoumba dunia na ulimwengu bali MUNGU Aliyetuma wote aliumba Mbingu na Nchi .
Sema watu, wanadamu na waandishi ndio huwa wanalazimishaga kuwa MUNGU aliumba dunia na ulimwengu na wanajua kabisa kuwa MUNGU hakuwahi kuumba dunia na ulimwengu.
Leo ndio ujue kuwa haiwezekani muovu kuwa na haki pasipo kuiba haki ya mwenye haki.
Hivyo kwa kuwa mimi mwenye haki sikuwa na haki hivyo mimi kuhudumiwa na MUNGU ilikuwa inawezekana sana kwa sababu kila MUNGU anapokuja kunihudumia alikuwa anaona sura ya muovu kwangu.
Ukiona unaumwa ujue kuna ambaye amechukua uzima wako yaani ujue uzima wako uko mahali unatumiwa.
Ukiona wewe ni masikini ujue kuna aliyechukua utajiri wako kwa kuwa kila mmoja alizaliwa akiwa tajiri.
Hakuna aliyewahi kuzaliwa masikini ndio sababu mtoto ukimuwekea mkeka hakai anaenda kukaa kwenye kochi, ukimpa damu ya MUNGU kwenye kikombe cha plastiki hapokei hataki anataka umpe kwenye glasi.

Ukiona kichwa wako ana mwanamke mwingine nje ya wewe ambaye ni kanisa wake ujue nguvu ya agano nguvu ya wewe kuonekana ni kanisa imechukuliwa na mwingine.
Zinapopungua mfukoni mwako ujue kuna mahali zilipo unatakiwa ufanye toba ili kurejesha fedha zije kwako.
Kutubu kwa kituo cha kerubi kuhifadhi vitu vyote vizuri na sisi wenye haki tukahifadhi mambo mabaya.
Kerubi alihifadhi utajiri uzima kupendelewa na MUNGU, faida thamani nk na wenye haki tukahifadhi taarifa mbaya maneno maneno, umbeya usengenyaji, mauti, mafarakano, umasikini.
Aidha Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoia Sadaka maalumu ya  kutohifadhi tena mauti mafarakano nyoka hila ushetani na mambo mabaya yote ndani yangu.
Ni ya kuondoa kitendo cha nyoka kuhifadhi  sifa za MUNGU, utajiri halisi, dhahabu n?
WARUMI 8:29 MUNGU alinijua tangu mwanzo, waliokuwa wamesimama mbele yangu wameondolewa.
Waliokuwa wamechukua haki yako kwa sadaka hii haki yako imerejea.
Sasa ni wakati wa kila mmoja kutafuta kanisa mahali lilipo kila mmoja atasema nipeleke kanisani maana kanisa sasa linajulikana.
Aliyekuwa anakuzuia kuja kanisani atakuruhusu, atakuachilia umtumikie MUNGU kwa uzuri na utakatifu.
“Ule mwanzo wa uharibifu haupo tena! Maigizo yameishia hapa. Kusikia kushika na kutenda neno”  alisisistiza.
Kuh Majira ya 7                                   *KUISHI JUU YA UMBO*
YOHANA 1:11 alikuja lakini waliowake hawakumtambua, hawakumpokea.
Hivyo umbo la uharibifu lilitokea kwa sababu ya kutompokea kristo wakati wa kizazi cha 3.
Kuna umo la wenye haki kutomtambua na kutompokea mwenye haki tena kutomfahamu mwenye haki.
Waovu ndio walimfahamu kristo kizazi cha 3 kabla ya wenye haki hivyo ndio sababu yesu hakupokelewa kabla hata kuzaliwa mpaka amezaliwa amekua, MUNGU akampaka mafuta bado walimkataa.
Kizazi cha 4 walimkataa Eliya wenye hila na mashetani nk. Ili uharibifu usitokee unatakiwa ukimuona WAKILI ujue umemuona MUNGU.
Ndipo hayo mema yatakapokujia na utakula mema ya Nchi.
Changamka maana moyo wenye changamko ndio dawa nzuri.
ZABURI 33:12 Taifa ni heri,  wenye haki aliowachagua kuwa urithi wake, ili uwe heri ilikuwa ni mpaka ; uishi kwa Neno, kumjua MUNGU, kuijua kweli, kumjua unayefuatana naye, Taifa ni heri na Kanisa ni heri.
Jambo la kufahamu ili kuishi juu ya umbo. Kila kinachoishi juu ya nchi kinachoonekana na kisichoonekana kina umbo.
Hata furaha ulionayo ina umbo,kila umbo la chochote kinabeba uhalisi wa kitu husika.
Kuna tabia ya umbo, tabia ya mzuri  na tabia mbaya.
Katika majira zote6 hawakuwahi kufundishwa ila sisi tumefundishwa kwa sababu yeye mwenyewe ndio yupo amekuja mwenyewe,
hivyo tambua kuwa una Neema kubwa kwa sababu katika hizo majira zote 6 wenye haki walikuwepo lakini haakufundishwa hili.
1PETRO 1:10  Leo ujue juu ya UMBO ni mahali MUNGU anapoishi ndio sababu yeye hakwaziki, hazimii moyo, hahukumu kwa maneno aliyoambiwa aliyosikia kwa yeyote.
MUNGU alikaa hapo tangu mwanzo ndio sababu hata alipoona kerubi ametengeneza siku saba zake pale giza ukiwa na utupu;
Hakupata shida hakuenda kumuuliza kwamba ulifanya nini pale hakuenda kumsuta hakusema utanitambua kwa unaniharibia utaratibu wangu.
Tunaona MUNGU akiendelea na uumbaji wake, hakubabaika aliendelea na majukumu yake pamoja na misukosuko mingi aliyokutana nayo hatuoni mahali anajuta anakata tamaa.
Juu ya umbo ni mahali pa faragha YOHANA 17:1- nasi ametuingia hapo.
Hivyo kizazi cha 3 waliona kushuka kwa sababu ilikuwa sio majira yake ila wewe kizazi cha MUNGU hutashuka chini.
Kituo cha kuishi juu ya tulipofika hata sura ya WAKILI ilibadilika, leo ujue ukiishi juu ya umbo kila kitu chako kinabadilika.

Ishi maisha ya kutoangalia mwingine, wewe DILI na sauti ya MUNGU ndani ya Wakili wake.
Juu ya umbo ndio kuna utajiri udhihirisho mafanikio yako yote yako hapo.
*MAMBO YALIYOSABABISHA UISHI KWENYE UMBO*
Kuangalia mazingira yanayokuzunguka naunayoyaona. MWANZO 18:10-15.
Kuishi juu ya umbo la elimu uliyosoma zamani LUKA 5:3-9 +  2KOR 10:5  ISAYA 40:28-31.
Maisha uliyoishi zamani na kuishi jana  ISAYA 43:18-19
MCHUNGAJI mmoja amekuja hivyo usisubiri alete adha ndipo ujue kuwa kaja ishi juu ya UMBO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni