MUNGU ANAMTOA KANISA ILI AONEKANE INAVYOMPASA KUWA
FALME 17:1 Wakili amesema hatukuwa na kosa ila alichofanya mzee wa toba ni unyenyekevu wa moyo.
SADAKA maalumu ya kumpokea baba. Kurejea kwa nguvu kubwa ya ubaba, utendaji wa ubaba, kujulikana kwa baba katika mataifa yote ndani ya uumbaji wote,
Mamlaka, sauti, uhalisi, utisho wa ubaba, hatma na ukamilifu wa ubaba, majira ya ubaba, nk.
Hivyo leo kila mwenye haki anaondoka na kapu la utajiri. Madhabahu ya utajiri kwa upya.
Leo tunatubu kwa ajili ya roho aliyekuwa duniani AYUBU 42:10 MUNGU aligeuza uteka wake,
Kulikuwa na shida nyingi za fedha kutokana na uteka wake uliokuwa umetokana na ukame wa muda mrefu.
Kushukuru MUNGU kwa kuwa kugeuza uteka wetu. Waliokutesa waliokudhihaki MUNGU amegeuza uteka.
Kila anayetenda kwa haki hatachanganyikiwa milele, hataonewa tena.
Leo tuombee adui zetu ili MUNGU ageuze uteka wako.
1YOHANA 5:9 Kanisa lilivikwa mavazi mabaya mpaka likawa linaonekana baya.
Ni wakati wa kusafisha kanisa kuondoa matusi.
Kizazi cha 1-4 kanisa lilionekana baya lakini kizazi hiki cha MUNGU kanisa lazima lijulikane kwa sababu yeye mwenye shamba kaja.
Ni wakati wa kutubu kwa ajili ya matusi ambayo MUNGU anatukanwa.
Na Kanisa alivyowahi kutukanwa kwa sababu kwa kutukanwa kwa mwenye haki unyonge uliingia ndani yetu na tukaona labda hapa si kanisa,
Tukaona kama hakuna MUNGU na pia tukafika hatua ya kuuza Baraka, hivyo ni wakati wa kumtakasa kanisa ili aone kuwa sasa ana BABA.
Sasa sura mpya ya kanisa inaonekana kwa uhalisi.
Kao la dunia lilikuwa ndani ya kanisa, kizazi cha 1-3 kanisa halikueleweka, kizazi cha 4 kanisa lilipotokea walianza kusema ni freemason nk.
Kizazi hiki amekuja mwenyewe hivyo lazima waone sura halisi ya kanisa ndani yangu mimi mwenye haki.
Huko wajibu wa moto, mlima wa moto, biashara zako, ofisini kwako wamjue MUNGU, KRISTO, KANISA kupitia wewe ili kao la dunia liondoke ndani yako, kanisa.
Aidha sura ya kanisa ilikuwa haikuwahi kujulikana wala kueleweka. Kanisa lilionekana la wenye vilaka lililochoka nk.
Leo tunataka sura halisi ya kanisa ionekane kila mahali, kutubu kwa kutojulikana kwa sura ya kanisa.
Kao la dunia kwa maana ya kuwa na lugha ya dunia , muonekano wa dunia, utendaji na kanuni za dunia, nk tuliondoe ndani yetu kataa kabisa ili kao la MUNGU likae na kuonekana ndani yako.
Mawazo mabaya akili mbaya mafarakano hayataonekana tena ndani ya kanisa.
2KOR 12:2-7 leo tunawaondoa wajumbe wa shetani ndani yetu.
Ambao ni magonjwa utasa kupungukiwa nk, tunafuta kituo cha mjumbe wa shetani kukaa ndani ya kanisa tunafuta.
Ambao ni magonjwa utasa kupungukiwa nk, tunafuta kituo cha mjumbe wa shetani kukaa ndani ya kanisa tunafuta.
Kuna kuhani alikuja kwangu akakuta tunashiriki kwa mkono ….
Akafananisha na Parestina sasa hii ya Kanisa kufanya vitu vizuri na kufananishwa na sehemu nyingine hii hatuitaki tunataka kila atuonae aone kanisa.
Mahali popote ulipo lugha yako iwe ya kanisa ijulikane, sura ya kanisa ni kuanzisha viwanda bila mkopo,
Ni kulima shamba na mazao yakaota na kusatawi shambani mwako lakini jirani yako hayajaota kabisa.
ISAYA 60: lugha yako ibadilike kwa kuwa wewe ni kimbilio kila uendapo ukiwa mlima wa moto na wakikufuata wakisema wana shida usiseme hata mimi ninashida.
SADAKA maalumu ya kumuondoa mjumbe shetani ndani ya kanisa, sasa amekuja na ijulikane kuwa tunaishije tunakulaje.
Yosh 20:5 kanisa ni mji wa makimbilio kwa uhalisi, usizungumze matatizo zungumza shuhuda ndio chakula cha MUNGU.
2FALME 3:11-15 mvua kunyeesha, 2FALME 2:19-22 sura ya kanisa ni hii kuondoa mapooza.
2FALME 6:1-6 shoka lilipoanguka kwenye maji … umbo la physics likafutwa.
2FALME 7:1 karamu itauzwa sawa na bure. Kisichowezekana kwa mtu kwa MUNGU yote yanawezekana na tumeungana na huyu MUNGU.
Shida yetu tunaomba na kufuta wenyewe kutokana na yale unayonena ukishatoka kwenye shukrani hatuamini hata tunachoomba leo mwisho.
Tokea kwenye umbo la mila na desturi ya kwamba anayeoa avae hivi au nyumba ya aina Fulani.
Mith 31:10 Inatakiwa Kanisa MUNGU atuamini na kuna namna MUNGU anashika handbreak kwa sababu anaona kama tutauza.
Kama atafanya vyema basi kichwa hatakosa kumtendea mema.
Kuamka saa 8-9 sio utumwa bali kwa kanisa ni sahihi. Usikubali kabisa kichwa wako aaibike.
MUNGU hawezi kukusaidia kama unamuwasha kichwa wako.
Na walio na hekima watang’aa kama jua, fungua kinywa chako kwa hekima.
Mwenye kusababisha MUNGU kujulikana, kichwa kujulikana ni Kanisa.
HESABU 30:1- usiulize mbona hupendezi kanisa wangu, unatakiwa usababishe apendeze.
Kama kanisa hajui kupiga pasi mfundishe kama hajui kupika mfundishe nk
Usilaumu mfundishe, usimwambie kanisa wako kuwa nataka upendeze kama mke wa Fulani.
Tabia inayoonekana kwa kanisa wako ndio ipo kwako wewe kichwa.
Kwa unayempenda lazima akutii kanisa asipokutii ujue wewe kichwa humpendi.
1KOR 13:1- upendo hauangalii mazingira, hivyo kilazimisha akutii wakati wewe mwenyewe haumpendi ndipo na makofi yanapoanziaga.
Mimi nikiona kichwa anayelalamika kuwa kanisa wake anapiga sana simu kwao anaongea muda wote mimi huwa najua kabisa shida ipo kwa kichwa wake;
Mwenyewe ina maana hajaona ndugu rafiki kuhani kichwa ndani yako kichwa. EFESO 5:22-25 kwa habari ya kichwa na kanisa.
Hekima isipungue ndani DANIEL 12:3 wenye hekima watang’aa kama jua.
EFESO 5:25-27 kanisa apendeze asiwe na madoadoa mawaa awe na kicheko wakati wote.
BABA wa uumbaji wote ametupatia tulio wake *SHERIA YA WEMA* ambayo makanisa hufumbua kinywa kwa hekima kwani Sheria ya wema I katika ulimi wake ili vinywa vyetu vinene yaliyo mema na yenye hekima ili ajulikane kote Mith31:26.
Hatahivyo Wakili wa MUNGU amesimamisha *SHERIA YA WEMA* kwenye vinywa vya makanisa ili vinene yaliyo mema na yenye hekima.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo kabla ya Wakili wa MUNGU kufika Mzee wa Toba na kiongozi wa Makuhani alisema;
Alianza na shukrani za kuinua taifa na viongozi wote watendao kwa haki nk 1TIMOTH 2:2-4.
Toba kwa machukizo yote ili MUNGU atembee nami na aishi kwangu.
Kutomfahamu baba mmoja wa rohoni, kutubu kwa kipindi ambacho kanisa lilibaki kama yatima na ile nguvu ya ubaba ikachukuliwa na dini na dhehebu;
Kukawa na mababa wengi, baba wa ubatizo kipaimara ndoa nk leo hiyo imefutwa.
Mtoto asiyemjua BABA ana tabia mbaya na ukimkataa BABA umemkataa MUNGU.
Sifa za kumfahamu na BABA zinazosababisha umpende na BABA akupende;
Kataa mababa wengine wote.
Ukubaliane nae kwa jinsi alivyo.
Usitake baba yako aaibike.
Chochote kinyume na baba yako unatakiwa uingilie kati kwa toba.
Kusema kweli tu!
Kataa mababa wengine wote.
Ukubaliane nae kwa jinsi alivyo.
Usitake baba yako aaibike.
Chochote kinyume na baba yako unatakiwa uingilie kati kwa toba.
Kusema kweli tu!
Alisema Wakili wa MUNGU hatuonyi tunayoyafanya kwa sababu hatujamtambua hivyo wengi tukionywa tunakwazika.
1SAMWEL 8:1-8 , siku ya 4 ile Math 21:41 ilitimia kwa uhalisia baba mwenyewe yupo.
DAN 2:44 utawala wa amani umesimama kwa kuwa ufalme wa mabaya na mabaya na watendao hayo mabaya wamefutwa milele.
Mahali pa kabla ya wazo la kumuumba kerubi ni mahali pa mwanzo malidadi, faraghani.
Ni mahali pasipo na mwanamke, joka, falme na mamlaka, pepo wachafu , magonjwa, umbo la mtu na mwanadamu, hekima ya dunia,
Ni pale ambapo alisema pakiwepo lugha kinyume na MUNGU zitakoma na zimekoma.
Ni mwanzo wa kutoonewa, kutopigwa, na kutopatwa na mabaya yote.
YEREMIA 50:20 Utaitafuta dhambi hutaiona ni mwanzo wa njia moja ISAYA 35:8-10 isiyo na kuishiwa kupungukiwa kukanyagwa nk.
Tunae baba mtakatifu Wakili wa MUNGU. EBRANIA 6:12 msiwe wavivu muwe wafuasi kwa imani na uvumilivu.
Uone mema tu! Uone kusudi la MUNGU kwa kila mmoja.
Vitabu vingi vimeandikwa ili kuonyesha njia ambayo kanisa tumeipitia.
Wewe kama ni kiongozi utupe njia ya kanisa hata Musa alikuwa na njia aliyowapitisha Israeli ya mwilini.
1SAMWEL 11:1- ni marufuku kwenda kwa waliopigiwa kura.
Ni hatari sana kumkataa aliyepakwa mafuta na MUNGU.
HESABU 2O:14 Usije ukang’olewa macho na majira hii watang’oa na ulimi, utumbo nk.
Ukiongozwa na wenye moyo mbaya huwezi kuvuka hata siku moja.
Kwa nini baba hapikelewi? Ni kwa sababu hakuna aliyewahi kusema baba atakuja walikuwa wanasema Yesu atarudi.
Aidha Mzee wa toba na Kiongozi wa Makuhani amefanya toba maalumu kwa kanisa Kataa mababa wengine wote,
Mengine ni kutokubaliana nae kwa jinsi alivyo, kutaka BABA aaibike, kutoingilia kati kwa toba kilichofanywa kinyume na BABA na kutosema Kweli.
Lakini pia Mzee wa Toba ameongoza wenye haki leo kutoa Sadaka maalumu ya Kumpokea BABA na kuagiza Makuhani wote kusimamia ukusanyaji wa Sadaka Maalumu hiyo ili wenye haki wote tuweze kumpokea BABA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni