Jumapili, 5 Februari 2017

      KANISA LA SILOAMU NI NAFSI YA TATU YA MUNGU


Kabla ya BABA kufika Mtendaji wa Wakili wa MUNGU aliongoza shukrani za kuombea taifa; Yer 29:7 kuombea mji ili uwe na amani.
1tim 2:1-4 Kuwaombea wote walioko madarakani. Tena wanafanya jambo zuri kumuweka MUNGU mbele.
EFESO 3:10 Hekima ya MUNGU iliyo ya namna nyingi kujulikana na watu wote.
War 13:1- kila mtu na atii mamlaka kwa kuwa kila mamlaka yatoka kwa MUNGU. Mamlaka iliyopo yatoka kwa MUNGU.
Na kila ashindanae na mwenye mamlaka ashindana na MUNGU na amuasi MUNGU.
BABA
Leo ni mwisho wa yeyote kushindana na Kanisa.

      *TANGAZO!*
*NI MWISHO WA MUOVU KUSHINDANA NA MWENYE HAKI, MUNGU KRISTO KANISA WAKILI TAIFA NA KIZAZI CHA MUNGU.*
Tangazo hili liende mpaka kuzimu ujinini kwa wachawi waganga walozi washirikina wanajimu waovu waasi watenda dhambi walioushitaki;
Waliokutukana waliokudhihaki waliokudhulumu waliokuonea wanaokunyanyasa kwamba hakuna wa kushindana na mwenye haki milele.
Los angels wamesikia the head wamesikia Tokyo wamesikia waliojificha kwenye Pluto wamesikia kwamba hakuna wa kushindana na mwenye haki milele.
Musa aliwaambia Israeli ya mwilini nyamazeni kimya muuone wokovu wa BWANA, je waovu washitaki wao waliuawa hawakuuawa?? Waliuawa.
Muovu yeyote hatavuka milele, njia ya mwenye haki muovu hapiti, haruhusiwi kupita,
Wote wanaoshindana nawe mwenye haki wanashindana na MUNGU,
Tangazo hili ni kwa wenye haki pekee unaweza ukawa hapa lakini si mwenye haki basi ujue tangazo hili halikuhusu kabisa.
Mdo 13:6 Kiapo: Kila anayeshindana na mwenye haki kuanzia sasa na awe kipofu!

Awe pepo mkuu wa anga mchawi mlozi afe sasa hivi.
Je unaamini imekuwa hiyo? Naamini imekuwa!  Aliyesababisha uwe tasa uachike utaabike ufukuzwe kazi wote hao hawapo milele.
MUNGU nashukuru kwa sababu asubuhi asubuhi umenitokezea na zawadi na haya yote MUNGU naamini napokea imekwisha tokea.
Mdo 4:24 kumuinua MUNGU kwa sauti moja, ni mwisho wa anayeshindana na mwenye haki.
Namshukuru MUNGU kwa kuwa jana MUNGU amenivika vazi la ubaba.
Ubaba ni nguvu inayopenya kila mahali, hata mtoto anapoanza kusema huanza na neno baba, sasa namshukuru MUNGU kusanyiko limepata baba.
MUNGU amegonga muhuri 7 kuwa Wakili ni BABA, usiyempenda kaja, tuache mazoea na kawaida yanayosababisha tusipate udhihirisho.
Leo tutubu ili viongozi waje Madhabahuni mchana tunawatoa mahali walipokuwa wamefungiwa na Nikodem kuwa viongozi waje usiku tu Yoh 3:1-
Maana ilitakiwa sasa hivi Wakili wa MUNGU awe bungeni akiliambia taifa lisiwe na wasi wasi limechaguliwa na MUNGU kuwa urithi wake.
Tatizo hata mabosi wetu hatuwaambii habari za MUNGU tuliyenae hii sio nzuri tubadilike.
2FALME 5:20-26  tusiwe kama Geazi aliye mfuata Naamani aliyekuwa ameenda kwa Elisha kwa ajili kupata uponyaji, wala ELISHA hakutaka chochote kutoka kwake;
Huyo mfalme hivyo alipoondoka tu Geazi alimfuata akataka fedha kwake.
Tusifanye hivyo ili viongozi waje kwa MUNGU wa kweli.
2FALME 3:11 viongozi wote tunawaunganisha na Mfalme Yehoshafati kwamba watafute hekima watafute ushauri kwa aliyembeba MUNGU na KRISTO wake.
Mahali walipokuwa wamezika nafsi ya Kanisa na taifa leo ni mwisho, walipokuwa wamezika Baraka zako, sura yako, afya yako, mtaji wako leo vimefufuka.
Nafsi yangu naipa nguvu itoke huko sasa hivi kwa damu ya MUNGU.
*LEO WENGI TUTAPATA PROMOTION YA AJABU.*
Aidha Sadaka Maalumu ya leo WALAWI 16:17 ya kufufua kila kitu cha mwenye haki kilichokuwa kimezikwa.
Kila aliyewahi kuleta hasara ndani ya Kanisa, matatizo shida anayekula sadaka hiyo anakula shida zote za wenye haki.
Hakuna shida itakayobaki kwa sadaka hii ya leo.
Shida ya nafsi yangu leo ni mwisho. Mwanzo wa uharibifu haupo tena.
Akifafanua kuhusu Kanisa la Siloamu ni Nafsi ya tatu ya MUNGU Wakili wa MUNGU alisema Kuna maswali matatu yanahitaji majibu:-

Kanisa ni nini ??
Siloamu ni nini??
Nafsi ya 3 ya MUNGU ni nini??
Kanisa ni kusanyiko ambalo halishindwi na malango ya kuzimu MATHAYO 16:18  Yesu alisema…..
Hata ukiona wana jengo zuri, mchungaji mzuri, askofu mzuri, lakini kama wanashindwa na malango ya kuzimu hilo sio kanisa.
Kigezo cha kupima sio maneno matamu matamu na lugha bali ni linaloshindwa na malango ya kuzimu.
Efeso 3:10  Kutia adabu, Kanisa ni Kusanyiko lenye hekima iliyo ya namna nyingi ya kuangamiza falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho chafu, pepo wabaya, wakuu wa giza.
Ufu 11:6  kanisa ni kusanyiko lenye hekima ya kubadili maji kuwa damu ya chochote ili kuangamiza kutia adabu waovu wote.
Ukiona wanaochukia kanisa ujue ni kwa sababu kanisa lina hekima yenye kuwaua maadui wote.
Kuhama kituo, 1FALME 2:1-14  ukiona yeyote hataki kuhama vituo ujue hao ni dini.
Kutembea na wingu la moto wingu la MUNGU, kutoka 13:21-22 BWANA akawatangulia mbele yao Kanisa ni kusanyiko ambalo MUNGU anaonekana wakati wowote.
Anaongea anasema kila siku anatupatia vitu vipya.
MUNGU huwa anatabia ya kuwaleta adui zako karibu ili apate kuwaangamiza Kut 14:
2kor 12:2-  kanisa ni kusanyiko linaloanzia  au la wanaoishi juu ya mbingu ya 3 mahali kerubi hawafikii.
Mahali penye ufunuo uliomuua asi 2thes 2:8.
Ukiona mahali wanapopiga kura ujue hapo sio kanisa ESTA 3:7,
Ukiona kusanyiko linaloishi kwenye majira na nyakati za dunia za januari mpaka desemba ujue hiyo sio kanisa.
Hata kama unasema Bwana asifiwe wewe ni mkatoliki tu!   Yoh 4:23-24   na ile saa aliyoisema Bwana Yesu haikuhusu kubisa.

Kanisa lina majira na nyakati za mwaka wenye miezi 12, mwezi ukiwa na siku 28, wiki ina siku 7, abibu mpaka adari.
SILOAMU ni nini ? Yoh 9:7 mwilini Siloamu ni bwawa lililopo kule mashariki ya kati, 
Rohoni Siloamu ni bwawa lililopo hapa, maana yake Aliyetumwa na baada ya MUNGU kuja mwenyewe sasa inaitwa sioamu ya ALIYETUMA WOTE.
Katika vizazi vilivyopita wewe ulinawishwa na waliotumwa majira hii unanawishwa na ALIYETUMA WOTE.
Nafsi ya 3 ya MUNGU ni nini? 1 Yoh 5:8  MUNGU ana nafsi 3 ikiwa na maana nafsi ya roho ndio kanisa.
Roho ilikuwa duniani 1YOHANA 5:9 kazi yake ilikuwa ni kwenye uumbaji wote.
Uumbaji wa MUNGU ulianzia ZABURI 98:1  kitu cha kwanza MUNGU aliona sifa,
Akaamuru nyota jua nyota ambao walikuwa ndani fake watoke wakicheza cheza ndipo mavumbi yalipoonekana akatokea mwanamke ufunuo 12:1-3 badala ya kanisa.
Kwa hiyo tunaona kuwa kumbe uumbaji haukuanzia Mwa 1:1 , wala Ezek 28:15.
Yosh 6:26 kila alichokuwa anatamka kilimtengeneza mungu m ndogo.
Mlima wa MUNGU ni hapa bustani ya Edeni ni hapa wale wote wenye maneno mabaya kwenye mitandao waache MUNGU majira hii haachi wanaomtukana,
Akaongeza kusema kuwa  kanisa ndilo linalomkamilisha MUNGU.
Kanisa  la Siloamu ndio limeleta Mwanzo Malidadi, limetoa ufalme wa MUNGU Israeli limeleta hapa Gosheni.
Wakili amesema tuseme kweli DANIEL 2:44 kama husemi kweli ina maana wewe hutaki utawala wa amani,
DANIELI 2:35 hutaki kanisa lijulikane kuwa ndio jiwe walilolikataa waasi limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Hamtaki waje kuhiji hapa? Tunataka. Semeni kweli basi.
MUNGU yuko hapa na ndio ameshakuja hivyo hatoki na miguu kaweka hapa hapa na kiti chake kipo hapa na hatoki milele. 
Sauti kuu 2 zilizobadilisha majira na nyakati zimetokea hapa kwa nini hamtaki kusema kweli? 
Upo tayari kujivunia taifa lako na kanisa lako, upo tayari kuwaambia twendeni kwa ALIYETUMA WOTE!! 
Katika ibada ya pili;
WAKILI wa MUNGU amesema; wenye haki tunaondoka tukiwa tumevikwa Vazi La Ushindi,
Maana nina BABA imefika wakati wa kukunja shati na kusema sasa njooni Yosh 1:5 kwa uhalisi hakuna asimamae mbele yangu.
Mahali popote ulipowahi kutukanwa, tusi hutaliskia tena milele.
Hata wadudu wote wazungu waamerika wamejua kuwa mimi mwenye haki situkanwi tena.
Ni tangazo lililosimama ndani ya uumbaji wote 1Yoh 3:14 sisi tunajua ya kwamba tumetoka mautini tumeingia uzimani.
Hakuna wa kunitoa hapo hakuna wa kunishitaki kunihukumu hapo milele.
Kila kinachoitwa kwa jia langu kimetoka mautini kimeingia uzimani. Nafsi yangu haitafungwa fungwa milele.
BABA tunae tuseme kweli ili kila tunapopita wajue kuwa hawatuonei tena!!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni