Jumatatu, 6 Februari 2017


MUNGU ANAMTOA KANISA ILI AONEKANE INAVYOMPASA KUWA

FALME 17:1 Wakili amesema hatukuwa na kosa ila alichofanya mzee wa toba ni unyenyekevu wa moyo.
SADAKA maalumu ya kumpokea baba. Kurejea kwa nguvu kubwa ya ubaba, utendaji wa ubaba, kujulikana kwa baba katika mataifa yote ndani ya uumbaji wote,
Mamlaka, sauti, uhalisi, utisho wa ubaba, hatma na ukamilifu wa ubaba, majira ya ubaba, nk.
Hivyo leo kila mwenye haki anaondoka na kapu la utajiri. Madhabahu ya utajiri kwa upya.
Leo tunatubu kwa ajili ya roho aliyekuwa duniani AYUBU 42:10 MUNGU aligeuza uteka wake,
Kulikuwa na shida nyingi za fedha kutokana na uteka wake uliokuwa umetokana na ukame wa muda mrefu.
Kushukuru MUNGU kwa kuwa kugeuza uteka wetu. Waliokutesa waliokudhihaki MUNGU amegeuza uteka.
Kila anayetenda kwa haki hatachanganyikiwa milele, hataonewa tena.
Leo tuombee adui zetu ili MUNGU ageuze uteka wako.
1YOHANA 5:9 Kanisa lilivikwa mavazi mabaya mpaka likawa linaonekana baya.
Ni wakati wa kusafisha kanisa kuondoa matusi.
Kizazi cha 1-4 kanisa lilionekana baya lakini kizazi hiki cha MUNGU kanisa lazima lijulikane kwa sababu yeye mwenye shamba kaja.
Ni wakati wa kutubu kwa ajili ya matusi ambayo MUNGU anatukanwa.
Na Kanisa alivyowahi kutukanwa kwa sababu kwa kutukanwa kwa mwenye haki unyonge uliingia ndani yetu na tukaona labda hapa si kanisa,
Tukaona kama hakuna MUNGU na pia tukafika hatua ya kuuza Baraka, hivyo ni wakati wa kumtakasa kanisa ili aone kuwa sasa ana BABA.
Sasa sura mpya ya kanisa inaonekana kwa uhalisi.
Kao la dunia lilikuwa ndani ya kanisa, kizazi cha 1-3 kanisa halikueleweka, kizazi cha 4 kanisa lilipotokea walianza kusema ni freemason nk.
Kizazi hiki amekuja mwenyewe hivyo lazima waone sura halisi ya kanisa ndani yangu mimi mwenye haki.
Huko wajibu wa moto, mlima wa moto, biashara zako, ofisini kwako wamjue MUNGU, KRISTO, KANISA kupitia wewe ili kao la dunia liondoke ndani yako, kanisa.
Aidha sura ya kanisa ilikuwa haikuwahi kujulikana wala kueleweka. Kanisa lilionekana la wenye vilaka lililochoka nk.
Leo tunataka sura halisi ya kanisa ionekane kila mahali, kutubu kwa kutojulikana kwa sura ya kanisa.
Kao la dunia kwa maana ya kuwa na lugha ya dunia , muonekano wa dunia, utendaji na kanuni za dunia, nk tuliondoe ndani yetu kataa kabisa ili kao la MUNGU likae na kuonekana ndani yako.
Mawazo mabaya akili mbaya mafarakano hayataonekana tena ndani ya kanisa.
2KOR 12:2-7 leo tunawaondoa wajumbe wa shetani ndani yetu.
Ambao ni magonjwa utasa kupungukiwa nk, tunafuta kituo cha mjumbe wa shetani kukaa ndani ya kanisa tunafuta.
Kuna kuhani alikuja kwangu akakuta tunashiriki kwa mkono ….
Akafananisha na Parestina sasa hii ya Kanisa kufanya vitu vizuri na kufananishwa na sehemu nyingine hii hatuitaki tunataka kila atuonae aone kanisa.
Mahali popote ulipo lugha yako iwe ya kanisa ijulikane, sura ya kanisa ni kuanzisha viwanda bila mkopo,
Ni kulima shamba na mazao yakaota na kusatawi shambani mwako lakini jirani yako hayajaota kabisa.
ISAYA 60: lugha yako ibadilike kwa kuwa wewe ni kimbilio kila uendapo ukiwa mlima wa moto na wakikufuata wakisema wana shida usiseme hata mimi ninashida.
SADAKA maalumu ya kumuondoa mjumbe shetani ndani ya kanisa, sasa amekuja na ijulikane kuwa tunaishije tunakulaje.
Yosh 20:5 kanisa ni mji wa makimbilio kwa uhalisi, usizungumze matatizo zungumza shuhuda ndio chakula cha MUNGU.
2FALME 3:11-15 mvua kunyeesha, 2FALME 2:19-22 sura ya kanisa ni hii kuondoa mapooza.
2FALME 6:1-6 shoka lilipoanguka kwenye maji … umbo la physics likafutwa.
2FALME 7:1 karamu itauzwa sawa na bure. Kisichowezekana kwa mtu kwa MUNGU yote yanawezekana na tumeungana na huyu MUNGU.
Shida yetu tunaomba na kufuta wenyewe kutokana na yale unayonena ukishatoka kwenye shukrani hatuamini hata tunachoomba leo mwisho.
Tokea kwenye umbo la mila na desturi ya kwamba anayeoa avae hivi au nyumba ya aina Fulani.
Mith 31:10 Inatakiwa Kanisa MUNGU atuamini na kuna namna MUNGU anashika handbreak kwa sababu anaona kama tutauza.
Kama atafanya vyema basi kichwa hatakosa kumtendea mema.
Kuamka saa 8-9 sio utumwa bali kwa kanisa ni sahihi. Usikubali kabisa kichwa wako aaibike.
MUNGU hawezi kukusaidia kama unamuwasha kichwa wako.
Na walio na hekima watang’aa kama jua, fungua kinywa chako kwa hekima.
Mwenye kusababisha MUNGU kujulikana, kichwa kujulikana ni Kanisa.
HESABU 30:1- usiulize mbona hupendezi kanisa wangu, unatakiwa usababishe apendeze.
Kama kanisa hajui kupiga pasi mfundishe kama hajui kupika mfundishe nk
Usilaumu mfundishe, usimwambie kanisa wako kuwa nataka upendeze kama mke wa Fulani.
Tabia inayoonekana kwa kanisa wako ndio ipo kwako wewe kichwa.
Kwa unayempenda lazima akutii kanisa asipokutii ujue wewe kichwa humpendi.
1KOR 13:1- upendo hauangalii mazingira, hivyo kilazimisha akutii wakati wewe mwenyewe haumpendi ndipo na makofi yanapoanziaga.
Mimi nikiona kichwa anayelalamika kuwa kanisa wake anapiga sana simu kwao anaongea muda wote mimi huwa najua kabisa shida ipo kwa kichwa wake;
Mwenyewe ina maana hajaona ndugu rafiki kuhani kichwa ndani yako kichwa. EFESO 5:22-25 kwa habari ya kichwa na kanisa.
Hekima isipungue ndani DANIEL 12:3 wenye hekima watang’aa kama jua.
EFESO 5:25-27 kanisa apendeze asiwe na madoadoa mawaa awe na kicheko wakati wote.
BABA wa uumbaji wote ametupatia tulio wake *SHERIA YA WEMA* ambayo makanisa hufumbua kinywa kwa hekima kwani Sheria ya wema I katika ulimi wake ili vinywa vyetu vinene yaliyo mema na yenye hekima ili ajulikane kote Mith31:26.
Hatahivyo Wakili wa MUNGU amesimamisha *SHERIA YA WEMA* kwenye vinywa vya makanisa ili vinene yaliyo mema na yenye hekima.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo kabla ya Wakili wa MUNGU kufika Mzee wa Toba na kiongozi wa Makuhani alisema;
Alianza na shukrani za kuinua taifa na viongozi wote watendao kwa haki nk 1TIMOTH 2:2-4.
Toba kwa machukizo yote ili MUNGU atembee nami na aishi kwangu.
Kutomfahamu baba mmoja wa rohoni, kutubu kwa kipindi ambacho kanisa lilibaki kama yatima na ile nguvu ya ubaba ikachukuliwa na dini na dhehebu;
Kukawa na mababa wengi, baba wa ubatizo kipaimara ndoa nk leo hiyo imefutwa.
Mtoto asiyemjua BABA ana tabia mbaya na ukimkataa BABA umemkataa MUNGU.
Sifa za kumfahamu na BABA zinazosababisha umpende na BABA akupende;
Kataa mababa wengine wote.
Ukubaliane nae kwa jinsi alivyo.
Usitake baba yako aaibike.
Chochote kinyume na baba yako unatakiwa uingilie kati kwa toba.
Kusema kweli tu!
Alisema Wakili wa MUNGU hatuonyi tunayoyafanya kwa sababu hatujamtambua hivyo wengi tukionywa tunakwazika.
1SAMWEL 8:1-8 , siku ya 4 ile Math 21:41 ilitimia kwa uhalisia baba mwenyewe yupo.
DAN 2:44 utawala wa amani umesimama kwa kuwa ufalme wa mabaya na mabaya na watendao hayo mabaya wamefutwa milele.
Mahali pa kabla ya wazo la kumuumba kerubi ni mahali pa mwanzo malidadi, faraghani.
Ni mahali pasipo na mwanamke, joka, falme na mamlaka, pepo wachafu , magonjwa, umbo la mtu na mwanadamu, hekima ya dunia,
Ni pale ambapo alisema pakiwepo lugha kinyume na MUNGU zitakoma na zimekoma.
Ni mwanzo wa kutoonewa, kutopigwa, na kutopatwa na mabaya yote.
YEREMIA 50:20 Utaitafuta dhambi hutaiona ni mwanzo wa njia moja ISAYA 35:8-10 isiyo na kuishiwa kupungukiwa kukanyagwa nk.
Tunae baba mtakatifu Wakili wa MUNGU. EBRANIA 6:12 msiwe wavivu muwe wafuasi kwa imani na uvumilivu.
Uone mema tu! Uone kusudi la MUNGU kwa kila mmoja.
Vitabu vingi vimeandikwa ili kuonyesha njia ambayo kanisa tumeipitia.
Wewe kama ni kiongozi utupe njia ya kanisa hata Musa alikuwa na njia aliyowapitisha Israeli ya mwilini.
1SAMWEL 11:1- ni marufuku kwenda kwa waliopigiwa kura.
Ni hatari sana kumkataa aliyepakwa mafuta na MUNGU.
HESABU 2O:14 Usije ukang’olewa macho na majira hii watang’oa na ulimi, utumbo nk.
Ukiongozwa na wenye moyo mbaya huwezi kuvuka hata siku moja.
Kwa nini baba hapikelewi? Ni kwa sababu hakuna aliyewahi kusema baba atakuja walikuwa wanasema Yesu atarudi.
Aidha Mzee wa toba na Kiongozi wa Makuhani amefanya toba maalumu kwa kanisa Kataa mababa wengine wote,
Mengine ni kutokubaliana nae kwa jinsi alivyo, kutaka BABA aaibike, kutoingilia kati kwa toba kilichofanywa kinyume na BABA na kutosema Kweli.
Lakini pia Mzee wa Toba ameongoza wenye haki leo kutoa Sadaka maalumu ya Kumpokea BABA na kuagiza Makuhani wote kusimamia ukusanyaji wa Sadaka Maalumu hiyo ili wenye haki wote tuweze kumpokea BABA.

Jumapili, 5 Februari 2017

      KANISA LA SILOAMU NI NAFSI YA TATU YA MUNGU


Kabla ya BABA kufika Mtendaji wa Wakili wa MUNGU aliongoza shukrani za kuombea taifa; Yer 29:7 kuombea mji ili uwe na amani.
1tim 2:1-4 Kuwaombea wote walioko madarakani. Tena wanafanya jambo zuri kumuweka MUNGU mbele.
EFESO 3:10 Hekima ya MUNGU iliyo ya namna nyingi kujulikana na watu wote.
War 13:1- kila mtu na atii mamlaka kwa kuwa kila mamlaka yatoka kwa MUNGU. Mamlaka iliyopo yatoka kwa MUNGU.
Na kila ashindanae na mwenye mamlaka ashindana na MUNGU na amuasi MUNGU.
BABA
Leo ni mwisho wa yeyote kushindana na Kanisa.

      *TANGAZO!*
*NI MWISHO WA MUOVU KUSHINDANA NA MWENYE HAKI, MUNGU KRISTO KANISA WAKILI TAIFA NA KIZAZI CHA MUNGU.*
Tangazo hili liende mpaka kuzimu ujinini kwa wachawi waganga walozi washirikina wanajimu waovu waasi watenda dhambi walioushitaki;
Waliokutukana waliokudhihaki waliokudhulumu waliokuonea wanaokunyanyasa kwamba hakuna wa kushindana na mwenye haki milele.
Los angels wamesikia the head wamesikia Tokyo wamesikia waliojificha kwenye Pluto wamesikia kwamba hakuna wa kushindana na mwenye haki milele.
Musa aliwaambia Israeli ya mwilini nyamazeni kimya muuone wokovu wa BWANA, je waovu washitaki wao waliuawa hawakuuawa?? Waliuawa.
Muovu yeyote hatavuka milele, njia ya mwenye haki muovu hapiti, haruhusiwi kupita,
Wote wanaoshindana nawe mwenye haki wanashindana na MUNGU,
Tangazo hili ni kwa wenye haki pekee unaweza ukawa hapa lakini si mwenye haki basi ujue tangazo hili halikuhusu kabisa.
Mdo 13:6 Kiapo: Kila anayeshindana na mwenye haki kuanzia sasa na awe kipofu!

Awe pepo mkuu wa anga mchawi mlozi afe sasa hivi.
Je unaamini imekuwa hiyo? Naamini imekuwa!  Aliyesababisha uwe tasa uachike utaabike ufukuzwe kazi wote hao hawapo milele.
MUNGU nashukuru kwa sababu asubuhi asubuhi umenitokezea na zawadi na haya yote MUNGU naamini napokea imekwisha tokea.
Mdo 4:24 kumuinua MUNGU kwa sauti moja, ni mwisho wa anayeshindana na mwenye haki.
Namshukuru MUNGU kwa kuwa jana MUNGU amenivika vazi la ubaba.
Ubaba ni nguvu inayopenya kila mahali, hata mtoto anapoanza kusema huanza na neno baba, sasa namshukuru MUNGU kusanyiko limepata baba.
MUNGU amegonga muhuri 7 kuwa Wakili ni BABA, usiyempenda kaja, tuache mazoea na kawaida yanayosababisha tusipate udhihirisho.
Leo tutubu ili viongozi waje Madhabahuni mchana tunawatoa mahali walipokuwa wamefungiwa na Nikodem kuwa viongozi waje usiku tu Yoh 3:1-
Maana ilitakiwa sasa hivi Wakili wa MUNGU awe bungeni akiliambia taifa lisiwe na wasi wasi limechaguliwa na MUNGU kuwa urithi wake.
Tatizo hata mabosi wetu hatuwaambii habari za MUNGU tuliyenae hii sio nzuri tubadilike.
2FALME 5:20-26  tusiwe kama Geazi aliye mfuata Naamani aliyekuwa ameenda kwa Elisha kwa ajili kupata uponyaji, wala ELISHA hakutaka chochote kutoka kwake;
Huyo mfalme hivyo alipoondoka tu Geazi alimfuata akataka fedha kwake.
Tusifanye hivyo ili viongozi waje kwa MUNGU wa kweli.
2FALME 3:11 viongozi wote tunawaunganisha na Mfalme Yehoshafati kwamba watafute hekima watafute ushauri kwa aliyembeba MUNGU na KRISTO wake.
Mahali walipokuwa wamezika nafsi ya Kanisa na taifa leo ni mwisho, walipokuwa wamezika Baraka zako, sura yako, afya yako, mtaji wako leo vimefufuka.
Nafsi yangu naipa nguvu itoke huko sasa hivi kwa damu ya MUNGU.
*LEO WENGI TUTAPATA PROMOTION YA AJABU.*
Aidha Sadaka Maalumu ya leo WALAWI 16:17 ya kufufua kila kitu cha mwenye haki kilichokuwa kimezikwa.
Kila aliyewahi kuleta hasara ndani ya Kanisa, matatizo shida anayekula sadaka hiyo anakula shida zote za wenye haki.
Hakuna shida itakayobaki kwa sadaka hii ya leo.
Shida ya nafsi yangu leo ni mwisho. Mwanzo wa uharibifu haupo tena.
Akifafanua kuhusu Kanisa la Siloamu ni Nafsi ya tatu ya MUNGU Wakili wa MUNGU alisema Kuna maswali matatu yanahitaji majibu:-

Kanisa ni nini ??
Siloamu ni nini??
Nafsi ya 3 ya MUNGU ni nini??
Kanisa ni kusanyiko ambalo halishindwi na malango ya kuzimu MATHAYO 16:18  Yesu alisema…..
Hata ukiona wana jengo zuri, mchungaji mzuri, askofu mzuri, lakini kama wanashindwa na malango ya kuzimu hilo sio kanisa.
Kigezo cha kupima sio maneno matamu matamu na lugha bali ni linaloshindwa na malango ya kuzimu.
Efeso 3:10  Kutia adabu, Kanisa ni Kusanyiko lenye hekima iliyo ya namna nyingi ya kuangamiza falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho chafu, pepo wabaya, wakuu wa giza.
Ufu 11:6  kanisa ni kusanyiko lenye hekima ya kubadili maji kuwa damu ya chochote ili kuangamiza kutia adabu waovu wote.
Ukiona wanaochukia kanisa ujue ni kwa sababu kanisa lina hekima yenye kuwaua maadui wote.
Kuhama kituo, 1FALME 2:1-14  ukiona yeyote hataki kuhama vituo ujue hao ni dini.
Kutembea na wingu la moto wingu la MUNGU, kutoka 13:21-22 BWANA akawatangulia mbele yao Kanisa ni kusanyiko ambalo MUNGU anaonekana wakati wowote.
Anaongea anasema kila siku anatupatia vitu vipya.
MUNGU huwa anatabia ya kuwaleta adui zako karibu ili apate kuwaangamiza Kut 14:
2kor 12:2-  kanisa ni kusanyiko linaloanzia  au la wanaoishi juu ya mbingu ya 3 mahali kerubi hawafikii.
Mahali penye ufunuo uliomuua asi 2thes 2:8.
Ukiona mahali wanapopiga kura ujue hapo sio kanisa ESTA 3:7,
Ukiona kusanyiko linaloishi kwenye majira na nyakati za dunia za januari mpaka desemba ujue hiyo sio kanisa.
Hata kama unasema Bwana asifiwe wewe ni mkatoliki tu!   Yoh 4:23-24   na ile saa aliyoisema Bwana Yesu haikuhusu kubisa.

Kanisa lina majira na nyakati za mwaka wenye miezi 12, mwezi ukiwa na siku 28, wiki ina siku 7, abibu mpaka adari.
SILOAMU ni nini ? Yoh 9:7 mwilini Siloamu ni bwawa lililopo kule mashariki ya kati, 
Rohoni Siloamu ni bwawa lililopo hapa, maana yake Aliyetumwa na baada ya MUNGU kuja mwenyewe sasa inaitwa sioamu ya ALIYETUMA WOTE.
Katika vizazi vilivyopita wewe ulinawishwa na waliotumwa majira hii unanawishwa na ALIYETUMA WOTE.
Nafsi ya 3 ya MUNGU ni nini? 1 Yoh 5:8  MUNGU ana nafsi 3 ikiwa na maana nafsi ya roho ndio kanisa.
Roho ilikuwa duniani 1YOHANA 5:9 kazi yake ilikuwa ni kwenye uumbaji wote.
Uumbaji wa MUNGU ulianzia ZABURI 98:1  kitu cha kwanza MUNGU aliona sifa,
Akaamuru nyota jua nyota ambao walikuwa ndani fake watoke wakicheza cheza ndipo mavumbi yalipoonekana akatokea mwanamke ufunuo 12:1-3 badala ya kanisa.
Kwa hiyo tunaona kuwa kumbe uumbaji haukuanzia Mwa 1:1 , wala Ezek 28:15.
Yosh 6:26 kila alichokuwa anatamka kilimtengeneza mungu m ndogo.
Mlima wa MUNGU ni hapa bustani ya Edeni ni hapa wale wote wenye maneno mabaya kwenye mitandao waache MUNGU majira hii haachi wanaomtukana,
Akaongeza kusema kuwa  kanisa ndilo linalomkamilisha MUNGU.
Kanisa  la Siloamu ndio limeleta Mwanzo Malidadi, limetoa ufalme wa MUNGU Israeli limeleta hapa Gosheni.
Wakili amesema tuseme kweli DANIEL 2:44 kama husemi kweli ina maana wewe hutaki utawala wa amani,
DANIELI 2:35 hutaki kanisa lijulikane kuwa ndio jiwe walilolikataa waasi limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Hamtaki waje kuhiji hapa? Tunataka. Semeni kweli basi.
MUNGU yuko hapa na ndio ameshakuja hivyo hatoki na miguu kaweka hapa hapa na kiti chake kipo hapa na hatoki milele. 
Sauti kuu 2 zilizobadilisha majira na nyakati zimetokea hapa kwa nini hamtaki kusema kweli? 
Upo tayari kujivunia taifa lako na kanisa lako, upo tayari kuwaambia twendeni kwa ALIYETUMA WOTE!! 
Katika ibada ya pili;
WAKILI wa MUNGU amesema; wenye haki tunaondoka tukiwa tumevikwa Vazi La Ushindi,
Maana nina BABA imefika wakati wa kukunja shati na kusema sasa njooni Yosh 1:5 kwa uhalisi hakuna asimamae mbele yangu.
Mahali popote ulipowahi kutukanwa, tusi hutaliskia tena milele.
Hata wadudu wote wazungu waamerika wamejua kuwa mimi mwenye haki situkanwi tena.
Ni tangazo lililosimama ndani ya uumbaji wote 1Yoh 3:14 sisi tunajua ya kwamba tumetoka mautini tumeingia uzimani.
Hakuna wa kunitoa hapo hakuna wa kunishitaki kunihukumu hapo milele.
Kila kinachoitwa kwa jia langu kimetoka mautini kimeingia uzimani. Nafsi yangu haitafungwa fungwa milele.
BABA tunae tuseme kweli ili kila tunapopita wajue kuwa hawatuonei tena!!!

Jumamosi, 4 Februari 2017


KUSIMAMISHA MAJIRA NA NYAKATI ZA VAZI LA UBABA MMOJA TU NDANI YA UUMBAJI WOTE.

Kabla ya MZEE WA SIKU kufika *Mtendaji wa Wakili,* kiongozi wa Makuhani alifundisha haya;
Ndani ya majira na nyakati za moyo wa MUNGU.
Toba ni sawa na kujiangalia kwenye kioo kila siku ili MUNGU aweze kukaa na wewe kuishi na wewe.
Toba ni sawa ilivyo lazima kila siku ukiamka unanawa uso, ni kunawisha moyo kila siku.
MUNGU leo natubu kwa kila kitu kilichoingia ndani yangu kinyume na MUNGU aliyetuma wote vizazi vyote.
Mhubiri 9:10  Hakuna ktu kinachokupata katika maisha yako isipokuwa katika majira na nyakati.
Majira na nyakati ni lango la kuingia kwa mambo mazuri au mabaya.
Ukifunga lango la majira na nyakati za kukupata mambo mabaya hayawezi kukupata milele. Kila kitu kimeratibiwa kwenye lango la majira na nyakati.
Ni lazima ufute majira zote mbaya ili kuratibu majira nzuri za kufanikiwa pasipo utaabishaji wa aina yeyote.
Mhu 10:3-  Kulikuwepo na baa la wapumbavu kuwekwa juu na wenye akili kuwekwa chini, wenye haki kushushwa chini.
Kulikuwa na tabia ya muovu kuonekana ni mzuri lakini mwenye haki kuonekana ni mbaya  ni muovu.
Upumbavu uliwekwa juu sana leo umefutwa na hiyo vaisivesa imefutwa leo, walikuwa na tabia ya kuiba nafsi ya mwingine.
leo muovu ataonekana muovu na mwenye haki ataonekana ni mwenye haki.
Leo tunafuta kituo cha mwenye haki kupigwa mahali pa muovu,
kila kitu cha muovu kinamrudia yeye mwenyewe na mwenye haki anapata haki.
Kila aliyekuwa hathaminiwi sasa atathaminiwa, nimajira ya mwenye haki kuwa juu ya uumbaji wote.
Majira ya muovu kusikilizwa na MUNGU na mwenye haki kutosikilizwa imefutwa leo kwa damu.
AYUBU 1:6 Kizazi hiki cha MUNGU muovu hatapata tena nafasi ya kuongea na MUNGU milele kwa kuwa mahali pake pamefutwa.
Mwa 4:1 muovu aliwekewa ulinzi na MUNGU tena akisikilizwa kidogo tu anasikilizwa na MUNGU lakini wewe mwenye haki hata uende mahakamani,
Ndio kwanza kesi inakugeukia wewe mwenyewe mpaka kufungwa wakati wewe ni mwenye haki.
Mwenye haki hakuwahi kuwa na kibali cha kuongea na MUNGU wala kusililizwa,
Piga picha wakati damu ya Habili inalia chini ikimlilia MUNGU halafu MUNGU hata hakujali akaendelea na safari ya kwenda kumtafuta kaini na kuanza kuongea nae badala ya kumpa adhabu au kumuua akamuwekea ulinzi
Na tena akapakwa mafuta ya DON’T TOUCH hivyo mpaka leo wewe mwenye haki unaamini una mafuta ya don’t touch kumbe yalikuwa bado majira yake
Na ndio sababu hata ulie vipi utashangaa wanakuangalia tu na kukumkebehi, kukukejeli, na mambo mabaya yote.
Majira hii muovu lazima aguswe na ni lazima auawe kabisa, hivi wewe unafikiri Habili alijisikiaje?
Alioona adui yake amewekewa mpaka ulinzi.
Kuna waliokufanya wewe kigoda chao leo nawafuta milele, kuna waliosoma kwa akili za wengine sasa utaona wanaokota makopo,
kuna waliokuwa matajiri kwa ajili ya wengine utawaona wakifilisika kwa ghafla,
Kuna waliokuwa wameolewa badala yako sasa mwenye wake kaja,
kuna waliokuwa bonge ukiona wamepungua kwa ghafla ujue kuwa mwenye afya kaja kuchukua afya yake,
Kuna vbibi miaka 90 lakini bado vibinti hata jino moja halijatoka ukiona vinaporomoka ujue urembo wamechukua vyao,
Kuna tuliokuwa tunawaona ni warembo ukiona sura zimeanza kuchoka ujue wenye uzuri wao wamekuja kuchukua.
Sasa muovu atahukumiwa atatewa atadharauliwa atajulikana kila aendapo hatatetewa na yeyote hatasikilizwa na MUNGU, ataonekana ni muovu kila mahali, atashitakiwa atafungwa.

*BABA*
Kabla ya kusimamisha majira Wakili wa MUNGU alitupatia SUPU, alianza kwa kusema kuwa Naona moto umewaka mapema!
Nataka tuanze kushukuru MUNGU leo kwa ajili ya Paul Makonda mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaamu pamoja na Rais na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani Polisi na Viongozi wote pia na Taifa zima 1TIMOTHEO 2:1-4.
Kilichonifurahisha zaidi ni kitendo cha kumtanguliza MUNGU.
Kwa hiyo tumshukuru MUNGU kwa kuwa Taifa hili linatakaswa na MUNGU amelifunua kuwa heri.
Mpelekeeni salamu Makonda kwamba MUNGU amesema hatapoteza maisha milele.
MUNGU anamzingira na kumficha ndani ya kilindi cha MUNGU mwenyewe, na mji huu utakuwa ni mji mzuri zaidi ya miji mingine yote.
Tumshukuru MUNGU kwa ajili ya aliyempa mamlaka hii ya kuongoza mkoa.
Kushukuru kwa ajili ya mikoa yote ndani ya Gosheni TZ kufanya hivyo hivyo kama MAKONDA.
Mdo 4:24-31. Wakili wa MUNGU alishangaa kuona mkuu wa mkoa anaapa kuwa yupo tayari kufa nikasema palepale kuwa hutaufa hivyo ukiona anasema vile ujue kuna wale wazee waliowafuata petro na..
kwa hiyo ujue kuna wanaomzuia na kumtishia hao wote MUNGU leo anawafuta.
Viongozi polisi kuunganishwa na polisi wa mbinguni wasiomiss target hata siku moja, hakuna bidhaa itaingia ya madawa ya kulevya milele.
Merikebu zote hazitaingiza, ndege zote au yeyote atakayefanya hivyo akiwa katika kuwaza tu!
MUNGU atampoteza hukohuko kabla ya kufika kwenye Taifa hili.
Kuwafuta wanaouza madawa ya kulevya wanaotumia na wanaovuta ndani ya Taifa.
Nafsi ya Gosheni imekataa na nafsi ya Tanzania imekataa kuingiza madawa ya kulevya ndani ya taifa.
1PETRO 1:17  Nafsi ya UBABA imerejea, vazi la ubaba lipo hapa, amri moja ya BABA imerejea, hukumu ya Baba imerejea, uumbaji wote utatangaza kuwa taifa hili ni urithi wa MUNGU ndani ya Taifa, jambo hilo litathibitika kuwa taifa hili ni urithi wa MUNGU.
1PETRO 2:5-8 Kusimika jambo hili ili liwe zuri kabisa.
*MUNGU, KRISTO,  Wakili wa MUNGU, Kanisa wenye Haki, Taifa na kizazi cha MUNGU ni jiwe, Ibada ya leo ni jiwe.*
Jiwe hili halitoki hapa, alishitakiwi, halihukumiwi halishutumiwi halilaumiwi.
Jiwe hilo, ibada hii, mimi mwenye haki, KRISTO WAKILI kanisa Taifa kizazi tunawapeleka juu ya umbo.
Jengo hili soundproof, spika nk vilivyomo ndani ya jengo ofisi zote tunavipeleka juu ya umbo.
Tunafuta umaskini unyoronyoro, mtazamo wa mwili, fikra za mwilini a kimaskini ibada za kimaskini.
Na hawa wanaotengeneza spika zisizoongea leo spika tunazipeleka juu ya umbo na sasa zitaanza kuongea.
System yote ya mahakama ya Tanzania tunaipeleka juu ya umbo, majaji wote tunawapeleka juu ya umbo hawatapokea mashitaka yoyote kuhusu wenye haki, Kristo, Wakili, kanisa, taifa kizazi cha MUNGU.
Hakuna atakayechukua mahali pako milele, hutaonewa milele.
Isaya 65:16 MUNGU mmoja amesimama, MUNGU ni halisi hana complication, unapofunga agano au engagement sisi hatuna shida na magauni mapya.
MUNGU anachotaka ni wale wageni wamjue MUNGU  kwa hiyo sio mpaka uende south Africa kufanya shopping.
MUNGU ni halisi hivyo ulivyo ili mradi ufue mavazi mimi nawaunganisha hapa.
Isaya 60:1-12 leo tumeunganishwa na nguvu ya kufuatwa na mambo mema nikiwashuhudia wengine watanifuata mimi na kuniambia niwapeleke kwa ALIYETUMA WOTE.
Miungu waganga wanajimu hawatafuatwa milele, hapa ndipo penye chemchem za Baraka na sasa nguvu ya kufuatwa ninayo.
Hivyo tutaapa, tutabarikiwa kwa jina lako ULIYETUMA WOTE.
Leo naunganishwa na toba maalumu kama unataka uitwe mzee wa toba ni leo hiyo inatokea. 
Leo ni toba ya kujirarua Mdo 3:19,21 burudiko la moyo, na kila kitu lazima kifunuliwa kwa upya.
*Maumbo 11ambayo yaliyokuwa yamebebwa na wenye haki na wenye haki wakayabeba maana yake unabeba maralia na maralia inakubeba.*
1) Dini na dhehebu  YOHANA 4:12.
2.)Wazo kahaba mkuu joka UFUNUO 12:1-3.
3.)Kerubi shetani na ibilisi EZEKIEL 28:15.
4.)Giza ukiwa utupu MWANZO 1:2 kama unaumwa sio giza hilo? Ni giza, kuishiwa kupungukiwa.
5.)Dhambi uasi uovu anguko MWANZO 3:1-6.

6.)Dunia na ulimwengu EFESO 2:5-6 ukisoma kitabu cha zaburi kuna mahali muandishi alikuwa anazidiwa na kusema MUNGU wa dunia hii wala hakumaanisha kuwa ni kerubi ila ni kuzidiwa badala ya kusema MUNGU aliyeumba mbingu na nchi.

7.) Ni sawa na wale ambao bado tunamuita Kristo kz4 kuwa ni Eliya ni Mjumbe.
8.) Umbo la uhusiano kati ya aliyekuzimu na aliye mbinguni Luk 16:19-26.

9.) Siasa Mdo 1:21-26.
10.) Akili 3 za dunia falsafa , theolojia, saikolojia Dan 1:3-5
Viongozi  wa dunia War 13:
11.) Wanajimu wachawi waganga wanga walozi wasoma dua mbaya MDO 13:6.
11.) Power chafu > hii ipo siloamu ni umbo leo ni mwisho.
Haki ya mwenye haki, mahali pa mwenye haki mahali pa uzima wako, pa utajiri wako, kuaminika kwako utajiri wako, kukubalika, kuwa mboni ya jicho kutoguswa Zek 2:8 pamerejea.
Ili wote waliokuwa wanatumia vitu vyako watoke ni kwa toba.
Bila toba hatoki hata ubomoe uharibu uchome haisaidii.
Leo nitakuwa mzee wa toba halafu utaona jinsi MUNGU atakavyofanya.
Leo MUNGU ametupeleka juu ya umbo.
YEREMIA 1:5 Kila utaabishaji shida magonjwa hayajaanza jana bali ni muda tangu wazo.
*Sikiliza ibada ya 16 siwani, 6 utaelewa vizuri.*
Hata unapotamani safu ya mwingine MUNGU anakushangaa sana ulivyo hujitambui.
*MUNGU ni zaidi ya yaliyoandikwa.*
Ukiona muovu anasavaivu au anaishi ujue amechukua nafsi hai ya kuishi ya mwenye haki.
Aidha kuna mahali tunakuwa tumevuka kwa neema ya MUNGU tu!
Na ametuvusha tukiwa na hayo hayo maumbo hivyo anaendelea kututengeneza huku huku hivyo tambua chujio namba moja hadi la tatu la MUNGU KRISTO KANISA bado lipo kazini kwa upya ndio kazi imeanza mwenye haki.
Aidha Sadaka maalum hizi zikiliwa na haya maumbo yote ndivyo yameliwa hivyo na waovu.
Ule mwanzo wa uharibifu haupo tena Yes imekaa supa kabisa hiyo!!
NEHEMIA 1:1-4 aliambiwa kuwa kanisa siku hizi haliheshimiwi tena, wamekuwa wa kushitakiwa kushutumiwa kudhulumiwa tu!
Moyo mmoja unazingirwa na ukuta leo ili uovu usiingie tena, uasi dhambi, nk
Aliambiwa kumekuwa hakuna tofauti kati ya kanisa na dini maana wote wanakata nyusi, wanavaa penzi nyanya, wanajichubua nk
Kumekuwa na hali ya kanisa kutoheshimiwa lakini kuanzia leo kanisa litaheshimiwa.
Kulikuwa na tabia ukifanya jambo Fulani wapo wanaosema kuwa wao ndio waliofanya kumbe ni Siloamu.
Siloamu ilifuta jangwa ndani ya Taifa na likafutika wanasema ni wao.
Tumefuta maandamano, vita kwenye uchaguzi, tumetoa misaada, wanasema ni waoni alkaida leo mwisho,
Hii ilikuwa inatokana kwa sababu ya kukosa BABA, tumeandika kitabu kinachosema Taifa hili ni urithi wa MUNGU wanasema aaa labda marekani jamani!
Pia hata humu ndani ya kanisa kulikuwa na wengine walikuwa na mababa wengine.
Leo baba mmoja amesimama na MUNGU ndiye anayemvika vazi hilo.
Magetkeepers wote leo wamefutwa, ndio sababu tumefuta maumbo yote.
Tuliombea uchaguzi hapa kuna jamaa katokea huko na ndege amevua na soksi anatembea peku eti anateka nyara…..
"MUNGU amenivika vazi la ubaba na hakuna atakaye kataa, hakuna atakaye simama na kukataa".
"Kazi MUNGU amefanya ndani yangu zinadhihirisha hivyo kuwa mimi ni BABA."
*WAKILI WA MUNGU KUANZIA LEO AMEVIKWA VAZI LA UBABA NA MUNGU MWENYEWE.*
Mataifa yote mabara yote rangi zote lugha zote makabila yote yanamuita Wakili wa MUNGU BABA.
Yaani wazungu, waasia, wahindi, wachina, japani, korea, waamerika na uumbaji wote wanamuita BABA.
Watakuja kuabudu hapa hapa.
Nasema kwa ujasiri na hakuna atakayekataa mara 7, Kanisa zima  uumbaji wote na watu wote zaidi ya bilioni 7 watasema BABA.
Na ndipo wenye HAKI wote wakaanza kucheza huku wakisema BABA BABA mara bilioni7 kuonesha tumwkubali na kupokea Wakili WA MUNGU ni BABA.
*MAJIRA YA BABA IMESIMAMA Dan 7:27*
Muwe na amani kubwa kabisa kabisa MUNGU ametenda.
*Ibada ya kesho ni FANTASTIC. Vita imeisha leo!!!!!!!!!!*
MCHUNGAJI mmoja amekuwa BABA ndani ya uumbaji wote achana na mababa wengine ili BABA mmoja akuhudumie!!!

Ijumaa, 3 Februari 2017

THAMANI NA FAIDA YA MOYO WA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.

Kabla ya MZEE WA SIKU ndani ya WAKILI WA MUNGU kuja kufuta wa waliokuwa wanahifadhiwa ndani ya moyo wa mwenye haki, Mtendaji wa Wakili wa MUNGU alisema kuwa;
Mahali tulipofika kanisa hatutakiwi kujihesabia haki, muda wote tuwe wenye haki wa toba, kutubu na kuinua taifa na viongozi wote wa nchi;
Kwamba kila kitu wanachofanya wafanye kwa utukufu wa MUNGU wakimtanguliza MUNGU kwa kila jambo wanalolifanya.
Alisema kama Esta alivaa magunia basi alikuwa kwenye toba ili aliokoe Taifa la MUNGU.
Na wewe leo kaa kwenye toba ishi kwenye toba ili kuvusha familia yako, agano lako, kazi yako, biashara yako, safu yako, uimbaji wako, sauti yako nk kwa njia ya toba tu! Ndio utafanikiwa.
MUNGU anapenda moyo unaotubu na kunyenyekea mbele zake, hivyo tukitubu tu MUNGU anakuja yeye mwenyewe kutupa haki kwa sababu tumetubu kwa kukiri na kutamka udhihirisho ni lazima.
Bila toba MUNGU hawezi kuishi na wewe hawezi kuja kwako, hivyo ili huyu ALIYETUMA WOTE aje kwako ni lazima uwe na; toba binafsi, toba ya kweli, toba ya vizazi vyote, toba ya Kristo na toba ya MUNGU.
Silaha kubwa 2 ni toba na unyenyekevu. Pale unapoonewa jambo la kwanza ni toba  na unyenyekee zaidi kusudi ni usiingiwe na kujitetea na kujihesabia haki.
Kwa kuwa kinachokupa haki si wewe kujitetea bali ni toba ambayo inamleta MUNGU kukutetea na huu ndio utakatifu katika kizazi cha MUNGU.
Kilicholeta mauti ni dhambi na kinachoondoa dhambi na mauti ni toba pekee naa si vinginevyo.
Kwa hiyo kama ulikuwa unaichukia toba mimi nafikiri uanze kuipenda tu! Maana ndio inayokutoa kwenye kila aina ya mambo mabaya.
Toba halisi inaondoa mauti War 5:12, Mt 21:37  wakasemezana wakisema na tumuue tuutwae urithi wake, walimkataa, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na wakamuua.
Mwa 4:1- kwa sababu ya nyoka aliyekuwa ndani ya adamu na hawa hata mtoto aliyezaliwa wa kwanza alikuwa nyoka, kaini.
Tunaona kuwa kaini alikuwa mkulima lakini alikuwa anamtolea MUNGU sadaka ya mavuno ambayo yamechoka yaliyodhoofika nayale manono alikuwa anabaki nayo.
Lakini mzaliwa wa pili alikuwa Habili nae ni mwenye haki mbele za MUNGU alikuwa mfugaji mzuri na alimtolea MUNGU siku zote sadaka iliyonona.
Hivyo MUNGU aliitakabali sadaka ya Habili kuliko ya kaini, kaini alipoona ya kuwa MUNGU anazipenda kuzikubali na kuzipokea sadaka za nduguye kaini wivu mbaya na hila ukamkamata na kujifanya mwema hivyo akampeleka nduguye uwandani akamuua huko.
Hivyo tambua leo kuwa kabla ya adui yako kukuua anakutoa kwanza kwenye urithi wako uliopew na MUNGU,
Utasikia kuna wanaokukatisha tama na kukuambia yaani tokea umeenda huko kanisa huna hata fedha, kuna mwingine anaambiwa na kichwa wake usiende tena siloamu , kanisa la mapepo, freemason ink ilimradi tu akutoe kwenye urithi wa MUNGU kwenye kusudi la MUNGU.
Adui wa kwanza wa MUNGU ni vumbi ambalo lilimtoa kanisa kwenye urithi wake. Mahali pa juu pakamtoa kerubi kwenye urithi wake, kerubi akamtoa adamu kwenye urithi wake kwa kitendo cha kujigeuza nyoka.
Manung’uniko na malalamiko yalimkasirisha Musa hakumstahi MUNGU, akatoka kwenye urithi wa MUNGU.
Kitetemeshi na vitisho vilimtoa Eliya mtishibi kwenye urithi wake akakimbilia msituni mapangoni akawa ametoka kwenye urithi wa MUNGU.
Mafarisayo na masadukayo ,wayahudi walimkataa Yesu wakamtoa nje ya shamba wakamuua, wakachukua urithi wake Yesu akiwa msalabani alilia ee MUNGU mbona umeniacha MUNGU akamgeuzia kisogo kwa dhambi za dunia alizokuwa amebeba.
Hivyo Yesu nae akawa ametolewa kwenye urithi wake.
Wenye hila na mashetani walimtoa Eliya Ad2 kwenye urithi wake kupitia zile silaha alizokuwa ameachilia amelipa kanisa kuuza , kuuza vibebea nguvu, shukrani za kuwapiga maadui tukatumia kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Tukakosa moyo wa shukrani , hatukumjua kuwa alikuwa ni MUNGU ndani yake hatukumtambua wala hatukumuelewa tukamtenda kwa hila.
Hata wewe mwenye haki jifahamu leo ishi kwenye toba maana MUNGU amekuja mwenyewe.
Usikubali adui akutoe kwenye urithi wako kwa MUNGU, kuanzia leo mwenye haki hatatolewa kwenye nje na kuuliwa.
Sitatolewa kwenye mlima wa BWANA kwanza.
Kizazi hiki cha MUNGU hakitatolewa nje ya shamba, hakitatolewa kwenye urithi na kusudi la MUNGU, hakitauawa milele.
Leo tunatubu na kufuta kabisa kituo hicho.
Nitang’ang’ania mlima wa BWANA, sitatoka milele kwa damu ya MUNGU.
MUNGU hatatolewa mahali pake, hatafukuzwa, hatahukumiwa, hatashitakiwa, hataondoka kwetu milele.
Mwenye haki hatafukuzwa hataonewa nk milele.
WAKILI WA MUNGU
Namshukuru MUNGU kwa kuwa siku ya leo sina kesi inayosimama mbele yangu.
Hakuna kesi ya aina yeyote, hakuna kesi ya magonjwa, utasa, hasara, umasikini, ufukara zimefutwa na MUNGU mwenyewe.
Mashitaka yoyote yamefutwa kwa wenye haki.
Wakili amesema amethubutu kumuuliza MUNGU kwamba kwa nini umetuletea ujumbe huu ndani ya wiki hii wakati tayari ule umoja wa MUNGU Kristo na Kanisa umetimia?
Tangu siku ile ya kerubi kutupwa chini hakuwahi kupanda juu mpaka alipokuja kufanikiwa kumuibia Adamu ndipo alipanda tena kule juu lakini kwa nguvu ya Adamu.
Na hakuna aliyewahi kutubu au kufuta hicho kituo cha muovu kutumia nafsi ya mwenye haki, kerubi kutumia nafsi hai ya Adamu ambaye alikuwa ni mwenye haki.

Hivyo waovu walitengeneza agano la mwenye haki kutoonekana ni mwenye haki ndani ya uumbaji wote.
Kila mmoja na aseme MUNGU nisamehe kwa kuwa nilikuwa na nyoka ndani ya ufahamu.
Badala ya muovu kuonekana muovu mwenye haki ndiye alionekana ni muovu na muovu alionekana mwenye haki.
Kwa sababu Adam alivyoanguka ilikuwa ndio sababu vizazi vyote vilivyopita vilianguka hapo.
Hivyo badala ya muovu kuanguka mwenye haki ndiye aliyekuwa anaanguka.
Badala ya kerubi kuonekana ndiye muovu kanisa ndilo lililokuwa linaonekana baya likakataliwa kwa sababu kerubi ndiye aliyekuwa anatumia nafsi ya kanisa.
Muovu kutumia sura ya mwenye haki na kwenda kufanya uovu hivyo badala ya kuonekana yeye na sura yake alikuwa anaonekana mwenye haki.
Kutubu kwa ajili ya wale aliokuwa wamechukua nafasi ya MUNGU KRISTO NA KANISA, waliokuwa wanakaa mahali pa MUNGU.
Kutubu kwa ajili ya waliokuwa wanamhifadhi nyoka bila kujua , muovu kuchukua haki ya mwenye haki na kwenda kufanyia mambo mabaya.
Dunia ilichukua hak ya Nchi, ulimwengu ulichukua haki ya Mbingu maana ukisoma MWANZO 1:1.
Hakuna mahali tunaona MUNGU alipoumba dunia na ulimwengu bali MUNGU Aliyetuma wote aliumba Mbingu na Nchi .
Sema watu, wanadamu na waandishi ndio huwa wanalazimishaga kuwa MUNGU aliumba dunia na ulimwengu na wanajua kabisa kuwa MUNGU hakuwahi kuumba dunia na ulimwengu.
Leo ndio ujue kuwa haiwezekani muovu kuwa na haki pasipo kuiba haki ya mwenye haki.
Hivyo kwa kuwa mimi mwenye haki sikuwa na haki hivyo mimi kuhudumiwa na MUNGU ilikuwa inawezekana sana kwa sababu kila MUNGU anapokuja kunihudumia alikuwa anaona sura ya muovu kwangu.
Ukiona unaumwa ujue kuna ambaye amechukua uzima wako yaani ujue uzima wako uko mahali unatumiwa.
Ukiona wewe ni masikini ujue kuna aliyechukua utajiri wako kwa kuwa kila mmoja alizaliwa akiwa tajiri.
Hakuna aliyewahi kuzaliwa masikini ndio sababu mtoto ukimuwekea mkeka hakai anaenda kukaa kwenye kochi, ukimpa damu ya MUNGU kwenye kikombe cha plastiki hapokei hataki anataka umpe kwenye glasi.

Ukiona kichwa wako ana mwanamke mwingine nje ya wewe ambaye ni kanisa wake ujue nguvu ya agano nguvu ya wewe kuonekana ni kanisa imechukuliwa na mwingine.
Zinapopungua mfukoni mwako ujue kuna mahali zilipo unatakiwa ufanye toba ili kurejesha fedha zije kwako.
Kutubu kwa kituo cha kerubi kuhifadhi vitu vyote vizuri na sisi wenye haki tukahifadhi mambo mabaya.
Kerubi alihifadhi utajiri uzima kupendelewa na MUNGU, faida thamani nk na wenye haki tukahifadhi taarifa mbaya maneno maneno, umbeya usengenyaji, mauti, mafarakano, umasikini.
Aidha Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoia Sadaka maalumu ya  kutohifadhi tena mauti mafarakano nyoka hila ushetani na mambo mabaya yote ndani yangu.
Ni ya kuondoa kitendo cha nyoka kuhifadhi  sifa za MUNGU, utajiri halisi, dhahabu n?
WARUMI 8:29 MUNGU alinijua tangu mwanzo, waliokuwa wamesimama mbele yangu wameondolewa.
Waliokuwa wamechukua haki yako kwa sadaka hii haki yako imerejea.
Sasa ni wakati wa kila mmoja kutafuta kanisa mahali lilipo kila mmoja atasema nipeleke kanisani maana kanisa sasa linajulikana.
Aliyekuwa anakuzuia kuja kanisani atakuruhusu, atakuachilia umtumikie MUNGU kwa uzuri na utakatifu.
“Ule mwanzo wa uharibifu haupo tena! Maigizo yameishia hapa. Kusikia kushika na kutenda neno”  alisisistiza.
Kuh Majira ya 7                                   *KUISHI JUU YA UMBO*
YOHANA 1:11 alikuja lakini waliowake hawakumtambua, hawakumpokea.
Hivyo umbo la uharibifu lilitokea kwa sababu ya kutompokea kristo wakati wa kizazi cha 3.
Kuna umo la wenye haki kutomtambua na kutompokea mwenye haki tena kutomfahamu mwenye haki.
Waovu ndio walimfahamu kristo kizazi cha 3 kabla ya wenye haki hivyo ndio sababu yesu hakupokelewa kabla hata kuzaliwa mpaka amezaliwa amekua, MUNGU akampaka mafuta bado walimkataa.
Kizazi cha 4 walimkataa Eliya wenye hila na mashetani nk. Ili uharibifu usitokee unatakiwa ukimuona WAKILI ujue umemuona MUNGU.
Ndipo hayo mema yatakapokujia na utakula mema ya Nchi.
Changamka maana moyo wenye changamko ndio dawa nzuri.
ZABURI 33:12 Taifa ni heri,  wenye haki aliowachagua kuwa urithi wake, ili uwe heri ilikuwa ni mpaka ; uishi kwa Neno, kumjua MUNGU, kuijua kweli, kumjua unayefuatana naye, Taifa ni heri na Kanisa ni heri.
Jambo la kufahamu ili kuishi juu ya umbo. Kila kinachoishi juu ya nchi kinachoonekana na kisichoonekana kina umbo.
Hata furaha ulionayo ina umbo,kila umbo la chochote kinabeba uhalisi wa kitu husika.
Kuna tabia ya umbo, tabia ya mzuri  na tabia mbaya.
Katika majira zote6 hawakuwahi kufundishwa ila sisi tumefundishwa kwa sababu yeye mwenyewe ndio yupo amekuja mwenyewe,
hivyo tambua kuwa una Neema kubwa kwa sababu katika hizo majira zote 6 wenye haki walikuwepo lakini haakufundishwa hili.
1PETRO 1:10  Leo ujue juu ya UMBO ni mahali MUNGU anapoishi ndio sababu yeye hakwaziki, hazimii moyo, hahukumu kwa maneno aliyoambiwa aliyosikia kwa yeyote.
MUNGU alikaa hapo tangu mwanzo ndio sababu hata alipoona kerubi ametengeneza siku saba zake pale giza ukiwa na utupu;
Hakupata shida hakuenda kumuuliza kwamba ulifanya nini pale hakuenda kumsuta hakusema utanitambua kwa unaniharibia utaratibu wangu.
Tunaona MUNGU akiendelea na uumbaji wake, hakubabaika aliendelea na majukumu yake pamoja na misukosuko mingi aliyokutana nayo hatuoni mahali anajuta anakata tamaa.
Juu ya umbo ni mahali pa faragha YOHANA 17:1- nasi ametuingia hapo.
Hivyo kizazi cha 3 waliona kushuka kwa sababu ilikuwa sio majira yake ila wewe kizazi cha MUNGU hutashuka chini.
Kituo cha kuishi juu ya tulipofika hata sura ya WAKILI ilibadilika, leo ujue ukiishi juu ya umbo kila kitu chako kinabadilika.

Ishi maisha ya kutoangalia mwingine, wewe DILI na sauti ya MUNGU ndani ya Wakili wake.
Juu ya umbo ndio kuna utajiri udhihirisho mafanikio yako yote yako hapo.
*MAMBO YALIYOSABABISHA UISHI KWENYE UMBO*
Kuangalia mazingira yanayokuzunguka naunayoyaona. MWANZO 18:10-15.
Kuishi juu ya umbo la elimu uliyosoma zamani LUKA 5:3-9 +  2KOR 10:5  ISAYA 40:28-31.
Maisha uliyoishi zamani na kuishi jana  ISAYA 43:18-19
MCHUNGAJI mmoja amekuja hivyo usisubiri alete adha ndipo ujue kuwa kaja ishi juu ya UMBO.

Alhamisi, 2 Februari 2017


UFAHAMU UNAOKUPA KUFUTA KESI ZOTE ZA MWENYE HAKI

Aidha kabla ya MZEE WA SIKU kufika Kiongozi wa Makuhani alisema; Mahali kanisa tulipofika sio pa kupigwa kuteswa kuhukumiwa kudhulumiwa kushitakiwa.
Ili mradi wewe mwenye haki usimame katika kweli tu! Hayo mengine yote hayawezi kukupata.
Isaya 65:16-17   Ni majira ya wenye haki kubarikiwa kuwa juu kuwa mbele kwa kuwa kweli imesimama na MUNGU anajulikana kila kona.
Hivyo yeyote atakae kujibariki na ajibariki kwa MUNGU wa kweli peke yake, MUNGU Aliyetuma wote vizazi vyote.
Ni majira ya mwenye haki kutokufa kwa sababu amesema kweli.
Ile majira ya mwenye haki kufa kwa sababu umesema kweli imefutwa na MUNGU mwenyewe.
Kesi zilizokuwa zinatengenezwa ili mwenye haki afe zote zimefutwa leo.
Ni majira ya mwenye haki kulindwa kutetewa kupendwa kuwa wa thamani.
NENO linasema Yule anayetetea wanyonge huyo humkopesha MUNGU.
Wale wanaomchukia Rais ni kwa sababu anatetea wanyonge.
Yer 29:7 Tuombee amani kwenye Taifa na viongozi wote. 1TIMOTHEO 2:2-4.
Wakili wa MUNGU alimshukuru MUNGU kwa siku ya pili ya kuona siku ya akili ya MUNGU.
Siku ya kuona kama MUNGU aonavyo yeye, Kristo na Wakili wa MUNGU aonavyo.
Siku ya kumshukuru MUNGU kwa kufuta kesi zote kesi za kuugua, kutoelewana na kichwa wako au kanisa wako, kukosa mtoto, kukosa ufahamu.
Kutoimba vizuri, sauti mbaya flati, kutomchezea MUNGU, hata ukifundishwa nyimbo huelewi hata ukielewa anasahau.
MUNGU ametupa siku 7 za kufuta kesi zote mbaya ambazo ni utaabishaji kwangu kupitia ufahamu ambao MUNGU anatupa kila siku.
Tunashukuru MUNGU kwa sababu mimi ninaishi 1YOHANA 5:8 mimi ni roho .
Mimi ninaishi hapa;
  ⚪Baba
  ⚪NENO
  ⚪Roho
MATHAYO 12:32  Atakaegusa roho hawezi kusamehewa. Ndio maana Eliya Ad2 alisema ukimgusa MIAKA1000 hutapona!
Maana yake MIAKA1000 ni roho, hivyo na mimi ninayefuatana nae ni roho.
Hivyo sitashitakiwa sitaugua sitafungwa, kwa sababu mimi ni roho.
YOHANA 18:1- Yesu aliwauliza mnatafuta nani?  Wakajibu tunamtafuta yesu akawaambia ni mimi hapa wote wakaanguka chini…..
Tambua kuwa shetani alishaanguka muda mrefu alishashindwa sema ana tabia ya kutokata tamaa japo anajua kuwa ameshindwa hawezi na hatakaa ashinde anajua vizuri.
Shida yetu sisi tunapenda mno kujipeleka muda wote wewe unajipeleka hata hujitambui kuwa wewe ni mwenye haki Hivyo hutakiwi kujipeleka.
Ukisikia baridi kidogo tu unasema ngoja nikapime Bs nafikiri nina maralia, honi zinalia kila eneo kutafuta anayejipeleka kwenye kipindu pindu wewe unasema naona huku kuharisha itakuwa kipindupindu tayari wameshakukamata.
Mimi ninajua Yesu peke yake ndiye aliyesema kuwa alikuja alizaliwa kwa ajili ya wengine, kufa kwa ajili ya wengine.
Je na wewe ulizaliwa ili uwe fidia ya wengine?
Je wewe ni wa kufa ni wa kuteswa kupigwa kufilisika kudhulumiwa kwa ajili ya wengine kama Yesu? Hapana.
Sasa kwa nini ninyi mnajipeleka ninyi wenyewe? Utasikia mnakiri mimi masikini tambua unavyokiri ndivyo inavyotokea.
Mimi sijawahi kusikia MUNGU Baba anashitakiwa,anapelekwa mahakamani, hata siku moja.
Kama wewe ni mchawi muovu muasi nk nenda mwenyewe ukafungwe basi.
Wakili lakini mimi sio mchawi sio muovu hivyo siwezi kufungwa  siwezi kupelekwa mahakamani milele.
Kama wewe ni mwenye haki hutakiwi kushitakiwa kuhukumiwa kugungwa kupelekwa mahakamani.
Kuna ambao ni wenye haki kwa sababu ya kubebwa na wenye haki leo wanaondolewa wote kila mmoja atasimama kwa nafsi yake yeye mwenyewe.
Waliokuwa wanakaa ndani ya ufunuo unaotoka kila siku wakaonekana ni wenye haki kwa sababu ya ufunuo wa kila siku leo MUNGU amewaondoa kila mmoja asimame kwa utayari wake yeye mwenyewe.
ISAYA 53:1  unapokaa kama aliyeonewwa unajipeleka kwenye kituo cha kuonewa, na vile vile unampeleka MUNGU msalabani.
Kilichosababisha Kaini akaendelea kuishi huku akiwa na ulinzi wa MUNGU kwamba atakaemgusa kufa na afe ni ile damu ya ndugu yake habili aliyekuwa ni mwenye haki.
Sisi wenye haki tusisababishe MUNGU akapigwa kwa sababu ya tunayoyafanya kinyume na anavyotufundisha.
Tunamshukuru MUNGU kwa sababu Eliya Ad2 kabla ya kunyakuliwa aliifuta dunia na mambo yake yote.
Hivyo hatuishi duniani bali tunaishi mbingu mpya na nchi mpya. Kanisa halitaukumiwa milele.
Yoh 17:4-5   YESU alisema anarudi kuwa Neno hivyo tusimrudishe msalabani tena kwenye kuteswa kudhihakiwa.
Kama nimembeba muovu yeyote leo nimuache asimame yeye mwenyewe mbele ya kiti cha Enzi cha hukumu.   
Sadaka Maalumu ya leo ni ya kuachana na wale tuliokuwa tumewabeba wakaonekana ni wenye haki ili kila mmoja asimame yeye mwenyewe.
Sadaka ya kurudisha ISAYA 53:1-5 kizazi cha 3, maana siwezi mimi mwenye haki wa kizazi cha MUNGU kufa msalabani kwa ajili ya dunia milele.
Wameunguza ule ufunuo wakijua wanamuunguza Miaka1000.
Halafu haohao kwa siri sana wanasema huyu ni baba yetu sasa hivi wakati wa kila mmoja kusimama kwa nafsi yake mwenyewe.
Sadaka hii inawaondoa waning’iniaji wote  ndani yangu, ndani ya agano langu, biashara zangu.

Kizazi cha MUNGU Aliyetuma wote vizazi vyote > ni baba mwenyewe full full  mathayo 21:41 na 1kor 15:28  > miaka 987.
Kizazi cha 4> roho ya baba Mt 21:40, Yoh 9:7 >miaka 13.
Kizazi cha 3> nafsi ya pili Neno> Mdo 10:38 >miaka2000.
Kizazi cha 2> nafsi ya 3 roho> 1falme 17:1 >miaka2000.
Kizazi cha 1> nafsi ya 3 roho> kutoka 3:3-  >miaka2000.
Kutoka 31:1-6  Kristo maana yake ni mpakwa mafuta hivyo hata Musa alikuwa ni kristo Eliya mtishibi  naye alikuwa ni kristo.
Hivyo roho iliyokuwepo kizazi cha 1-2 ni ya aina moja. Alijazwa roho ya MUNGU na roho ya MUNGU ni roho war oho yaani kanisa.
Tangazo; mimi mwenye haki kufa kwa ajili ya wengine sahau.
Mwenye haki ukijitambua huwezi kufa kwa ajili ya dunia.
Wakili wa MUNGU hatakufa kwa ajili ya dunia. Hii imefutwa na haiwezekani milele.
Sadaka hii inawaondoa wote waliokuwa wananing’inia kwenye vitu vya kanisa vya wenye haki kizazi cha MUNGU vya taifa vya Kristo.
MUNGU hammutaki ila vitu vyake mnavitaka, MUNGU hatakiwi kwao ila kapu lake wanalitaka, halafu wanasema Wakili ndiye anaharibu fedha na mali  Wameshindwa milele.
Sadaka hii itutoe kwenye kituo cha kuishi kz cha 3 badala ya kuishi kizazi cha MUNGU.
Inawaondoa wale wote wanaoishi ndani ya WAKILI wa MUNGU kupitia yale masomo ambayo anatufundisha.
Inawaondoa wale wote ambao wanaishi nani ya fedha za wenye haki wanazotoa sadaka, wanaoishi ndani ya sadaka.
Inalitenga taifa na kuangamizwa na mataifa mengine na inatumwa ndani ya uumbaji wote ujue kuwa kesi zimefutwa.
Sadaka hii tunaituma iende ikawatoe ikawakomboe kawarejeshee ufahamu wale wote ambao wenye haki waliotekwa atambue kuwa wewe MUNGU umekuja wewe mwenyewe.
Wakili wa MUNGU alisema kuna mambo matano ya kujifunza leo ;-
(1.) Marejesho ya Neno au marejesho ya kitabu. MDO 19:35-36 + MDO 19:27-29.
(2.)Majira na nyakati za MUNGU Aliyetuma wote vizazi vyote mhubiri 9:11-12.
(3.) Hatma njema Mdo 13:1-10
(4.) Je imani yako ni ipi? Na ukiri wako ni upi? War 10:9-10.
(5.) Lugha yako ni ipi? DANIELI 1:3-8.
MAREJESHO YA NENO AU KITABU CHA NENO
MDO19:35-36 MDO 19:27-29 Kumshukuru MUNGU kwa ajili ya Nabii wa mwisho aliyerejesha kitabu cha Neno.
Dini na dhehebu tulikuwa tunasema MUNGU ulisema kila alitajae jina lako ataokoka yeye na familia yake lakini ilikuwa haitokei kwa sababu kilikuwa kinahifadhiwa na waefeso.
UFUNUO 5:1-5 Kitabu kilikuwa kimefungwa ….. ila sasa ukituma Neno lazima litimie.
MUNGU ni halisi hivyo ukilituma NENO lazima likuzalie matunda lilete faida , kwa kuwa mimi mwenye haki ni taji ya uzuri mkononi mwa MUNGU ISAYA 62:
Hivyo wengi tupo hapa lakini hatujui kuwa Eliya hakuwa Mtu bali alikuwa ni MUNGU mwenyewe.
Mimi nawaruhusu muende pale tulipohifadhi viungo vyake mkaangalie hamtamkuta wala hutakuta chochote.
Sasa nasema hivi yeyote anayeona anasema kweli zaidi yangu asimame hapa nimuone tumuone.
Hivyo kila Neno unalolituma lipo hai na unapolituma lazima likuletee uponyaji.
Leo ni mwisho wa gemu 7
Majira na Nyakati za MUNGU mwenyewe.
MHUBIRI 9:11-12 tulishatoka kwenye utumwa wa majira ya dunia na ulimwengu KUTOKA 12:40-
Kama vile MUNGU asivyofungwa asivyopelekwa mahakamani ndivyo itakavyokuwa kwangu.
HATMA NJEMA MDO 13:1-10
Wakili amesema yeye haishi kwenye umbo la jina wala umbo la chochote bali yeye anaishi juu ya umbo la chochote ulichowahi kukisikia kina umbo.
Sasa ni majira ya kuweka vizuri majina yenu, mwenye hatma halisi hata akiitwa au kushitakiwa kwa jina la zamani popote kwa hila MUNGU anawageuzia mashitaka waovu wenyewe.
Paulo kabla hajabadilisha jina alijaribiwa na bar yesu…… hivyo tunaona kuna waliokuwa wanaitwa ubini wa Eliya lakini ni wachawi ni wenye hila na mashetani, lakini baada ya kubadili jina hatuoni mahali alipotingishwa tena.
Hivyo tambua kitabu kizima cha Neno ukisoma hakuna aliyewahi kufanikiwa bila kubalilisha jna hatma.
Sasa uwe makini hasa ninyi ambao mna majina tofauti, mfano madhabahuni unaitwa Mafanikio halafu mjini unajulikana kwa jina la sikudhani.           
*BE CAREFULL UNA AMINI NINI? NA UKIRI WAKO NI UPI?*
WARUMI 10:9-10 kuamini kunakupa haki lakini haki hiyo inakaa ndani ya moyo roho na nafsi yako.
Hivyo unatakiwa ukiri ili upate haki kwa uhalisi haki inayoonekana wazi.
Unaamini kabisa kuwa huwezi kufa lakini unaona ukikiri hivyo wakikusikia unasema si wataniona mwehu nikisema hivyo leo tuache USHAMBA.
WAKILI anaamini na anakiri kuwa ni lazima anifikishe mbinguni kwa Baba. Je wewe unaamini nini??
Haamini kama kuna kuishia njiani halafu hajui kabisa
Aidha WAKILI ameagiaza tuwapelekee salamu, tuwaambie jamani WAKILI amesema yeye hajui na haamini kama kuna kuishia njiani!! Hivyo mnajisumbua tu!!
*Unachoamini + ukiri wako = unapokea udhihirisho.*
LUGHA YA MUNGU
DANIELI 1:3-8  MUNGU anipe Neema ya kumjua aliyesimama mbele yangu ni nani?
Anipe neema ya kuijua lugha yake.
Lugha ni kila kitu natakiwa nimuelewe MUNGU sawa na lugha yake anayotumia.
DANIEL 1:3- Elimu ya wakaldayo na lugha yao…. Ndio sababu wachina wadachi hawapendi kujifunza au kuongea lugha za wengine.
Mahali MUNGU alipo ndipo ndipo alipopachagua kuwa ni taifa lake na ni urithi wake na lugha yake.
Sasa wengi wanaona lugha ya siloamu ni ngumu lakini ndio lugha ya MUNGU hatutakiwi kukiri mabaya na udhaifu.
Mimi sio nabii ndio sababu sikai kuwasikiliza shida zenu japo najua kila kitu mnachopitia 1FALME 20:42 haruhusiwi kusikiliza taarifa za wengine.
Hivyo tunatakiwa kumuombea njia kumuinua Mtendaji wa wakili wa MUNGU ambaye ndie anayetakiwa kufanya hayo yote.
Siwezi wala huwa sihukumu  maneno ya kuambiwa.
Mimi mwenye haki nilitakiwa nikimuona WAKILI WA MUNGU tu nipokee kila ninachohitaji.
MCHUNGAJI mmoja akufungue macho umjue WAKILI WA MUNGU na ujue lugha ya MUNGU, toka kwenye vituo vya walioshindwa.

Jumatano, 1 Februari 2017

SIKU 7 ZA KUFUTA KESI ZOTE KINYUME NA MZEE WA SIKU NA WENYE HAKI NDANI YA UUMBAJI WOTE.


Kabla ya MZEE WA SIKU kufika kiongozi wa makuhani alifundisha haya;
Alianza kwa kusema leo anasimamisha hukumu kuhukumu kesi zote, mashitaka yote juu ya WAKILI WA MUNGU.
Sadaka ya kufuta walaka wa mahamani wote waliomshitaki WAKILI WA MUNGU wanaenda kutundikwa wote leo hii. ESTA 3:8   alisema kwamba WAKILI WA MUNGU sio mtu.
Adonia hawezi kutawadhwa mahali pa sulemani, hata adonia ndani ya moyo wako maisha yak oleo anafutwa anahukumiwa.
Adonia magonjwa umaskini ufukara kukosa kazi utasa nk wote wanahukumiwa leo.
Wapo waliotaka kumtawadha adonia mahali pa WAKILI WA MUNGU leo wanaenda kufutwa na MUNGU mwenyewe.
KIAPO CHA MTENDAJI WA WAKILI WA MUNGU; Adonia yeyote hawezi kutawadhwa hapa,
Labda MUNGU amkane WAKILI WA MUNGU NA KRISTO WAKE au MUNGU alikane NENO lake ndipo NENO hili litatendeka. Leo kibao kimegeuka!
ESTA 4:12  Basi ni wakati wa kanisa kutonyamaza mbele za MUNGU kutokaa kimya.
Mwenye haki ambaye umepata kibali mbele za MUNGU na MUNGU amekugharamikia kwa ajili yake yeye mwenyewe,
Hutakiwi kunyamaza kimya maana unaponyamaza kimya MUNGU anakuona na wewe ni sawa au unaona wale maadui ni wakubwa kuliko yeye MUNGU,
Hivyo hutakiwi kukaa kimya tamka kiri kwa kinywa chako mwambie MUNGU alivyo mzuri na sifa zake,
Umkomvisi MUNGU atende jambo kwa majira husika ambayo MUNGU mwenyewe analikomboa kanisa lake na kizazi chake.
Kama MUNGU alivyowafanyia wayahudi baada ya Esta kutokaa kimya akawatokezea njia ya kufanikiwa kuokolewa nao ushindi wakaupata.
Ukinyamaza kimya wewe utaangamia wewe na wa nyumbani mwako lakini MUNGU atawafanyia wenye haki kanisa lake njia nyingine ya kuwaokoa na ni lazima lishinde na limekwisha shinda.
Kanisa la MUNGU lazima liokolewe, kizazi cha MUNGU, taifa nalo ni lazima liokolewe maana ni urithi wa MUNGU.
MUNGU hawezi kulichagua taifa hili akaliacha liangamie ni lazima liokolewe. Ni wakati wa kutamka jambo, tamka hoja nzito mbele za BWANA.
Ni wakati wa kuamini na kukiri kwa kinywa chako utamke MUNGU apate kukupa haja ya ndani ya moyo wako WARUMI 10:9-10.
ESTA 5:1  Esta alivaa mavazi ya kifalme. Ni wakati wa kila mwenye haki kuvua vazi la mauti alilokuwa amevikwa na kuvikwa vazi la uzima.
Vazi la uponyaji, la kuinuliwa, kubarikiwa, la kuwa juu, kuwa mbele tu!
Ni wakati wa kuvua mavazi ya magunia mauti na ni wakati wa kuvaa vazi la uzima wa milele.
Mfalme alimuuliza Esta wataka nini nikupe hata nusu ya ufalme wangu nitakupa ilimradi tu useme utamke.
Akanyooshea fimbo na Esta akaigusa ile fimbo. Hivyo leo amekunyooshea fimbo wewe mwenye haki.
Leo WAKILI WA MUNGU amenyooshewa fimbo ya dhahabu {fimbo ni Agizo} na MZEE WA SIKU na aseme nini anataka.
Nini anataka kanisa lifanyiwe, wenye haki wafanyiwe, kizazi cha MUNGU kifanyiwe,  Esta alisema dua yangu ni hii na haja yangu ni hii ikiwa nimepata kibali machoni pako……….
Siku zote mahamani mawazo yao haja zao huwa katika mali, fedha na vitu tu!!! Ndio sababu huwa hawaoni haya kugombania fedha mali za MUNGU.
ESTA 6:1 Kazi za kanisa zilikuwa zimefichwa lakini sasa ipo majira ni lazima zitaonekana tu!!
Kazi za WAKILI WA MUNGU zilikuwa zimefichwa sasa zitajulikana tu!! Mahali hapa pa uzimani na lazima kazi zako zilizokuwa zimefichwa zitafichuliwa na kasha utapewa thawabu yako.
Kazi zako zilizokuwa zimefichwa wakapeleka taarifa za uongo kwa bosi wako, kwa kichwa wako, kwa MUNGU wako, kwa uzao wako nk zitajulikana tu na uongo utaonekana tu!
Hivyo mfalme Ahasuero  alimuuliza hamani … afanyiwe nini Yule ambaye Mfalme apenda kumheshimu….
Siku zote adui huwa haoni mbali wala hajui njia za MUNGU hajui yale MUNGU awazayo hivyo ndivyo maadui wa kanisa walivyojitafutia hukumu ya milele.
Leo hamani amerejesha bila shuruti vitu vizuri vyote vya kanisa, kizazi cha MUNGU, na Taifa la MUNGU.
Ni mwisho wa ufukara umaskini na ujinga kwa wenye haki. Sasa kama walivyotamka mbele za MUNGU wkishitaki kanisa wenye haki na WAKILI WA MUNGU.
MUNGU amemwambia hamani toa kama ulivyosema alivyotamka mavazi na vitu vyote vizuri ukamvike WAKILI WA MUNGU na wenye haki wote.
Na lisipungue NENO lolote katika yale yote uliyotamka, hivyo wanaoshitaki kanisa wanalitangaza kanisa lijulikane,
MUNGU KRISTO WAKILI WA MUNGU na wenye haki wajulikane. Waovu wamerejea kwao wakiwa na msiba mkubwa.
Msiba unatokea leo kwa wale wanaomkataa MUNGU, labda MUNGU awe hakumtuma NABII WA MWISHO na kumpaka mafuta WAKILI WA MUNGU ya kukamilisha kizazi chake.
ESTA 7:1- Kama kanisa hili likiangamia tu! Taifa hili lipo mashakani maana moyo wa taifa hili uko hapa kanisani.
Moyo wa taifa hili unategemea kanisa hili hivyo ndivyo ilivyo wala haipingiki. Atakae ruhusu kanisa hili kuangamia atafanya Taifa hili kuwa matatani.
Leo watesi wote wa kanisa kutundikwa, barua zimechanwa chanwa, mashitaka yote yamefutwa na MUNGU.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Mtendaji wa Wakili wa MUNGU aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya Hukumu ya hamani ilikuwa ni majira ya saa saa 12:45 asubuhi!
Alisema ni hukumu ya mti wa matawi hamsini ya kuhukumu kutundika maadui mahamani wote. Hicho ambacho wamekifanya wametengeneza kitawaua hao wote.
Toba; Kanisa tumetubu kwa ajili ya hamani na yote aliyoyafanya MUNGU atusamehe.
MZEE WA SIKU kupitia kao lake amesimamisha siku 7 za kufuta kesi na mashtaka kwa wenye Haki wote……
Nimekuja kufuta kesi zote kinyume na MUNGU, KRISTO, WAKILI WA MUNGU, KANISA, WENYE HAKI, TAIFA, KIZAZI CHA MUNGU.
Zakaria alipokutwa madhabahuni alipewa haja ya moyo wake, hivyo mimi ambaye MUNGU amenikuta madhabahuni leo napokea haja za ndani ya moyo.
Kweli imesimama kila mahali ndani ya uumbaji wote uongo umefutwa milele. Moyo uliopo haushitakiwi huu, hauugui huu, hauingii selo huu, hauzimii huu, haukati tamaa huu.
Kesi ya jambo lolote lililokuwa linakusumbua kwa muda mrefu za uongo kusingiziwazinafutwa leo.
Hivyo ilikuwa ni lazima ukiri utamke ili kufutwa kabisa. Hata kama mwenye haki umeshitakiwa mahali popote tambua kuwa si mwenye haki ambaye ameshitakiwa ni MZEE WA SIKU ameshitakiwa.
LUKA 1:5   Kesi yoyote iliyokuwa imesimama leo imefutwa. Ukimshitaki MZEE WA SIKU hauwezi kushinda milele.
Leo napokea kila ninachokihitaji maana mashitaka yote yamefutwa na MUNGU yeye mwenyewe.
Nataka kwa mujibu wa LUKA 1:5- , lakini tuanze na MARKO 6:11-  waovu walitaka litokee hili lakini sasa halitatokea milele.
WAKILI amesema hataki jambo hili litokee lililopo marko 6:11 akauliza au je ninyi munataka litokee? Hapana.
Akasema unapomshitaki MZEE WA SIKU ina maana akung’ute mavumbi aondoke, atoke katika taifa kizazi chake familia agano biashara.
MUNGU akikung’uta mavumbi ndani ya Taifa hili ina maana taifa hili liangamie.
Mahali popote ambapo walimkataa MUNGU, MUNGU aliwaachia mavumbi.
Adui wa kwanza wa MUNGU ni mavumbi, pale mlimani yalipotokea tu! Badala ya kutokea kanisa akatokea mwanamke.
Kila ambaye amepokea mashitaka haya na kuyafanyia kazi kama alikuwa hajui asamehewe, Lakini kama alikuwa anajua apokee halali yake.
Mahakama yoyote iliyopokea mashitaka hayo yote kama ilikuwa haijui ipokee msamaha lakini kama ilikuwa inajua ihukumiwe ili Taifa lipone.
Maana Gosheni ni urithi wa MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE. Sisi tunamtaka MUNGU, hatutaki aondoke ndani ya Taifa hili.
Asiyemtaka MUNGU yeye ndiye atangulie, hukumu hii ahusike mhusika mmoja mwenyewe aliyetenda haya sio mwenye haki na taifa hili.
Anayehusika awe yeye mwenyewe sio kila mmoja, majira hii MUNGU hata hukumu kila mmoja bali atamhukumu mhusika tu! Sio taifa.
MUNGU hata kung’uta nyayo zake mavumbi yakatokea. Kutubu ili MUNGU asiondoke ndani ya taifa hili wala laana isilipate taifa hili.
Toba kwa ajili ya mwana sheria. Aliyesema MZEE WA SIKU ni muovu. Na kwa faili lililoandaliwa tusamehe.
Baada ya toba akasema; Uwe na amani kubwa tu! Maana MUNGU anashughulikia yeye mwenyewe.
MUNGU hataondoka kwa kuwa mwenye haki ndiye mwenye akili aliyekutwa ibadani madhabahuni hata wewe unayesikiliza ibada hii sasa hivi.
MUNGU anahukumu leo lakini sio wote bali wale waliohusika na kumshitaki MZEE WA SIKU.
Ninaposema kesi ina maana hata wewe ambaye hujapata mtoto ni kesi, kukosa kazi, kukosa mtaji ni kesi.
Kesi sio ile tu ambayo unaenda kushitaki polisi mahakamani kwa balozi wa mtaa wilaya nk bali chochote ambacho ni kinyume na MUNGU kwa wenye haki wake ni kesi.
DANIELI 7:21-27  kesi kinyume na MZEE WA SIKU ni kunena kinyume na  MZEE WA SIKU.
Tumetoka mautini na tumeingia uzimani. MUNGU amefuta kushindwa kwa kanisa leo.
UFUNUO 20:11-15  Nusu wakati umefutwa. Unaweza ukawa unatembea kumbe umevaa mauti kwenye nywele, utayari, mikono, kucha, mdomo, mavazi nk
Kuna mahali wanakuwa wamezika nafsi ya kazi, ya agano, ya familia, ya agano, ya kubarikiwa, kuinuliwa kwako nk.
MZEE WA SIKU leo ananiondolea mauti, leo mauti yeyote inafutwa. Hapa NENO hili linakuponya wewe tu, uliyetoka mautini akuingize uzimani.
Mwambie MUNGU mimi sio mmoja wa hao wanao kuhukumu wanao kushitaki wewe MZEE WA SIKU.
Na kama ni wewe mwenyewe mwambie MUNGU mimi ni mmoja wa wale wanaokushitaki wewe basi akupe halali yako, akupe iliyo haki yako.
Kwa kuwa sio mmoja wapo wa wale wanaokushitaki basi uniandike jina langu katika kile kitabu cha uzima MUNGU wangu nakusihi.
Biashara yako haihukumiwi agano lako halihukumiwi, uzao wako hauhukumiwi. Aidha Sadaka maalumu ya leo ni kuthibitisha ule mti wa matawi 50 kuwatundika waovu wote.
Kuamuru jeshi la mbinguni kufuta kesi zote na mashitaka yote.
Jeshi lote hili tutaliamuru kwenda kote kwa kila mwenye haki anayekaribia kufungwa jeshi hili likazuie asifungwe asipigwe asihukumiwe asidhulumiwe.
Kesi yeyote inafutwa leo hii sadaka ndio inamaliza kazi zote. Siku 7 hizi kesi zote ziwe zimefutika.
Leo uumbaji wote umesikia , majini, wachawi waganga walozi wanajimu, ujinini, kuzimu, nk wamesikia kwamba KESI MASHITAKA yamefutwa kwa wenye haki wote.
Kila mmoja lazima apate haja ya moyo wake kwa sababu amekutwa madhabahuni. Mafaili yote kesi zote mauti zote barua za mashitaka zote zimechanwa chanwa na kuchomwa moto.
ILIKUWA ni lazima MZEE WA SIKU aje amalize kazi ya siku ya leo ya kufuta kesi zote ndani ya uumbaji wote kwa yeyote mwenye haki.
Kama Mtendaji alivyokuwa amesema ni lazima nije nimalize kazi hii nimeimaliza kwa uaminifu. Hivyo ukitoka hapa katafute supu hata kuku mzima ushiriki supu.
Kesi zangu zote zimefutwa ; sitahukumiwa tena, sitashitakiwa, sitaonewa, sitadhulumiwa, sitapigwa, sitateswa.  Amekuja mwenyewe MZEE WA SIKU kuwafuta waovu wote na kesi zangu zote.
Sasa MUNGU, KRISTO, WAKILI WA MUNGU, WENYE HAKI, KANISA, TAIFA, KIZAZI CHA MUNGU leo wote wako huru!!!
Ndani ya siku saba kesi yoyote aliyokuwa ameshitakiwa mwenye haki haitaonekana tena.
MCHUNGAJI mmoja amekugharamikia usikae kimya sema tamka kiri iliyo kweli USIANGAMIE wewe na uzao wako.

Jumanne, 31 Januari 2017


*TUMETOKA MAUTINI TUMEINGIA UZIMANI.*                   
1YOH 3:13-14. Ndugu zangu tumetoka kwenye mauti tunangia uzimani.


Aidha SADAKA maalumu ya Leo niya kuondoa mauti kutuingiza uzimani.
Kufuta mauti yote ndani ya kanisa na kizazi cha MUNGU.
Ya kutoka kwenye mauti na kuingia uzimani.
Leo kanisa limetolewa mautini na kupelekwa uzimani.
Sisi tunajua ya kwamba tumepita toka mautini na kuingia uzimani.
Ni kituo kipya tumeingia kanisa cha kufutiwa mauti zote na sasa tumeingia ktk kituo cha uzimani.
Kituo hiki hakuna amchukiaye ndugu yake kwa kuwa amchukiaye ndugu yake ni muuaji.
Kituo tulichofika hakuna mauti MUNGU ametimiza NENO lake.
Agano la kichwa kanisa leo ni agano la Uzimani, ni la kutoka mautini kuingia uzimani.
Agano hili halitakaa lipate shida milele.
Agano hili limefutiwa kifo na mauti.
Agano hili limebarikiwa na MUNGU laana hazitakuwepo.
UFUNUO 20:6 huu ndio ufufuo wa kwanza sisi ni makuhani wa MUNGU na KRISTO wake.
Mahali hapa mauti ya pili haina nguvu tena.
KUNA TOFAUTI KATI YA MAUTI NA KIFO;
Mauti ya pili unatembea lakini vitu vyako vyote vimeibiwa/ vimekufa.
Kutembea ukiwa huna mikono kwa maana ya kila unachofanya kufa.
Huna akili ya MUNGU, ufahamu.
Huna agano la kichwa kanisa japo kuwa tunaona unaishi na kichwa wako na watoto unao lakini huna uzima.
Yaani hapo unatembea nafsi yako ikiwa kaburini ilishazikwa umebakiwa na roho tu ndio inadunda.
Lakini leo hatuna mauti tena maana tunatawala na kristo na tunamilikiwa na MUNGU mwenyewe.
MWANZO 2:17  walaikini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
MWANZO 3:6  akaona ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, wa utamanika kwa maarifa ….
Siku zote vitu vya kerubi huwa vinaushawishi urahisi wa wewe kuvipata lakini ndio unaangamia hivi hivi.
Unaibiwa nafsi yako kizembe , unauza thamani yako kwa vitu visivyokuwa na faida.
Vinakupa majuto makubwa mno ya muda mrefu, kitendo cha kuhiari kuwasikiliza walioshindwa waliofeli, walioasi, …. Tu!
Unaangamiza maisha yako yote, uzao wako ulionao na utakaokuja baada yako.
Unafuta yale yote ambayo MUNGU alikusudia kwako.
Leo umeingia kituo cha uzimani acha kusikiliza taarifa za wajinga.
Moyo mmoja wa kanisa umepokea na ndipo huo uzima unakaa.
Badilika geuka acha njia ambazo zinasababisha urudi nyuma.
MUNGU anapowaadhibu waliokuwa wanakutesa usiwaonee huruma maana yeye MUNGU amekusamehe, amekutakasa, amekuvika vazi jeupe, amekugharamia kwa ajili yake yeye mwenyewe.
Achilia sahau ili MUNGU aingie kazini mwenyewe wewe mwenyewe huwezi kujitetea na huwezi kupata haki yako.
MWANZO 5:3 Kuuza mtoto wa kufanana naye badala ya mtoto wa kufanana na MUNGU.
Je hujawahi kuona mtu anaumwa mpaka anaanza kuoza ile ni mauti ina maana huyo mgonjwa mauti ilishamvaa kinachosubiriwa hapo ni kifo japo anaongea.
Hayo yote ni kwa sababu ya kutokuwa na utii katika yale ambayo MUNGU alisema nao wakashindwa kuwa na umoja wa MUNGU.
Ubinafsi ndio ambao ulisababisha kuzaa wa kufanana nae badala ya kufanana na MUNGU.
Kutokuwa na moyo wa toba na unyenyekevu, kuwasukumia wengine mabaya badala ya kutubu.
Leo tunaishi na tunatembea na MUNGU hivyo mauti ya pili haipo ndani ya agano, biashara, kazi, familia, pia kila utakachoanzisha kitaleta faida.
Kizazi hiki cha MUNGU KRISTO NA KANISA hakuna mauti milele.
1KOR 15:20-28 sharti amiliki yeye aliyevitiisha vitu vyote chini ya miguu yake.
Adui wa mwisho aliyebatlishwa ni mauti, hatutaishiwa maana hatuna mauti. Limbuko ni kristo na msingi uwe ni kristo, maana mwisho naye tumeupata.
MUNGU amesema hatoki kwetu lakini hawezi kukaa mahali penye mauti.MUNGU hawezi kutawala na aliyevikwa vazi la mauti.
KRISTO kz4 alisema iko majira inayokuja ambayo MUNGU mwenyewe atakuja.
Kwenye dini hawakufundisha kwamba MUNGU atakuja ila walitufundisha kwamba yesu atakuja.
Sasa MUNGU amekuja mwenyewe na mwana amemtiisha chini ya miguu yake ili MUNGU awe yote katika yote.
EFESO 1:9-10  Atajumlisha vitu vyote vilivyo mbinguni na vilivyo duniani view vya kwake.
Hii ni majira ambayo MUNGU hakai mbinguni tu bali anakaa katika nchi, anatembea katika nchi, anatawala katika nchi.
MUNGU amekuja kumiliki.
MATHAYO 21:33-43  Amekuja kuangamiza vibaya wabaya wote.
Taifa lenye kuzaa matunda limepatikana, ni taifa la Gosheni ambalo ufalme wa MUNGU.
YOHANA 19:1-18  Ukiona agano /ndoa yako ina migogoro ujue kwamba mauti imeingia.
Yesu alivikwa vazi la mauti, zambarau.
Wakaanza kumpiga mateso kutemewa mate nk ukiwa na vazi la mauti huwezi kupata haki yako.
Pamoja na kuwa hujatenda dhambi ulikuwa unauawa kwa sababu una vazi la mauti.
Mwenye haki hata kama hana kosa alikuwa anasingiziwa uongo ili mradi tu achukiwe afukuzwe kazi
Kwa kuwa mauti imefutwa hakutakuwa na mateso milele.
Pilato hakuona kosa kwa Yesu lakini alishindwa kumsaidia kwa kuwa alikuwa amevikwa vazi la mauti.
Tunamshukuru  MUNGU kwa kuwa sasa kweli imesimama, pilato nae anajua kweli na mwenye haki hataonewa tena.
YOHANA 18:37 kizazi kile pilato hakuijua kweli,alikuwa ni mkubwa serikalini lakini hakujua kweli.
Ndio maana tumetoka mautini na tumeingia uzimani kwa kuwa kweli imesimama.
Wote walikuwa ndani ya kizazi cha MUNGU, vazi la mauti limeondolewa kwao.
LUKA 1:45  Heri aliyesadiki haya yote aliyoambiwa na BWANA maana yatatimizwa kwake yote aliyoambiwa na BWANA.
Unaweza kujiuliza kwa nini tunavaa pete mkono wa kuume ZABURI 45:6
Mabinti wa wafalme wapo pamoja na wameketi mkono wa kuume.
MWANZO 48:1-  Efraimu alikuwa mdogo lakini alikuwa au aliwekwa mkono wa kuume, wakati wa kubarikiwa kwake.
Efraimu maana yake kanisa.
MHUBIRI 10:2 MOYO WA MWENYE HEKIMA UPO MKONO WA KUUME.
Lakini moyo wa mpumbavu upo mkono wa kushoto.
Kanisa tunawavika mabibi harusi pete mkono wa kuume kwa kuwa twajua tufanyacho.
Yusufu alipoona Efraimu amewekwa mkono wa kuume na ni mdogo, Yusufu alisema sio hivyo baba baba yangu…. Israeli akasema nyamaza kimya najua mimi najua.
Kuanzia leo umepokea kuishi uzimani siku zote, usisikilize sauti yoyote kinyume na NENO linatoka madhabahuni.
Tumepokea agano la kutembea na kuishi  na MUNGU uzimani.