MOYO NI NINI?
WAKILI wa MUNGU kabla ya kufundisha NENO la leo alikuja na; -
Zawadi ambayo jana alituahidi. Akasema anafuraha mno, na furaha yake ya kwanza ni kwa sababu kwa mara ya kwanza ameona gari lililoandikwa “waliookoka wana raha”.
Kwa sababu hiyo sitakiwi kuona mateso, magonjwa, hasara, giza ukiwa utupu, nk kwa sababu umetoka ukoo Fulani.
Mshale wowote uliowahi kukutana nao kwa sababu ya asili mahali ulikotokea, ile nguvu ya umbo ya kukuingizia majuto, kujihukumu, matatizo, shida.
Hata kama umepigwa na kukanyagwa sana leo sahau kabisa, ulivyotukanwa, ulivyobezwa, leo samehe na usahau kabisa.
Furaha ya pili Ezekiel 28:18 Alipoinua moyo wake automatically moto ulitokeza ndani yake mpaka akawa majivu.
Hivyo leo chochote kilichoinuka kinyume na mimi leo au majira yoyote moto umetokeza ndani yake na umemteketeza kila aliyenidhulumu, aliyenisema mabaya.
Waliokuwa wanatesa agano lako, biashara zako, familia, kazi yako leo moto umetokeza ndani yao. Kwa Yule kahaba aliyechukua kichwa wako, chuma ulete kwenye biashara zako moto umetokeza ndani yake na umeteketeza.
Aliyenifanyia hila, aliyekuwa anazuia kiwanda changu, mashamba yangu, leo moto umetokeza ndani yake na amekuwa majivu, najisi, kitu kisichofaa.
Na wale wanaoenda kwa mganga kutafuta msaada na mganga mwenyewe moto umetokeza.
Wanaoenda kuzimu kujificha moto umetokeza ndani yao.
Waliokuwa wanaisema SILOAMU vibaya leo moto umetokeza ndani yao.
Wale waliokuwa wanawatesa wenye haki, waliochukua vitu vyako leo moto umetokeza kwao.
NENO hili kama halikutokea kwa kerubi haitatokea kwako lakini kama ilitokea kwa kerubi sawa na MUNGU alivyosema basi hata kwangu leo lazima itokee.
Vikao walivyokuwa wanafanya vya kuangamiza kanisa leo moto umetokeza kwao.
Ulikuja kwa nauli ya kukopa leo kwa ibada hii ukitoka hapa lazima upokee simu ya kwamba kila kitu kimetiki.
MUNGU amelifuta umbo la zamani hivyo sitakumbuka mambo ya kale ya zamani milele, ramani kundi la waovu michoro yote waliokuchorea ya kuangamizwa , kukupiga wewe mwenye haki leo moto umetokeza kwao.
Isaya 43:18
LEO lazima utoke na jambo jipya . KIAPO; LEO UNAONDOKA HAPA NA JAMBO JIPYA.
Tena ukiwa ni amwingine kabisa, mpaka sura yangu itabadilika, nitaonekana kwa kila anionae ataona mwanga mionzi ya utukufu.
Yule malaika anayefuta mateso yote kwa wenye haki yuko hapa, Jeshi linalofuta kumbukumbu mbaya zote liko hapa.
WAKILI WA MUNGU; ametaka baada ya ibada hii, baada ya kusoma ibada hii, baada ya kusikiliza ibada hii kila mmoja amuone amekuwa na muonekano sura kama ya mtoto.
ILI KUTOKA KABISA KWENYE UMBO LA MTU NA MWANADAMU; kwenye mateso yote tumetoka, kwenye kumbukumbu mbaya zote tumetoka.
Leo sahau kabisa kwa wewe ambaye unajiona umetoka kwenye familia ya umasikini, leo nataka uone ya kuwa wewe ni mtoto wa mfalme.
Kujiona umetoka mabonde kwinama;
Kuanzia leo wewe mwenye haki lugha yako ibadilike, muonekano wako ubadilike, aliyewahi kuzaliwa katika shida na akaitwa shida leo asahau shida zote.
Sahau ili yote ambayo MUNGU ameyaandaa kwa ajili yako leo upokee. Maana pasipo kusamehe na kusahau huwezi kupokea.
Kama bado nakumbuka ya zamani leo nisahau ili nivuke na nivushe familia, kijiji ulichotoka.
Leo tunafuta kabisa umbo la mahali ulipozaliwa, hata kama ulizaliwa na chifu ujue leo MUNGU ndio chifu, ama na mfalme jua leo MUNGU ndiye mfalme.
Na leo MUNGU amenitoa kuwa wa mwisho na sasa leo mimi ni wa kwanza ambaye napewa fimbo ya chuma.
Kuna wanaokumbuka mpaka leo yaliyotokea kule shule alikosomea jinsi mwalimu alivyompiga kwa kosa la kuonewa, anakumbuka rafiki yake alivyomuibia akili yake nae akafelishwa.
Daniel 1:3-8 ulikuwa ni kijana mzuri tu ghafla unakutana na wakaldayo ambao walikufundisha tabia mbaya unakunywa pombe, unavuta sigara bangi, kuzini, kuiba, kuwa na hofu mashaka wasiwasi leo samehe na usahau.
Yote uliyowahi kukutana nayo ukiwa shuleni leo usahau.
Leo MUNGU ananipa moyo mwingine moyo mpya moyo mmoja kabisa nachotakiwa ni kuondoa kumbukumbu mbaya zote.
Danieli anasema hata jitia unajisi kwa chakula cha mfalme, hata wewe muapie MUNGU weka agano nae kwamba hutajitia unajisi kwa chochote kinachotaka kukutoa kwa ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.
Kama Daniel alishinda na mimi leo nimeshinda. Usiseme haiwezekani inawezekana vizuri.
Kuna waliowahi kunajisiwa na ndugu yake kabisa, ni kaka baba yake aliwahi kumbaka leo samehe na uachilie na usahau kabisa maana ni wakati wa kuwa matajiri tena kwa uhalisi.
Ujue rohoni kuna mapepo mengi yanayozuia wewe mafanikio yako.
LEO NAPOKEA BRAND NEW HEART
Kuna walioonewa kazini wakafukuzwa, wakafungwa, wakahukumiwa, wakatuhumiwa nk samehe na usahau, uone MUNGU atakavyokufanyia promotion MWANZO 39:1- yusufu alionewa lakini MUNGU alimuinua kwa majira husika ilipofika na hakuyaweka moyoni.
Yusufu hakushitaki hata kwa baba yake jinsi ndugu zake walivyokuwa wanamfanyia kwa sababu alijitambua kwa ile kanzu ambayo baba yake alimshonea alijua kuwa yeye ni wa tofauti.
Leo MUNGU amekushonea vazi jeupe vazi la utakatifu vazi la uaminifu na uadilifu lenye kukutofautisha na kutangaza ndani ya uumbaji wote ya kuwa umetoka kwenye dhiki kuu.
Yusufu aliijua hatma yake na wewe mwenye haki leo tambua kuwa hatma yangu haikuwahi kuguswa na yeyote ila tu MUNGU anataka nisamehe na nisahau ili itokee.
Kuna wanaokanyagwakanyagwa kwa sababu kuzuia rushwa, hata kama ndugu zako ukoo wako ndiyo wamekunenea maneno mabaya ya kukulaani leo nataka usamehe na usahau.
Maana kuanzia sasa watakutafuta watakuja huku wamepiga magoti maana watajua kabisa kuwa kweli ni ipi maana kweli imepata mahali pa kukaa hivyo watajua kuwa huna kosa.
Naona kama mnashangaa sana hamuamini kama iatokea??? Je Yusufu hakufuatwa gerezani??
Kuna aliyedhulumiwa mshahara wake leo unarejea.
Kila aliyewahi kuchukua marupurupu yako leo amerejesha.
IT IS PAY BACK TIME
Kuna walioteswa kwenye agano huko walikoolewa mpaka wanajuta wanaona kama walikosea jinsi mawifi wanavyomtesa, mama mkwe nk leo samehe na sahau.
MUNGU amewakumbuka leo unachotakiwa kufanya mama sahau yote, baba sahau yote. WAAMUZI 14: Samsoni na delila.
Kuna mabinti wamechumbiwa, kuna vichwa wamechumbia halafu wakaachwa bila sababu tena hawukuambiwa taarifa yoyote.
Binti kijana tambua leo MUNGU amekuandalia bonge la kichwa /kanisa kwa ajili yako, leo wewe samehe na sahau.
Kuna walioibiwa na kudhulumiwa fedha zao, nyumba zao, mashamba yao, viwanda vyao nk 1FALME 21:1- Wenye haki walipata shida mno majira hii MUNGU hakubali milele.
Leo usamehe na usahau maana kuna mkong’oto unaoendelea huko lazima watakuja huku wanakimbizana kukutafuta ili wakulipe haki yako.
Kujipigania wewe mwenyewe haiwezekani unatakiwa umuachie MUNGU ALIYETUMA WOTE kwa wewe kusamehe na kusahau ili MUNGU atende mwenyewe apendavyo kumtenda muovu LUKA 19:27.
Kuna walioonewa kwenye dini, dhehebu na wengine wameonewa humuhumu ndani SILOAMU leo nataka uwasamehe na usahau.
Maana kwa yaliyotokea mpaka wengine wanaota mpaka kwenye ndoto.
samehe Sahau ili uone MUNGU anavyofanya maana zile kamba zilizokuwa zimemfunga zinafunguka sasa hivi.
Wote niliokuwa nimewarundika kwenye akili ya kushoto na kulia, wakanielemea mpaka kuimba nikawa naimba flati kwa kuwa akili ya kushoto imebeba sauti nzuri, ufahamu mzuri akiba njema, akili ya kulia imebeba mahesabu makali.
Sasa ili nijue kweli umesamehe na kuachilia na umesahau ntaona tu jinsi unavyoimba, producer ukipiga gitaa hiyo ndio nitajua kama umesamehe na kusahau. Ukikuta mahali wanaimba vibaya, flati ujue kuwa akili ya kushoto imeelemewa.
Akili ya kushoto ikielemewa oooh!!! Utasikia flat tu!
Kuna waliomlaumu MUNGU AYUBU32:1- Usimpe orodha MUNGU ya vitu ulivyofanya kwa madhumuni ya kuhesabiwa haki.
Usimwambie MUNGU ujue mimi ndiye natoa sana hapa madhabahuni, nilimsaidia na kuhani … kulipa kodi ya nyumba ujue bila mimi angefukuzwa.
Leo tambua ukitoa sadaka ikakubaliwa umshukuru mno MUNGU, kuhesabu uliowahi kuwasaidia ni sawa na kujihesabia haki machoni pako mwenyewe.
1SAMWEL 15:20- MUNGU ALIYETUMA WOTE anapenda utii kuliko……… anachokuambia ufanye amesema sahau samehe ili awaangamize leo adui zako fanya hivyo ona hivyo na ishi hivyo.
WAKILI ; amesema yeyote haruhusiwi kujivuna, maana hata yeye haruhusiwi kujivuna wala kuringa, yeyote asiringe kuanzia MIAKA 1000 mpaka wa kwanza sana.
Aidha katka ibada hii Wakili wa MUNGU amefunua Jeshi Maalumu na Moto maalumu wla kuhukumu na kuteketeza kabisa akiba mbaya zote ndani ya Moyo wa kila mwenye Haki yetu.
Hivyo leo tunafuta kujihesabia haki tunataka wewe MUNGU ndio utuhesabie haki.
Sadaka maalumu ya leo Yeremia 30:23-24 ghadhabu ya MUNGU. Isaya34:8 kisasi cha MUNGU, 1PETRO 1:17 kiti cha MUNGU kuhukumu.
Alisema sadaka maalumu ya leo inahukumu uovu wote tangu mlimani maana Wakili alitubu kwaajili ya uovu wote tangu mlimani na vizazi vyote.
Wimbo; Sitatoka kama nilivyokuja nimekutana na BABA…….. KRISTO…….. WAKILI WAKE……. mahali hapa yupo MUNGU ( ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.
MUNGU tayari yuko hapa na sadaka hii imepata kibali mbele za MUNGU.
Kila aina ya kichaka cha mateso taabu nk kinaungulia hapa kwenye sadaka.
Kwa sadaka na shuhuda sitakutana na mateso tena MUNGU yuko hapa kuhukumu yote.
Hata ule mwiba MUNGU ameuondoa. Sitakumbuka mabaya tena maana moto umetokeza kwao.
Nashukuru kwa ajili ya waimbaji wamesema kweli inakaa ndani ya moyo. Pale MUNGU alipoanzia ndio tumefika, ndio sababu MUNGU ametupa leo somo la MOYO.
Mawazo , kumbukumbu, ujuzi, ufahamu, kufikiri yaliyokuwa ndani ya moyo.
Katika mengi zaidi kulikuwa na mioyo mingi badala ya moyo mmoja.
Kwa nini moyo umechorwa hivi kwenye zawadi tuliyopewa leo tofauti na jinsi ambavyo tumezoea, tofauti na ambavyo huwa unachora na tofauti na ulivyofundishwa shuleni.
Moyo ni nini ? ZABURI 19:14 Uone ndani ya moyo jinsi ambavyo kunakuwa na mawazo mengi tena tofauti tofauti.
Yaani umekaa ibadani sasa hivi lakini unasababisha uende pishoni, mlima wa moto , ofisini, nk ukiwa umekaa hapohapo.
Daudi aliwaza na kwa majira ile ilikuwa ni lazima uwaze na ilikuwa inaruhusiwa, hivyo aliomba kwa MUNGU kwamba mawazo yake yapate kibali.
Majira hii haturuhusiwi kuwaza bali ni majira ya TENDO MOJA HALISI. Kwa hiyo unaomba upate kibali kwa tendo.
Usiposalimiwa tu unawaza kuwa anakuchukia wala huwazi kwamba atakuwa ameamka ana mawazo mengi aa huwazi kuwa huko alikotoka kakutana na mangapi!
Ukiona wanaoongea mpaka wanagonga tayari umeshawaza wanakusema wewe.
Kuanzia leo miaka yote 1000 ya kutawala na KRISTO sitakuwa na WAZO BAYA milele.
LUKA2:19 Lakini Yule mariamu aliyaweka yale maneno moyoni mwake.
Moyo huwa unafikiri tatizo ulikuwa siku zote unafikiri mabaya.
Hata WAKILI hizi siku 3, 4 ambazo hakuonekana kuna waliofikiri sijui amenuna, amekasirika amezira wala hakuna aliyekuwa anasema atakuwa ameenda vituo vingine, au atakuwa ameambiwa na MUNGU abaki.
Kuna wengine walipewa taarifa za uongo na waliofeli tangu lini waovu wakaijua sauti ya mchungaji mmoja? Kuanzia leo mimi….. sitaisikiliza taarifa za waovu nikaziweka ndani ya moyo zikaniumiza.
Sitakutana na taarifa ya mjinga nikakubali nikaweka ndani ya moyo.
Leo naondoka na moyo wa MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE unaoona mema tu!
Jinsi moyo ulivyokuwa na mambo vitu vya hovyo!! KUMB 8:5
WAKILI alisema “mara nyingi nikimkemea yeyote hapa wengi huwa mnawaza mnafikiri kuwa kuna kitu nimeambiwa nimesikia kwa yeyote”.
Bali leo tambua kwamba sio kweli kwamba anakuwa ameambiwa bali ni MUNGU mwenyewe …. Kuna Neno linasema BABA humrudi mwanae…
MUNGU ametupa mwanzo malidadi tunatakiwa tuwe na moyo mmoja wa MUNGU usiosikiliza taarifa maneno, mambo mabaya yote nk
LUKA 6:45 tabia ya leo unanena mazuri kesho mabaya imefutwa na wengi tumekutana na watu wa aina hiyo, leo unaelewana na kichwa/kanisa kesho ngumi hamuelewani tena, leo unaelewana na watoto, majirani, ndugu kesho hamuelewani imefutwa.
Leo MUNGU anayaondoa yote maana ni wakati wa kuja na fungu la MUNGU yaani fungu la kumi kikapu imejaa .
Kwa hiyo leo hicho chumba na nafasi ndani ya moyo kimefutwa , leo vyumba viwili vimeondolewa kimebaki chumba kimoja cha HAZINA NJEMA.
MOYO WA KANISA ninaosema mimi ni ule moyo ulioungana na nafsi sio ule moyo unaokaa upande wa kushoto ambao unakuwa na pande mbili na unachorwa na mkuki.
ZABURI 119:11- ZABURI 27:4 Ifike mahali ujuzi wako uwe ni NENO tu! Ufahamu wako uwe ni wa NENO, kumbukumbu na mawazo na kufikiri kwako iwe ni NENO pekee.
Unafahamu kwa nini dar-es-salaam iliitwa bongo?? Ni kwa sababu ya uongo, udanganyifu hivyo ikatokea bongo fleva sifa za uongo, zilianzia hapo.
Ndio sababu mtoto akiwekewa bongo fleva hata kama upo kwenye daladala tu utaona anacheza.
kijana ukiweka bongo fleva anacheza utasema aliwahi kwenda disco kumbe ndio kwa mara ya kwanza anaisikia ndio utaona anavyojinyonga nyonga kama nyoka.
Kwa kweli leo tumepona kabisa kabisa! Maana MUNGU asingenipa huu moyo wake sijui ingekuwaje.
Kwenye mtihani wowote utakaokutana nao leo utajua tu cha kujibu maana umepewa moyo mmoja wa MUNGU na umejaa NENO.
Leo naondoke na moyo mpya ule wa zamani nauacha leo madhabahuni uungue kabisa.
MITHALI 3:3-4 Rehema na kweli zisifarakane na mimi mwenye haki milele. Yaani kusamehe bila kuombwa msamaha.
Ndio sababu nilikuambia ninapoona yeyote anataka kunikosesha namuona kama kichaa kwangu.
Mimi siishi kwa nafsi yangu wala kwa ajili ya family yangu bali naishi kwa ajili ya kizazi cha MUNGU.
Unafikiri MUNGU anapothubutu kuapa kuweka agano au kusema kwa kutumia kinywa changu na kusema kuwa Tanzania ni urithi wake unafikiri mimi natakiwa kukaakaa tu?
Lazima kila siku niombee taifa hata kama kuna polisi na wana silaha lazima niombee TAIFA. Niombee viongozi wote.
Mimi huwa sina tabia ya kuja kukuuliza eti nimesikia umesema hivi. Acha kuuliza utafuta kujitetea je utawafuata wangapi?
WAKILI WA MUNGU; Leo ujue kama ulikuwa unafikiri unajua mimi ni mtu leo ujue kuwa mimi sina chembechembe za mtu wala mwanadamu.
Ndio maana sina kikao na yeyote.
Kama wewe unataka moyo huo chukua , usimhukumu yeyote kwa maneno ya kuambiwa, usimshitaki yeyote.
Usimhukumu RAIS maana kuna wengine wanamhukumu tena kwa maneno ya kusikia.
Wengine mnathubutu kunihukumu hata mimi WAKILI WA MUNGU hamjui mtakufa? Je mlijua ELIYA AD2 anadanganya?
Maana Eliya alinitambulisha mimi kwenu, Akasema afadhali mnikosee mimi mtasamehewa lakini msimkosee MIAKA 1000 kwa kuwa hamtasamehewa milele na MUNGU.
Sasa je hao wanaonitukana wananishitaki je mnafikiri MUNGU atawaacha? Hawezi kuwaacha kabisa!!
Je hawakumjua ELIYA? Je hawakusikia? Je hawakuwepo hawakuonywa hawakuambiwa? Je hawakumwamini? Je hawajaishi nae?
Leo naondoka na moyo usiokufa, usiougua, usiolazwa mwananyamala, usiopungukiwa, usioishiwa, usiokutana na huzuni uchungu mateso usioona kutukanwa, usiozimia usioanguka Isaya 40:28-31.
NAONDOKA NA MOYO USIOISHIWA KILA SIKU SHANGWE NA NDEREMO.
Je huu moyo unaupenda? Uchukue huo! Moyo usioshitakiwa mahakama yeyote, haufungwi hauingizwi selo.
Kama mlijua mimi ni mtu, mimi sio mtu, nasema sio mtu mimi Wakili amesema.
NJIA ZA BWANA waambie kweli mimi sio mtu
Kila aliyekuchezea apokee mapigo, kila aliyekuonea, aliyekunyanyasa ni zamu yake leo kunyanyaswa. Kila aliyeonea Taifa hili ni zamu yao kuonewa.
Mataifa yaliyopokea siloamu yamepokea chochote walichokuwa wanahitaji.
Muwapelekee salamu hizi;
Rais wa Malawi amelikubali kanisa na cheti tayari. Shida yoyote iliyowapota Malawi leo ni mwisho.
MUNGU amekuja mwenyewe fullfull. Wimbo - amekuja mwenyewe MZEE WA SIKU kuongoza kanisa, kuangamiza vibaya wabaya wote.
Tunayabariki haya mataifa matatu maana yamempokea MUNGU mwenyewe mzima mzima.
Nimeambiwa Kenya, Rwanda watasaini, Botswana wanamsubiri wakamkabidhi cheti.
Uganda wamemwambia amalizie ujenzi wa vyoo wampe cheti.
Mozambique wanamsubiri kuh wakamkabidhi cheti, Zimbabwe kuhani aende akachukue cheti tayari.
Ila hawa niliokamata cheti chao hapa wabarikiwe, na hawa watakapopata shida yoyote hata wasipige simu wainue hiki hiki cheti na hiyo shida itaishia hapo hapo; nchi ya Malawi, Zambia na South Africa.
Ibada hii imeangusha ukuta wowote uliokuwepo kati yetu na MUNGU,
MARKO 7:20-23 Ili upokee huu moyo uliokuja leo , uliopokea leo lazima ukubali au unatakiwa kusamehe na kusahau.
Uwe na moyo wa rehema na neema ya kusamehe bila kuombwa msamaha.
Ili ujue kuwa umehama ama hujahama unatakiwa ukiona bado unashitaki wengine, una hasira, unakwazika tu, unazira safu kwa sababu umesemwa, bado unagaragara ukitaka uonewe huruma kwa mahali unapopita , unaona makosa kwa wengine.
Ukiona bado unaona majaribu mpaka leo ujue hujasamehe na hujahama, majira hii hatuna majaribu bali tuna mtihani.
KUMBU 8:2 Test Heart Hutaishi kwa mkate tu bali na kwa NENO linalotoka madhabahuni.
“CHETI cha kusamehe kuachilia na kusahau kanisa tumepewa.
Cheti hicho natakiwa nikiandae vizuri na nikipambe halafu nikining’inize sebuleni pale, chumbani kwako, jikoni hadi bafuni ili kila wakati kikumbushe kwamba umesamehe na kusahau.
Kazi ya kuhukumu ni ya MUNGU” alisema Wakili wa MUNGU.
Mtihani anatoa MUNGU anafanya yeye anasahihisha yeye na anatoa maksi A+.
Kila askofu, mchungaji, shehe, padre, watakuwa wanazungumzia SILOAMU.
Najua kuna wengine sasa hivi wameacha kula kwa vijiko huko lutherani na rc.
Kkkt wana morning glory, wana maombi ya kupatana , Je wametoa wapi hiyo ??? SILOAMU!!!!.
Sasa swali langu ni moja je tungekataa kutukanwa kusemwa vibaya? Haya yasingetokea.
Hivi ni kweli unaweza kuanza sekondari bila mtihani, unaweza kuingia chuo bila mtihani?
Mniambie leo je wasomi unaweza ukawa doctor mwalimu profesa bila mtihani? Unaweza kupataa phd diploma digrii pasipo mtihani?
Unapokutana na mtihani kwanza kabisa shukuru MUNGU kwa promosheni,utaona jinsi MUNGU atakavyotenda.
Atafanya yeye mwenyewe, atasahihisha yeye mwenyewe, maana mtihani katoa yeye na ni lazima upate A+.
Wale wanaonichukia ni wale watoto wanaopenda kila siku kurudia rudia mtihani na MUNGU anasema utarudia mpaka utakapokuwa mzee.
Maana kama unakimbia mtihani kuzeeka kwaja kwako.
Mtoto yeyote asiyependa mtihani sio mzuri maana anapenda kumaliza hela tu kwa ajili ya ADA maana anarudiarudia darasa.
Unapotoka ibadani kabla ya ibada kwa sababu unawahi appointment ina maana hutaki mtihani unakimbia mtihani.
ISAYA 55:1 UKIONA ISAYA 55:1 haikupi shida ujue umetoka na moyo wa MUNGU leo.
MWANZO 2:5 wakati MUNGU anatamka hayo yote hapakuwa hata na karamu lakini alijua tu kwamba kushiriki karamu damu, kuvaa, kupendeza, nyumba mtaji.
Leo ondoka ukijua wewe ni tajiri kuliko Trump.
YOELI 3:10 aliyedhaifu na aseme kuwa yeye ni hodari. Kama uliambiwa leo unkufa basi ujue na uone kuwa wewe ndiye unaetakiwa kuishi milele hutakufa.
Kama ulikuwa na chumba kimoja leo ona kuwa una gorofa, kama ulikuwa na jembe moja ona leo una trecta,
Kama ulikuwa unashitakiwa kila mahali,unachukiwa, unakataliwa, na mpaka kuna vikao vinavyoendelea kwa ajili yako vya kukufukuza leo nataka uone kuwa unapendwa.
Iko njia mahali pasipokuwa na njia ISAYA 43:16
Dada mwenye miaka 60 70 80 hata 100 nataka uone kuwa umevaa shera maana ISAYA 34:16 Inayosema hakuna atakayekosa kuwa na mwenzake.
Hata hivyo pamoja na yote hayo hakuna mwenye miaka 100 wote tuna miaka 6 tu! Wewe uliyeambiwa ugonjwa ulio nao huwei kupona leo uone kwamba umepona MATH 10:1 na LUKA 10:1
JE UMEPOKEA MOYO MPYA LEO? JE UNAJISIKIAJE?
Aidha Kiongozi wa Makuhani Kwenye ibada ya pili alisema tunaona kumbe moyo ulikuwa na vyumba 2 kimoja cha mema na kingine cha mabaya.
Hivyo hakuna asiyejijua jinsi alivyo kama wewe ni kahaba unajijua, kama wewe ni mwizi unajijua kama wewe hujasamehe hujasahau unajijua vizuri.
Wala usiseme mimi sijijui nilivyo je hujui rangi ulio nayo hujui vazi la kanisa ni nini?
Hivi unapoenda hospitali daktari akasema nimepima nimeona wewe ni kanisa wakati wewe ni kichwa utakubali? Hapana
Atakuambia nimepima mara 3 je utakubali wewe ni kanisa wakati wewe ni kichwa?
Je utakubali wewe ni kichwa na upo madhabahuni ukiwa na shera? Hiyo haiwezekani.
Uwe na hakika ya NENO safari hii hakuna sogea tukae.
Ni magari ya zamani sana yalikuwa yanaitwa chai maharage ndio yalikuwa na hiyo kanuni ya sogea tukae hata hivyo kwa sasa hayapo tena.
Hivyo tengeneza moyo wako leo usiwe na wale wa sogea tukae.
MCHUNGAJI MMOJA AMEKUPA MOYO WAKE ISAYA40:28-31 ISHI HIVYO ILI USIKUTWE NA EZEKIELI 28:18.